Dr. Slaa alikuwa anaongoza Kwa 61.6% - Marando | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa alikuwa anaongoza Kwa 61.6% - Marando

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Superman, Nov 3, 2010.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Source: Mwanahalisi: Jumatano, Novemba 3-9, 2010

  NEC inatuhumiwa kuhujumu matokeo ya Uchaguzi kwa lengo la kukinyima ushindi CHADEMA.

  Madai hayo yamo katika barua ambayo CHADEMA kiliwakilisha jana NEC kulalamikia utaratibu mzima wa kutangaza matokeo.


  Katika barua hiyo, Mwanasheria wa CHADEMA, Mabere Marando anasema NEC inatumiwa na CCM kuhujumu matokeo hayo ili CCM kionekane kinashinda. "Wamepanga kupora ushindi wetu, ndiyo maana kila ambapo CHADEMA imeshinda, CCM wamekataa kusaini karatasi za kura" alisema Marando.


  "Hata pale ambapo kura za madiwani na wabunge zimetangazwa, matokeo ya kura za urais hayatangazwi". Marando alisema NEC inafanya hivi kwa makusudi kwani maeneo ambayo CHADEMA haikuwa imeweka mkazo, matokeo ya madiwani, wabunge na ya urais yanatangazwa haraka . . . .


  . . . . . Lakini hata katika maeneo ambayo CCM imeshinda, Marando alisema matokeo yanayotangazwa na NEC hayaendani na yale yaliyotangazwa vituoni. "Huu ni Uchakachuaji". . . .


  . . . . . Marando alisema hadi juzi Jumatatu matokeo ambayo tayari walikuwa wamekusanya kutoka katika maeneo mbalimbali ya Nchi, yanaonyesha Mgombea Urais wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa anaongoza kwa wastani wa asilimia 61.6%..


  Aidha taarifa hizo zinasema Dk. Slaa amepanga kuwakilisha ushahidi MZITO unaoonyesha uchakachuaji mkubwa wa kura za Urais ulivyofanyika. Ushahidi huo ni pamoja na matokeo halisi ya vituoni ambayo yanapishana na yale ya NEC.


  Hatua zilizochukuliwa ni:


  1. Kwenda NEC - kupeleka barua

  2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi
  3. Tunakwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea kwa kuwaonyesha ushahidi kamili.

  Malalamiko haya yanakuja siku chache baada ya lori lililoingia nchini likitokea zambia kukamatwa mjini Tunduma likiwa limesheheni karatasi za kupigia kura zilizowekewa alama ya vema kwa Kikwete. NEC ilikanusha.


  Lakini katika kituo kimoja cha kupigia kura wilayani Musoma, lilikamatwa Lori lililokuwa na karatasi za kupigia kura na tayari zilikuwa na zimewekewa alama ya vema upande wa Kikwete. NEC haikutoa maelezo kuhusu tukio hilo.


  My take:

  Kama hizi taarifa ni za uhakika, basi hakuna maana ya zoezi zima la uchaguzi na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania. Bahati mbaya mshindi wa Urais akishatangazwa, huwezi kuupinga ushindi huo mahakamani.

  Ni vema sasa jumuiya zote za kiraia zinazotetea haki za kidemokrasia na za binadamu, wanachama na wapenzi wote wa haki na wana CCM wanaokerwa na hili kupaza sauti zao na kupinga kwa nguvu zote uzandiki huu. Arusha, Mbeya, Mwanza, Kawe, Ubungo na Iringa wameonyesha njia.

  Inawezekana, mambo mazuri yana gharama na si lazima gharama hiyo iwe ni kumwaga damu bali kupaza sauti na kukataa kutawaliwa na watu ambao watanzania hawajawachagua kwa haki.
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pasco (member wa JF), Umesoma alichosema Marando?

  Chadema wamefuata process kama ilivyotakiwa........... good
   
 3. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Wanaofaidika na haki ni wengi lakini wanaoitafuta hukutana na mengi. VIVA SLAA
   
 4. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,292
  Trophy Points: 280
  Swali moja rahisi ambalo NEC wangelitolea maelezo ni hivi...kwanini matokeo ya URAIS yalikuwa hayatangazwi sambamba na yale ya Udiwani na uBunge ilihali uchaguzi ulifanyika pamoja? Ninajua hata mtoto ''bright'' wa darasa la tatu anaweza kukupatia jawabu sahihi - CCM walijua kilichowapata na kwa bahati mbaya sana hawapo tayari kukubaliana na maamuzi ya wananchi walio wengi.

  Nadhani kuna haja ya kuongea na wafadhili haraka ili haya matokeo fake yasimamishwe mara moja na uchaguzi wa Rais ufanyike upya.

  Bila shaka Kiravu na Makame wameshatishwa na bila shaka wanafanya yale wanayoyafanya kwa amri kutoka juu
   
 5. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Wabunge majimbo 30 kati ya 200 plus na urais eti asilimia 61, give me a break! Kama huko si kuchakachua kwa mezani sijui utaita nini?
   
 6. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  tuko pamoja wanamageuzi... viongozi wanamageuzi mtuambiwe siku ya kuandamana na kuikomboa nchi yetu...
   
 7. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Ukisoma sheria za uchaguzi zinasemaje utapata jibu.

  Matokeo yote yanabandikwa vituoni kuanzia udiwani, ubunge mpaka urais. Kata inatangaza matokeo ya diwani, wilaya matokeo ya mbunge na NEC makao makuu matokeo ya rais.
   
 8. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,292
  Trophy Points: 280


  Hatua number 3 (kuonyesha ushahidi kamili wa kile kilichotokea) ingeunganishwa na zile mbili za juu. Lazima NEC wajue kwamba watu wameshtuka na wanajua kwa uhakika kila kinachofanyika. Wale wafadhili wetu ambao Mkwere anashinda huko na bakuli lazima nao wajue ukweli
   
 9. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,292
  Trophy Points: 280
  Kwa nini hayatangazwi kituoni wakati wanayabandika kituoni
   
 10. O

  Orche Senior Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  But the National Electoral Commission chairman rejected the idea.
  "There could be irregularities in terms of arithmetic in the vote tallying, but not enough to change the final results," Lewis Makame is quoted by the Reuters news agency as saying" Source BBC

  Hayo ni maneno ya Jaji Lewis Makame kuthibitisha kuwa matokeo wanayotangaza siyo yaliyotangazwa vituoni. Ni ajabu kwa Jaji kufanya vitukama hivyo halafu utegemee kupata haki mahakamani.
  Inauma sana, Mungu saidia Tanzania.
   
 11. r

  rastaman Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shule Jamaa wamekwenda. si mbumbumbu kama kiwete. hiyo ndo njia.
  there is not freedom without cost. let us free ourselves from ccm oppression.
  Change never by siting and singing we will overcome. change costs. dare not how much will cost us. w
  we need respect: ccm must respect the decision of millions of Tanzanians who decide to go for change.
  Katika historia ya dunia nzima hakuna mageuzi yaliyokuja bure bure tu!! kuwa namageuzi ya kweli lazima tukubali cost yoyote itakayo tupata. nawapa mfano mzuri mdogo.. wazanzibar iliwacost 2000 leo hii wanaheshimiana. wakenya 2007 ilwakost leo hii kuna utulivu. Kwa hiyo ndugu zangu tusife moyo. tusiogope vitisho. haki utafutwa, haki hupiganiwa. hata damu ikimwagika, lakini wajue kuwa ni hao hao Kikwete na wenzake ambao watakuwa chanzo. lete the world see. let the world witness and know that Kikwete is the DICTATOR:
  huko anakojivunia kuwa watamsaidia wakuuwa watanzania, nako kumesha gawanyika. tutapata support kubwa mno. Kila mtanzania aliye na macho ya kuona na masikio ya kusikia ameyaona na amesikia jinsi gani kikwete na wenzake ambao wanajiita wasomi lakini bado wanatumika kukandamiza haki za watu. hii ni Karne ya 21. lazima ujue hivyo baba. soma maandiko, ujue alama za nyakati. Watanzania tujue kuwa hata French revolution haikutokea tu. they paid for it.
  Watanzaia tuamke.
   
 12. C

  CCM Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rasta! Na Botswana, Namibia iliwacost nini? Huko kwenye utulivu bila kumwaga damu. Tusiige mifano isiyofaa. Na mbona mifano yako imelala hapa hapa tu? Japan, Australia na Uswisi imewacost nini kujenga amani. Fikiri kama mtu mzima.......AMANI KWANZA
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,445
  Trophy Points: 280
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,445
  Trophy Points: 280
  riziwani umekujahuku ?karibu sana
   
 15. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mabere haya yasiishie Tume tu. Wao ndo wahalifu twategemea wajikosoe? Ifunguliwe kesi mahakamani na mahakama iombwe kutoa amri ya kusitisha zoezi ovu linaloendelea mpaka haya yapatiwe majibu. Tukichelewa wakatangaza imekula kwetu. Tupo pamoja??
   
 16. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Ukitaka serikali ya kiafrika/kifisadi ishike adabu, dawa ni moja tu vikwazo vya uchumi. Na hasa kunyimwa misaada, mikopo na kufungiwa kwenda ughaibuni kwa viongozi wake wakuu. Chupi zitawabana tu.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  The whole thing was a farce and its too bad chadema has in essence no meaningful legal recourse
   
 18. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Mkulima acha upupu. Huko Kyela na Kigoma Slaa alikataliwa wagombea wake wa ubunge. Lakini akaahidiwa kura za uraisi. Pia kuna jimbo moja Chadema wamelichukua, lakini wamepata diwani mmoja tu, wakati CCM wamechukua kata zilizobaki kama nane hivi au zaidi.
   
 19. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa ndugu yangu...
   
 20. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  popcorn.gif

  Very good CHADEMA, very good.
   
Loading...