chiute2005
Member
- Feb 26, 2009
- 7
- 0
CCM walijua watu wanawapenda ndio maana walikuwa na jeuri hata ya kuwatukana wapigakura lakini walipoona matokeo ya kura wakashituka. Tukumbuke mwanzo matokeo yalipoanza kutolewa na vyombo vya habari waandishi waliopo maeneo husika walitangaza matokeo ya ngazi ya urais, ubunge na udiwani kama walivyotangazwa na wasimamizi. Baada ya CCM kuona mgombea wao anapitwa kwa zaidi ya asilimia 50-70 ( e.g. songea kikwete alipata kura kati ya 36-50 wakati Dk. Slaa alipata kura kuanzia 120 na kuendelea karibu kwa kila kituo cha kupigia kura) wamevipiga marufuku vyombo vya habari kutoa matangazo ya matokeo ya urais.
Shime watanzania wakati wa kuwaondoa mafisadi umefika
Mikakati katika bunge hili
1.kufuta na kubadilisha muundo Wa Tume Ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), kwa kumuondolea Rais madaraka ya kuteua Mwenyekiti na wakurugenzi wa Tume, bali mapendekezo ya majina matatu yawe yanawasilishwa bungeni na kuthibitishwa na bunge. Na bunge lipewe mamlaka ya kuwafukuza kazi na sio Rais
2. kufanya mabadiliko ya katiba kwa kufuta vyeo vya Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa kwani ndio wamekuwa vibaraka wa ccm kuhakikisha kushinda kwa gharama yoyote ikijumuisha kuchakachua matokeo
3.kufuta utaratibu wa mtu kuwa mbunge ndipo awe na sifa ya kuteuliwa kuwa waziri. Bali nafasi za uwaziri ziwe zinagombaniwa kwa mfano wa ubunge, anayeshinda ndiye anakuwa waziri katika eneo analolichagua. Hii itaongeza uwajibikaji. Pia idadi ya wizara, mawaziri na manaibu mawaziri wa serikali inayofuata iwe inaidhinishwa na bunge kabla ya uchaguzi au baada ya uchaguzi.
4.kuwaondoa wakurugenzi wa halmashauri kuwa ndio wasimamizi na watoaji wa matokeo ya uchaguzi kwani hawa wanateuliwa na rais na kwa vyovyote vile hawawezi kukiuka maagiza ya rais. Bali wakurugezi wa NEC watakaidhinishwa na bunge ndio wawe wasimamizi na ndio watangaze matokeo ya uchaguzi(tujadili ili kujua idadi yao iweje)
5.kurekebisha sheria, ili kuruhusu vyombo vya habari kutangaza matokeo ya uchaguzi kama yalivyotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo husika,
6.kuweka masharti ya kutoajiri wastaafu katika Tume Ya Uchaguzi. Sababu kubwa ni kuwa uwezo wao wa kufikiri kwa haraka na kutoa maamuzi ni mdogo sana na hawana uwezo wa kusimamia ukweli.
7. Kuweka ukomo wa mtu kuwa mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume kuwa misimu miwili ya miaka mitano mitano
8. Ujumulishwaji wa matokeo ufanyike katika maeneo ya wazi ambapo kila mtu ataona, teknolojia hapa inaweza kutumika ili kuondoa malalamiko, hili liwe moja ya takwa la msingi la kisheria. mfano Marekani kila matokeo yalipotangazwa katika kituo cha kupigia kura yalionekana wazi katika screen/tv ya Tume ya Uchaguzi pasipo wao tena kuhitaji kutangaza.Hata walipojumulisha na kutangaza mshindi wa jumla hakuna aliyeyakataa matokeo kwasababu yalikuwa wazi kwa kila mtu na walijua nani ameshinda hata kabla Tume haijamtangaza mshindi.
9.Tuangalie na maeneo mengine yenye mianya ya ufisadi na uchakachuaji wa matokeo na kuona jinsi ya kuziba mianya hiyo kitaalamu
Bila haya kufanyiwa kazi ushindi kwa upinzani itakuwa ni ndoto na mwishowe tutakuwa kama wakenya na wazimbabwe, Mungu atusaidie tusifikie huko, maana inanitisha ninapoona watanzania waliokuwa wapole na waoga kwa vyombo vya dola sasa wanaweza kupambana na vyombo vya dola hadi vyombo vya dola vinakimbia na kujificha- rejea vurugu zinazoendelea kwenye majimbo ya uchaguzi ikijumuisha ya kibaha mjini