Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameweka bayana kwamba chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakitashiriki mdahalo wa wagombea Urais wa upinzani hapo kesho.

Kiongozi huyo aliyekuwa anasubiriwa na mamilioni ya Watanzania kwenye mdahalo huo ametoa sababu kubwa mbili kwa chama chake kutoshiriki...

Sababu ya kwanza ni kwamba CHADEMA bado haijampata mgombea Urais na mchakato wa ndani unaendelea.

Na sababu ya pili ni kwamba Ilani ya chama bado haijapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho na itakuwa ni kichekesho kwenda kwenye midahalo bila kuwa na Ilani ya chama.

Dr Slaa amesema chama hicho kitakuwa tayari kushiriki midahalo ya aina hiyo mara taratibu za kumpata mgombea Urais zitakapokamilika ndani ya chama!

This is really rational !
 
Siyo wagombea urais ndiyo wanaokwenda kwenye mdahalo, bali viongozi wa upinzani kujadili mchakato wa urais, inawezekana wewe hujui kinachoendelea kuhusiana na huo mdhalo huo

Dr Slaa ndio Mwenyekiti wa Chadema?
 
Teh Teh Agano jipya na Mdahalo wapi na wapi?
 
CCM wameshafika zaidi ya 30, tuone kama CHADEMA baada ya Slaa atajitokeza mtu mwingine, akijitokeza unikate kidole.
Itakuwa jinai akikukata kidole bora atumie kidole chake kukukata kimba!
 
Nafikiri Ali Mufuruki amepoteza focus na mantiki ya mdahalo, mwanzoni nilifikiri huu ni mdahalo wa watia nia ngazi ya uraisi, sasa Dr Slaa, ZZK na Dr Makaidi hawajatangaza nia hiyo, sasa wanaitwa kwa malengo yapi? Wajadili kuhusu nini?! Confusing! ZZK na Dr Makaidi nasikia wametia nia kwenye ngazi ya ubunge sasa mdahalo wa Ali Mufuruki unawahusu nini!? Ndg Ali Mufuruki please fafanua kama ni member wa JF.
Bavicha mna vichwa vigumu sana!
 
Teh Teh Slaa ana muogopa sana Zitto sishangazwi na kukimbia mdahalo!
 
Mdahalo utakaorushwa kesho kuanzia saa 1 hadi saa 4 na Azam Tv unaoandaliwa na CEOrt chini ya kiongozi wao Ally Mufuruki, Dr Slaa amesema wao hawatashiriki Mijadala mpaka watakapomaliza kura za MAONI ndani ya chama.

Washiriki ni prof Lipumba CUF, Zitto Kabwe ACT, Dr. Slaa CHADEMA na Dr. Emanuel Makaidi NLD.

safi sana hongera chadema,huwezi kuwa pambanisha matumla na taisoni,zito ni matumla dr slaa ni taison
mwandaji wa mdahalo hajui kuandaa midahalo,angetakiwa awe anangalina saizi zao saizi ya zito ni salumu mwalimu au mtatiro hivi vitu vinaitifaki zake,nawashauri wana ukawa wenzetu kama cuf wamtume kijana wao ndio akanga ongee na zito na sio profesa
 
Soma heading ya huo mdahalo unahusu nini? kama sio wagombea Urais, Je CHADEMA wamemtaja mgombea wa Urais wao. Dr.Slaa katoa jibu sahihi na makini kwamba CHADEMA Bado hakijapata mgombea wa Urais lakini kubwa la muhimu Ilani ya chama bado haijapitishwa akienda kuongea anaongea yeye kama yeye au malengo yaliyowekwa na chama, Hao waendesha midahalo wasiwe na mihemko kam EL! wasubiri wagombea watajwe ndipo mdahalo ufanyike wanaharaka ya nini Kama nikuelezea masuala ya kitaifa wasiweke heading za presidents astraints? Na hao waendesha midahalo waliweka tu mtego kama Dr.Slaa angehudhuria inamaanisha kwamba yeye ndiye tayari mgombea wa CDM wakati Mkutano mkuu haujatoa jina la mgombea.
 
Sasa wew unataka kusema nin , kwani makaidi, zitto wapi amesema anagomea uraisi
Kwa kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanataka kuwasikia wagombea uraisi na sio hii midahalo isiyokuwa na mbele wala nyuma. Personally, hii midahalo ingesimamishwa kwani haisaidii bali inapunguza uzito wa midahalo ya wagombea hapo baadaye. Sasa wakishajadili kama sio wagombea itasaidia nini? Hapa zaidi watajadili watu badala ya hoja. Waachwe wagombea waje wajieleze wenyewe. Hii TV watafute program nyingine kama nia yao ni kutangaza biashara ! Hivyo, kudos to Dr. Slaa for his excellent and brilliant decision. Presidential material ni lazima usiwe cheap and Dr. Slaa is the one.
 
Hvi hawa wanaoandaa midahalo hii wnajua wanachofanya kweli au wanatafuta umaarufu tu! Toka mwaka 2010 hadi leo sidhani kama wameandaa mdahalo wowote. Leo kwa sababu ya uchaguzi tu ndio na wao wanaibuka. Kama kweli wao ni professional wa midalo mbona walikimbia tangu 2010 na kuwaachia UDASA peke yao? Halafu wanajua kabisa kwamba sasa hvi vyama bado vpo kwenye mchakato wa kupata wagombea na pengine kuweka sera zao sawa. Sasa unawaita kwenye mdahalo wakaongee nini kama siyo umbea na kurushiana matusi tu.
 
..nadhani Dr.Slaa yuko sahihi.

..Dr bado hajachukua fomu wala kupitishwa na chama chake kugombea Uraisi. Sasa angetokea ktk mdahalo huo angekuwa amekiuka taratibu za chama chake ambazo yeye ndiye msimamizi wake mkuu.

..Mufuruki angesubiri kwanza wapatikane watangaza nia wa CDM,CUF,NCCR,na NLD, ndipo aandae mdahalo wake.

..kwa kifupi, Mufuruki ameonyesha uchanga ktk kuandaa shughuli hii. kitu cha msingi anatakiwa kufanya kazi na vyama husika, na zaidi kuzingatia ratiba za vyama hivyo.

..sijui kwanini Mufuruki hakujifunza kutokana na makosa aliyoyafanya ktk kuandaa mdahalo wa wana-CCM. Mdahalo ule ulikosa washiriki kwasababu wengi walikuwa ndiyo kwanza wamechukua fomu na wako busy kutafuta wadhamini.

cc Kapwela, Alinda, Zakumi, Mkandara, Nguruvi3
Katika hili hata miye nakuunga mikono, Ali Mufurika angefanya Mjadala tu kama ilofanyika jana Maria Sarungi na Omar Ilyas walipokutanishwa bila upambe. Huwezi kuandaa Mdahalo wa viongozi wagombea Urais halafu ukaalika wote wasiogombea Urais kasoro mmoja tu. Ni Uchizi mtupu..
 
IKULU NI MAHALI PATAKATIFU sio pango la wala rushwa,sio kila mtu hata mafisadi papa wanataka kukimbilia kuingia,CDM wana adabu na wanapaheshimu IKULU
CCM wameshafika zaidi ya 30, tuone kama CHADEMA baada ya Slaa atajitokeza mtu mwingine, akijitokeza unikate kidole.
 
Mi nawashauri waandaa midahalo wawaalike watalaamu mbalimbali wa maendelo na uchumi waongee kuhusu mstakabali wa taifa letu. Nini kifanyike ili tusonge mbele! Kwani midahalo lazima wawe wanasiasa tu! Au wandaa midahalo wamekariri kwamba ili uwe mdahalo lazima washiriki wawe wanasiasa? Think out of the box!
 
Naupongeza uongozi wa chadema kushtukia mchezo mchafu uliokua umeandaliwa. Kwani walidhani dr angekurupukia mdahalo, nadhani pia walipanga na wema sepetu siku moja awe uso kwa uso na Dr slaa kwenye mdahalo.
 
Mdahalo wa urais alfu anashirikishwa zitto ambae kikatiba hana vigezo
 
Mdahalo wa urais alfu anashirikishwa zitto ambae kikatiba hana vigezo...upuuuzi huuu
 
Katika hili hata miye nakuunga mikono, Ali Mufurika angefanya Mjadala tu kama ilofanyika jana Maria Sarungi na Omar Ilyas walipokutanishwa bila upambe. Huwezi kuandaa Mdahalo wa viongozi wagombea Urais halafu ukaalika wote wasiogombea Urais kasoro mmoja tu. Ni Uchizi mtupu..

..inaelekea jamaa hana uzoefu kabisa.

..katika hayo maandalizi inatakiwa afanye kazi kwa karibu sana na timu za kampeni za wagombea husika.

..jambo la kwanza kabisa ni kuzingatia RATIBA za wagombea. sasa inaelekea huyu mwenzetu yeye anataka wagombea wafuate ratiba yake vile anavyowapangia.

..halafu pia hata haelezi huo mdahalo utahusu nini. kwenye nchi za wenzetu tumezoea kunakuwa na midahalo inayohusu masuala ya ndani, na mwingine unahusu foreign policy.
 
..nadhani Dr.Slaa yuko sahihi.

..Dr bado hajachukua fomu wala kupitishwa na chama chake kugombea Uraisi. Sasa angetokea ktk mdahalo huo angekuwa amekiuka taratibu za chama chake ambazo yeye ndiye msimamizi wake mkuu.

..Mufuruki angesubiri kwanza wapatikane watangaza nia wa CDM,CUF,NCCR,na NLD, ndipo aandae mdahalo wake.

..kwa kifupi, Mufuruki ameonyesha uchanga ktk kuandaa shughuli hii. kitu cha msingi anatakiwa kufanya kazi na vyama husika, na zaidi kuzingatia ratiba za vyama hivyo.

..sijui kwanini Mufuruki hakujifunza kutokana na makosa aliyoyafanya ktk kuandaa mdahalo wa wana-CCM. Mdahalo ule ulikosa washiriki kwasababu wengi walikuwa ndiyo kwanza wamechukua fomu na wako busy kutafuta wadhamini.

cc Kapwela, Alinda, Zakumi, Mkandara, Nguruvi3

Nilishangaa mdahalo wa watia nia Dr. Slaa na Zitto ni waalikwa. Hivi ni lini na wapi Dr. Slaa au Zitto ametangaza nia??
Kwa Prof. Lipumba ni sahihi maana yeye ameishatangaza nia.

Kwa hili ninamuunga mkono Dr. Slaa.
 
Hilo nitatizo huyu Dr.Slaa ameitwa kwenye mdahalo kama kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya chama chake sasa anachokikwepa ni kitu gani?
kwani kwenye hizo sababu mbili alizozitoa mbona ni sababuless,haziusiani kabisa hii ni kuonyesha kwamba hiki chama kwasasa hakina watu wenyeuwezo.inamaana mpaka tarehe ya leo chama hakijapata mikaka ya kuwaeleza watu....ajabu.
 
Back
Top Bottom