Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

mkigoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
1,180
Reaction score
309
Mdahalo utakaorushwa kesho kuanzia saa 1 hadi saa 4 na Azam Tv unaoandaliwa na CEOrt chini ya kiongozi wao Ally Mufuruki, Dr Slaa amesema wao hawatashiriki Mijadala mpaka watakapomaliza kura za MAONI ndani ya chama.

Washiriki ni prof Lipumba CUF, Zitto Kabwe ACT, Dr. Slaa CHADEMA na Dr. Emanuel Makaidi NLD.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameweka bayana kwamba chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakitashiriki mdahalo wa wagombea Urais wa upinzani hapo kesho.

Kiongozi huyo aliyekuwa anasubiriwa na mamilioni ya Watanzania kwenye mdahalo huo ametoa sababu kubwa mbili kwa chama chake kutoshiriki...

Sababu ya kwanza ni kwamba CHADEMA bado haijampata mgombea Urais na mchakato wa ndani unaendelea.

Na sababu ya pili ni kwamba Ilani ya chama bado haijapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho na itakuwa ni kichekesho kwenda kwenye midahalo bila kuwa na Ilani ya chama.

Dr Slaa amesema chama hicho kitakuwa tayari kushiriki midahalo ya aina hiyo mara taratibu za kumpata mgombea Urais zitakapokamilika ndani ya chama!
 
Amefanya jambo la maana lenye faida kwa Chadema.kila la heri raisi wetu mtarajiwa.
 
subirini aseme kwanza, na zitto anagombea urais wa nchi gani?
Siyo wagombea urais ndiyo wanaokwenda kwenye mdahalo, bali viongozi wa upinzani kujadili mchakato wa urais, inawezekana wewe hujui kinachoendelea kuhusiana na huo mdhalo huo
 
Back
Top Bottom