Sio Zitto pekee hata Dr.Slaa na Makaidi sio wagombea Urais.. Hivyo ingekuwa mjadala tu kila mtu aangushe sera maana swala sio la UCHUMI tu nchi yetu ina madudu mengi sana toka Udini, Ukabila, Ukanda na kubwa kuliko yote RUSHWA..Mdahalo wa urais alfu anashirikishwa zitto ambae kikatiba hana vigezo
Epa,Richmond ,Escrow wahusika wake wapo chama gani?
..nadhani Dr.Slaa yuko sahihi.
..Dr bado hajachukua fomu wala kupitishwa na chama chake kugombea Uraisi. Sasa angetokea ktk mdahalo huo angekuwa amekiuka taratibu za chama chake ambazo yeye ndiye msimamizi wake mkuu.
..Mufuruki angesubiri kwanza wapatikane watangaza nia wa CDM,CUF,NCCR,na NLD, ndipo aandae mdahalo wake.
..kwa kifupi, Mufuruki ameonyesha uchanga ktk kuandaa shughuli hii. kitu cha msingi anatakiwa kufanya kazi na vyama husika, na zaidi kuzingatia ratiba za vyama hivyo.
..sijui kwanini Mufuruki hakujifunza kutokana na makosa aliyoyafanya ktk kuandaa mdahalo wa wana-CCM. Mdahalo ule ulikosa washiriki kwasababu wengi walikuwa ndiyo kwanza wamechukua fomu na wako busy kutafuta wadhamini.
cc Kapwela, Alinda, Zakumi, Mkandara, Nguruvi3
Bado kama miezi minne ya uchaguzi lakini chama hakijapitisha ilani hadi mida hii.
Sasa amekimbia nini? kwani Slaa alisema anagombea urais?
Sioni umuhimu wa mdahalo huu wakati wagombea wa upinzani na wa chama tawala bado hawajapatikana.
Jokakuu:
Nadhani Maruruki anataka kutengeneza pesa haraka haraka kwa midahalo na sio kutumia nafasi hizo kufahamisha umma. CCM pekee yake ina wagombea utitiri. Kwanini asingesubiri mpaka kura za maoni zionyeshe nani wenye uwezo na angechagua watano kati yao?
Kuhusiana na wagombea wa CDM, CUF, NCCR na NLD, kama wapo kwenye UKAWA na wanatarajia kumtafuta mtu mmoja, kwa maoni yangu inabidi wawe na protocols za kuwasaidia kumpata mgombea na vilevile kuheshimu protocols hizo. Sioni kama midahalo itawasaidia.
...............heading za presidents astraints?.............
Ni mgombea wa kudumu, hana mpinzani.