Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

majibu ya dr.slaa nimeyakubali na yana logic nadhani waandaaji wa mdahalo wangekuwa na subira. harakati ya nini?
 
Kumbe Dr Slaa ametulia! Nimefurahi kusoma kumbe yeye hajachaguliwa/kuteuliwa kugombea nafais ya uraisi ndani ya chama chake, na ingekuwa makosa yeye kushiriki kwa kudhani angeliweza kuwa moja wa wagombea. Nachelea lakini isije ikawa naye hataki kuwa mgombea....yaani itoshe tu basi aonyeshe NIA!
Dr Peter Slaa Rais wa mioyoni mwa watanzania. Hapo ndipo ninapoipenda hekima yake!! Mazumbukuku kama ZZK yangekimbilia kutafuta misifa lakini Dr Mnyenyekevu ka nini sijui!
Dr ndiye hasa rais anayetufaa!! hata wakati aliposhinda aliombwa hakukurupuka na mitamaa!! Asingekuwa na subira tungeogelea kwenye dimbwi la maji mekundu saa hizi.
Dr WP SLAA ni Rais wa tano wa JMT trust me!!
 
Wakuu,
Chama dola wajanja sana ukipitia vizuri sheria ya uchaguzi utajua kwa mini hats Lowassa alikataa kushiriki.Luna watu wanalengwa na wataenguliwa siku za mwisho kama uchaguzi was serikali za mitaa walivyofanyiwa CDM. Hivyo wadau bila mihemko ya vyama tuangalia sheria za uchaguzi zinasemaje MTU anaopotangaza nia mambo gani hapaswi kufanya mpaka kipindi cha kampeni. Huu utitiri was wachukua form ccm pia in tactics imetumiwa na ukichunguza sana walioandaliwa hawana mbwembwe na trend take inaonekana. Chama dola kinauwezo was kushawishi màmuzi vyama pinzani angalieni sana. Chama dola kina uwezo was kuharibu uchaguzi pale wanapozidiwa mbinu upinzani hamuwezi.
 
Kwa sasa labda midahalo ya siala zima la BVR na mchakato wa kuandikisha wapigakura, tukishapata wagombea ndipo tuwahoji waombaji. or mdahalo uwe ndani ya vyama mf. ccm kwa ccm wapewe mdahalo, the same for ukawa wakishachukua wote form na kutangaza ndipo nao wafanyiwe mdahalo
 
Mi nawashauri waandaa midahalo wawaalike watalaamu mbalimbali wa maendelo na uchumi waongee kuhusu mstakabali wa taifa letu. Nini kifanyike ili tusonge mbele! Kwani midahalo lazima wawe wanasiasa tu! Au wandaa midahalo wamekariri kwamba ili uwe mdahalo lazima washiriki wawe, wanasiasa? Think out of the box!

Kwanza hao wanasiasa watazidi kutueleza uongo juu ya mstakabali wa uchumi wa nchi yetu kwasababu za mbio zao za kuelekea ikulu. Waitwe wataalamu wa uchumi ktk hiyo midahalo ili wananchi pamoja na hao wanasiasa tuweze kuiona nchi yetu imejikwaa wapi na nani atatufaa kuiinua tuelekee mbele. Siyo hawa walioshiriki kuifikisha hapa ilipo ndo waende tukawasikilize katika hiyo midahalo, tuwaachie majukwaa ya siasa waogelee hadi wachoke.
 
Kama slaa hajatangaza nia kwa nini umualike subiri basi achukue hata form ya kugombea
 
Zitto ni Mgombea Urais?Katiba inamruhusu?Huyo Mafuruki angeuita Mdahalo wa Wenyeviti wa vyama vya siasa labda ila sio Wagombea Urais,kama ni wagombea Urais Zitto hana sifa hizo kinachofanyika anataka kuleta fujo tu ndiyo maana wengi wanaamini Zitto anatumika,Hongera Dr Slaa kwa kukwepa Mshale.
 
Mleta mada unapotosha.Ni wazi kwamba waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi upande wa upinzani ni Prof Lipumba tu,waliobaki ni wagombea kutoka CCM,sasa unawezaje kusema Dr Slaa amekimbia mdaharo unaowahusu wagombea uraisi wakati Chadema hawajamtangaza mgombea wao?,Mbona haihitaji degree kuelewa hilo?
 
Bora amekimbia:sly:😱😕😡🙄😛🙂😉😎😀😱:what:🙁:banghead:
 
..I agree with u.

..hata kwenye ule utitiri wa CCM angeweza kutafuta wachache ambao anaona wana-potential.

..makosa aliyofanya ni kuwashtukiza wakati wamechukua fomu na wako ktk harakati za kutafuta wadhamini.

..muda huu ambapo wanarudisha fomu na kabla CCM-CC haijakaa angeweza kuwapata wachache akafanya nao mdahalo. I believe wako ambao watakuwa na hamu ya kushiriki.

..kuhusu UKAWA inabidi asubiri kwanza mpaka wapatikane watia nia ktk vyama vinavyounda umoja huo ndipo aandae mdahalo.

* Sioni kama ni sahihi kama yeye angeamua kuwaengua wengine kwenye mdahalo wa watia nia wa CCM. Mdahalo ungepoteza mantiki kwa umma..

* Kwa siasa ya Tanzania ilivyo hawezi kuendesha mdahalo wa watia nia wa chama kimoja..kwani watia nia hutegemea ilani ya chama kutoa hoja ya sera na mipango..

* Haileti maana mdahalo kuwa kati ya UKAWA na ACT kwani ACT haishirikiani nao...kwahiyo mdahalo baina ya vyama unatakiwa ushirikishe hadi CCM...Chukulia mfano, kuwa na mdahalo wa CCM na ACT mda huu..

* Kwa upande wa CCM mdahalo hauwezekani kwahiyo asubiri mgombe wake apatikane..kwa upande wa upinzani, aandae mdahalo wa UKAWA anaweza kufanikiwa. Baada ya hapo aandae mdahalo mkuu wa wagombea Urais CCM (Atakaeteuliwa), UKAWA (Atakaeteuliwa), ACT n.k
 
Nadhani sababu aliyoitoa ni ya msingi. Mdahalo ni wa wagombea urais. chadema bado hawajaanza kuruhusu wanachama kuwania urais. Atashiriki kama nani?
Wangeelwa unachosema, tatizo shule!
 
Huyu ccm kweli, sasa anakwenda kufanya nini Ikulu au ndo kwenda kutuendesha kwa maoni ya 1st lady??? Nchi yetu haina viongozi
 
Hongera Dr kwa maamuzi mazuri.
Pia siku nyingine tuna kuomba usihudhurie midaharao inayorushwa na tv isoyokua na coverage kubwa hapa nchi mdahao unakua wa kibaguzi, sie wakulima hatuona na kusikia mdahalo ilihali tuna hamu ya kukusiki Rais wetu, tunaomba pia utangaze nia muda ukifika.

Kwa wandaaji wajitahidi kurusha midahalo kwene tv zenye coverage kubwa kama ITV maanaipo kwene ving'amuzi vingi.
 
Back
Top Bottom