Dr. Slaa afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

Dr. Slaa afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

katika saikolojia tunasema kwamba mtu unapomzungumzia adui wako kila mara ina mana kwamba bado ana thamani katika maisha ndio maana hata ulipogombana nae umeshindwa kujizuia kuishi pasipo kukzungumzia

pia tunasema kwamba kila unapo mzungumzia adui yako ndivyo unavyo zidi kushuka chini kimawazo maana utakuwa hautoi mawazo ya kusaidia Taifa utakuwa kila mara unatengeneza bomu la kumuangamiza.

Unavyomzungumzia sana adui yako ndivyo unavyozidi kumpa kick na kuutesa moyo wako pale anapogundua kwamba nusu ya maisha yako yanachunguza maisha yake so atakuwa anafnya kila jambo ambalo anaona litakuwa negative au litakufanya ucoment kwa kila jambo analolifanya
 
20151227173642_zpsurf3rdlg.png
 
Mbona rangi ya uso na mikono ya bibi arusi havina mshabihiano! kauso ka bibi arusi keupe mikono rangi halisi! hata hivo hongera zao!
 
Huhuhu mushumbusi kweli wewe unajua kuchezakarata zako kula maisha mmama.mi huwa nashangaaa sana wanawake uchumi uchumi mmpewa n.a. mifano mlipewa hapo mwenzomwanaume hajiweziikwa mwanamke kumbukeni adamu na hawa sembuse mushumbusi n.a. slaaa msiwe kama wema sepetunga kuchezea uchumi wake umeona wakina Jack mengi wanawake tumieni vizuri uchumi wenu mjitambue hakuna mwanamke ambaye atataka njaaa hahaha
 
Inapofikia hatua ya wananchi kushindwa kutenganisha ushabiki wa soccer na Ushabiki wa Siasa basi ujue "brainwashing is on point! " Hivi mtu mzima na akili zako unashindwaje kutofautisha maisha binafsi na Siasa?!

Besides Doctor Slaa kalifanyia mengi Taifa, mbali na makosa yake na madhaifu yake bado anastaili heshima kama binaadam yeyote yule bila kujali itikadi za Kisiasa, kiimani na wala kikabila!

**Siku watanzania tukijifunza kuheshimiana na kuheshimu mipaka baina ya utu wetu, undani wetu na utendaji wetu ndio siku tutakayopiga hatua mbele kutoka hapa tulipo ila kwa sasa "Sifa za pekee ziwaendee wale wanasiasa (sio wote) waliofanikisha Zoezi la DIVIDE & RULE (aka ABUSE)!!" mmefanikiwa sana kuhakikisha nchi haiongozwi unless FITNA & UZANDIKI vishike hatamu!

**Hongera sana wanandoa!
 
Huyo ni chaguo lake .... awe mfupi .... awe mnene .... awe mwembamba .... awe mweupe .... ni chaguo lako. Hongera zao maharusi. Nawatakia Hane muni njema!
 
Hilo kanisa sio la Chung moon Jung kweli? The unification church ambalo ASKOFU Millingo nae alifunga ndoa na mkorea mwaka uleeee? Maana naona wapambe ni wakorea/wachina!
Chief unawajua hawa The Unification Church?mwaka 2013 walileta tawi lao pale Sinza nyuma ya Mabatini Police Station acha bwana nilipiga pesa chafu msimu huo maana mpunga ulikua nje nje kuna watoto wa Kihaya walishtuka mapema wakaniita kwenye ujasiria dini baadae nikapepea zangu.
Mama Dr itakua kanywa maji mengiiiiii sanaaaa maana usoni sio haba aseee ana ng'aaaaa haswa.
 
IMG_20160303_061829_281.JPG

Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.

Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.

Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo.
Wanasheria mtujuze je ndoa ya wawili hawa itakuwa halali wakirudi Tanzania?
 
Natamani kuoa bukoba haiwezekani yaekekea kuna mambo, mazito huko!si bure mpaka mwanakondoo avurugikiwe!/
 
babu piga mazoezi uondoe kitambi hicho, vinginevyo utasaidika na vijana wazungusha mikono hewani
 
Back
Top Bottom