Dr. Slaa afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

Jamjicho

Member
Jan 25, 2016
15
11

Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.

Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo.

Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.
 
......alieuacha upadri.....akavunja nadhiri ya upadri wake aliowekewa mikono na mapadri......akashindwa kuuvumilia upadri.....akafanya unyanganyi ....hatimaye ....akaoa......mungu amsimamie.....!?
 
Giant men wengi ni victim wa kuangushwa na wanawake.angalia
Samson na Delila
Daudi na Berthsheba
Solomon na wanawake wake (Queen of Sheba nk)
Adam na Eva
Clinton na Monica Lewisky ....
udhaifu mkubwa wa mwanaume upo kwenye sehemu zake za siri I guess...
 
IMG_20160303_061829_281.JPG

Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.

Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.

Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo.
 
Hongera Dr Slaa..kila la heri! Kina mdee huku wanaendelea kunyanyaswa na serikali kama walivyo kufanyia wewe. But Mbowe a nawasubiri kama kawa kina Mwigulu waje kugombea dk za Mwisho kwa tiketi ya CDM!
 
......alieuacha upadri.....akavunja nadhiri ya upadri wake aliowekewa mikono na mapadri......akashindwa kuuvumilia upadri.....akafanya unyanganyi ....hatimaye ....akaoa......mungu amsimamie.....!?

Nikisoma comments za watu wanaoongea negative kuhusu mtu kufunga ndoa inanishangaza sana

Kisaikolojia naona dalili za wivu tu hakuna kingine

Kuna kijigazeti fulani kinamilikiwa na makanjanja fulani toleo lifuatalo utaona kitaweka suala la ndoa na hii picha front page na au ukurasa wa katikati.Kisha kitajiita "Gazeti la Uchunguzi"

That's just how losers and mediocres console themselves

You should face your own life if you have one

Wengine watakuja hapa kulalamika mbona hajafungia nchini kama wale waliolialia kwenye thread ya jana usiku

Hii tabia ya kuzamia kwenye sherehe za watu ipo Tanzania tu.Dunia haiko hivyo

Tubadilike tuache majungu,Wivu na Chuki.

It will cost you nothing kutoa maneno ya Baraka kwa mwenzako aliyetenda jambo la kheri

Who the hell are you to judge others?

Tena wengine kama huyu anamtaja "mungu" wake kwa kumuandika kwa kuanza kwa Herufi ndogo,unafiki tu wa kutaka kuonyesha kuwa sisi tunamjua Mungu zaidi kuliko wengine.

Get a life !
 
Back
Top Bottom