Dr. Slaa aanza ziara ndefu barani Ulaya

Dr. Slaa aanza ziara ndefu barani Ulaya

Duh hii hatari, Yaani huko Babu anatembea na picha za marehemu (Umeziona lakini - au inteljensia!!!) Huku Jamaa Mwigulu Nchemba naye anatembea na yule kijana aliyemwagiwa tindikali Igunda majukwaa yote kuzunguka nchi nzima kwa kuinadi CCM.
HIVI VYAMA VIMEANZA KUTUMIA MAJONZI YA WATANZANIA KAMA MTAJI WA KISIASA??
NINI TOFAUTI YA CDM (21yrs old) WANAOTEMBEA NA PICHA HUKU CCM (35yrs old) IKITEMBEA NA WAJERUHIWA??

hahahahahaha yule njamaa wa tindikal amegeuzwa mtaji wa ccm!
 
Wameishia kunibambikizia zigo la kupeleka computers ahadi ambayo ilitolewa na CHADEMA UK.

Ningejua alikofikia babu germany ningempelekea hizi computers arudi nazo azipeleke badala ya kubeba picha kwenye mabegi ni bora angebeba computers

Ustaarabu ni jambo la maana sana.I really doubt kama umeenda shule!Nahisi hata maisha ya kawaida tu huko UK utakua mtu wa ajabu sana.Hauna courtesy,unayoandika humu yanatoa taswira halisi.Grow up bro!
 
hahahahahaha yule njamaa wa tindikal amegeuzwa mtaji wa ccm!

Namuonea huruma kwa kudhalilishwa majukwaani. Haki za binadamu siku hizi ndio zinaruhusu hayo, tufanye nini kesi ya the hegue nayo ishatupwa mchangani.
 
Namuonea huruma kwa kudhalilishwa majukwaani. Haki za binadamu siku hizi ndio zinaruhusu hayo, tufanye nini kesi ya the hegue nayo ishatupwa mchangani.

Heche na picha za Mauaji ya mwangosi na zile Moro anafanya nini nazo huko ulaya?
 
Heche na picha za Mauaji ya mwangosi na zile Moro anafanya nini nazo huko ulaya?

Ni ulimbukeni, kutembea na mwananchi hai ukinadi sera za chama, tena chama kikongwe kama hicho. Tena hisia tu kuwa alimwagikwa tindikali na upinzani!!!. Hakuna kithibitisho chochote cha tukio hilo hivyo ni kosa kweli tena chama kinajiuwa kinaponadi sera hizo mbele ya watanzania ambao ni wafuatiliaji wa mambo / Propaganda zinavyoendeshwa.

Hilo la heche ni hisia kuwa anatembea na Picha, Hata kama itakuwa kweli ni nani aliyeangalia tukio la mwangosi leo unaweza ukamwambia kuwa huyo aliuwawa na washabiki wa Chadema?. Je waliomuuwa mbele ya huyo kamanda na kushitakiwa ni wafuasi wa Chadema?
Under this technology wanaendelea kudanganyika wale wasioona na wasikuwa na kumbukumbu ya matukio na jinsi yanavyofanyiwa kazi nchini.

Ukitaka kujijua vizuri tabia yako na jinsi ulivyo, sikiliza watu wanaongeaje kuhusu wewe na sio unajinadije kwa watu.
kama CCM bado inaamini watanzania wamelala waendelee na propaganda hizo.
 
Ustaarabu ni jambo la maana sana.I really doubt kama umeenda shule!Nahisi hata maisha ya kawaida tu huko UK utakua mtu wa ajabu sana.Hauna courtesy,unayoandika humu yanatoa taswira halisi.Grow up bro!
Aisee mbeba sumu una bonge la akili
 
ujerumani kuna wakakisi wa kutisha na vizazi vya adolf hitler. waswahili usema ukitaka kunijua mimi mtazame rafiki yangu.
 
Natamani hizi baadhi za ziara za mtalii wetu jk angepewa dr slaa nina uhakika kuna mengi tungejifunza kuhusu namna gani wenzetu walio mbele yetu kimaendeleo wamefanikiwa kwa ziara hii moja tu ya dr slaa kule german nimeanza kujifunza mambo mengi ya kusisimua ukilinganisha zile ziara 300 za fastjet ambazo hakuna hata moja alichorudi nacho.nasikia nape naye alikwenda german mbona hawatuambii walichoambulia huko?au walihisi kama wanaangalia movie za kichina na wakatoka watupu baada ya workshops kumalizika?naye mwigulu alikuwa na kazi kujisifia sijui alikuwa nchi gani nini alichoambulia huko hatuambii zaidi ya majigambo.hizi elimu za kununua zina matatizo sana.teh teh teh teh!
 
Chadema mbona mnafanya siri kuweka wazi safari ya Dr Slaa nchini Ujerumani.

Ukweli ni huu Dr Slaa amekwenda Ujerumani kuonana na chama rafiki wa Chadema, Christian Democratic Union (CDU)

So what? Unafikiri ni mjinga kama Prof Lipumba na Kikwete walioamua kuunganisha kura?? Na kuwatumia baadhi ya "waislam" kama "toilet paper" ? Siku zote chadema ipo open na ndio maana wanatangaza hata misaada inayopata hadharani mchana kweupe. Sio kuficha ficha kama hao waliberali na maccm
 
Aisee, hawa jamaa wanaweza chukua nchi hivi hivi.
 
Certificate>certificate>Diploma>Phd! Elimu ya Dr Slaa!

Kwa what is Phd?. Maana naona unashangaa.
Labda nikisaidie,
Simply, Ph. D holder is a professional researcher. Kwa hiyo u can star a PhD training at any point.
Labda swali la msingi ni je, chuo alichosoma kinatambulika kiithabati?.
Vinginevyo hakuna tatizo hapo.
 
Eddie,
Walafi daima hufikiria nafsi zao na posho. Wana mageuzi hufikiria namba ya kukomboa mataifa Yao.
Nikuhakikishie, hakuna posho coyote iliyotolewa na hakuna sent hata mmoja ya chadema imetumika katika ziara hii. Dr. Slaa amesafiri na ndege kwa kutumia Economy Class kwa kutambua kuwa ukombozi sio sherehe bali kupitia milim a na mabonde kwa ajili ya watanzania wengi walioweka matumaini yaeo kwa Chadema.

Tarehe 5June, nimekuwa na mikutano mbalimbaeli Karlsruhe na viongozi wa ngazi mbalimbali. Nimejifunza mengi hasa kuhusiana na mfumo wa Utawala wa Local Government, Karlsruhe ipo katika State of Baden Wurtenburg.

Kuanzia Tarehe 6 June nimehudhuria Breakfast Prayer iliyoshirikisha viongozi Wabunge, Maspika, Mabalozi na viongozi wa Vyama kutoka nchi 100 kutoka Dunia nzima, na wajumbe zaidi ya 1,000. Huu ni Mkutano wa 18 tangu Breakfast Prayer Gatherings imeanza. Mkutano umeandaliwa na wabunge wa Bundestag (Bunge la Ujerumani). Kati ya waliohudhuria ni Wabunge wa Iran, Sudan na Southern Sudan. Ilifurahisha sana kuona Spika wa Sudan na Southern Sudan kukaa meza mmoja baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusiana na mgogoro baina ya nchi zao mbili. Huu ni mkutano unaounganisha madhehebu yote ya Dini, bila kubagua mataifa, rangi, na au dini zao. Dini zote zinaamini kuna Mwenyezi Mungu, na kumekuwa na themes mbaelimbali katika mkutano huu wa siku tatu.

Kuanzia kesho Nina mikutano kadhaa katika Lander ( States mbalimbali) kwa mikutano na MinisterPresident ( Mawaziri wakuu wa States hizo pamoja na maofisa mbalimbali. Kila nitakapopata nafasi nitakuwa nikiwajulisha matukio mbalimbali. Wenye nia njema wanaweza kuniuliza wanavyopenda kuliko kufanya posts za upotoshaji. Nawatakia nyote neema na baraka tele. Yako mengi yanayotuunganisha watanzania katika swala la dini zetu mbalimbali kuliko yanayotutenganisha. Nimejifunza mengi kwa Iran, ambayo ni takriban 99% Islamic lakini Bunge Lao Lina wabunge Waislamu, wayahudi na Wakristu.

Ukiwa huko pia waulize hao Wajerumani waliwezaje kupiga hatua kubwa hivyo ya Maendeleo kwa kutumia Lugha yao? Wakati nyinyi CHADEMA (nimesikia) mnataka kukifuta Kiswahili shuleni au kukiweka Daraja la pili baada ya Kiingereza, sasa huko waulize hao jamaa, waliwezaje kutengeza Mercedes Benz, BMW, Siemens na Wanasayansi na Wahandisi wa kufa Mtu kwa kutumia Lugha yao na SIO kiingereza!

Mimi nikipata tu hilo jibu ndio nitawakubali CHADEMA, kwa maana nyingine CHADEMA wanihakikishie kwamba Kiswahili kitakuwa Namba moja na kubaki namba moja na hizo Lugha nyingine ziwe Daraja la Pili, kinyume na hapo nitawapinga kwa nguvu zangu zote vyovyote vile niwezavyo, na popote pale nilipo!
 
Dr. Unajenga matumaini, hamasa, faraja na ushirika wa dhati katika ukombozi wa Nchi yetu na watu wake, tunapenda viongozi wawazi na wakweli kama wewe watawale taifa lenye utajiri usiojulikana umuhimu wake toka miaka hamsini iliyopita. Ni dhahiri kuwa utatupatia majibu ya kisayansi kuhusu ujio wa rais wa china na huyu Obama unamanufaa gani kwa taifa hili na hasara gani.ili tujue wazi kama bado tuna uhai au unaendelea kupotezwa.
 
Hivi CDM hakuna wasomi wa kwenda kwenye hizo ziara? Mzee Slaa anawika bongo tu huko kwa wazungu anaenda kutuchafulia jina la Tanzania na vidocument vyake visivyo na maana.
 
Dr. Unajenga matumaini, hamasa, faraja na ushirika wa dhati katika ukombozi wa Nchi yetu na watu wake, tunapenda viongozi wawazi na wakweli kama wewe watawale taifa lenye utajiri usiojulikana umuhimu wake toka miaka hamsini iliyopita. Ni dhahiri kuwa utatupatia majibu ya kisayansi kuhusu ujio wa rais wa china na huyu Obama unamanufaa gani kwa taifa hili na hasara gani.ili tujue wazi kama bado tuna uhai au unaendelea kupotezwa.

Naamini Dr Slaa anakusoma na atatupatia majibu mujarab.
 
Ukiwa huko pia waulize hao Wajerumani waliwezaje kupiga hatua kubwa hivyo ya Maendeleo kwa kutumia Lugha yao? Wakati nyinyi CHADEMA (nimesikia) mnataka kukifuta Kiswahili shuleni au kukiweka Daraja la pili baada ya Kiingereza, sasa huko waulize hao jamaa, waliwezaje kutengeza Mercedes Benz, BMW, Siemens na Wanasayansi na Wahandisi wa kufa Mtu kwa kutumia Lugha yao na SIO kiingereza!

Mimi nikipata tu hilo jibu ndio nitawakubali CHADEMA, kwa maana nyingine CHADEMA wanihakikishie kwamba Kiswahili kitakuwa Namba moja na kubaki namba moja na hizo Lugha nyingine ziwe Daraja la Pili, kinyume na hapo nitawapinga kwa nguvu zangu zote vyovyote vile niwezavyo, na popote pale nilipo!

Habari za kusikia changanya na za kwako ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom