Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, Juni 5, mwaka huu, ameanza ziara ya takriban wiki 3 barani Ulaya katika nchi ya Ujerumani.
Kwa mujibu wa habari kwenye Ukurasa wa Facebook ya CHADEMA na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Dkt. Slaa ambaye aliondoka nchini Juni 4, mwaka huu ktk ziara hiyo ya kikazi, atakutana na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.
Namnukuu-''Ni kweli mkubwa, Katibu Mkuu yuko nje ya nchi tangu juzi kwa ziara ya kikazi nchini Ujerumani, itakayochukua wiki tatu...atakuwa na ratiba tight kidogo, akiwa huko kama unavyojua Dkt. Slaa yuko kazini karibu muda wote, kwa sababu kwa sasa hakuna muda wa kupoteza hata sekunde, si unajua M4C iko matendoni mkubwa, ndani na nje ya nchi, ameenda kikazi,'' amesema Makene.
Itakumbukwa mwezi uliopita Dr Slaa alifanya ziara nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alifanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Michael Satta katika Ikulu ya Lusaka.