Dr. Slaa aanza ziara ndefu barani Ulaya

Dr. Slaa aanza ziara ndefu barani Ulaya

CHADEMA hemu jifunzeni utu, tamaa ya madaraka nyie, tamaa ya pesa nyie, tamaa ya wake za watu nyie. Sasa kwa hali hii mtakuwa na utu kweli?
 
Mkuu hiyo ni lazima na wanaitumia kama kitambuisho cha chadema.

Mkuu hivi familia ya Mwangosi inapata chochote kwenye hiyo CD, naona viongozi wa Chadema wanapishana kutembeza hiyo CD, mwezi uliopita John Heche alitumwa kuitembeza Ulaya.
 
Kila lililo jema huko ughaibuni, tunaamini yote ni kwa mapenzi mema ya taifa letu na wapenda mabadiliko kiujumla!
 
MUNGU akulinde na AKUONGEZEE hekima zaidi Ili Hadi hao WAZUNGU wajivue MAGAMBA na Waione CCM kama Kundi la WALANGUZI.
 
Mkuu hivi familia ya Mwangosi inapata chochote kwenye hiyo CD, naona viongozi wa Chadema wanapishana kutembeza hiyo CD, mwezi uliopita John Heche alitumwa kuitembeza Ulaya.
Wameishia kunibambikizia zigo la kupeleka computers ahadi ambayo ilitolewa na CHADEMA UK.

Ningejua alikofikia babu germany ningempelekea hizi computers arudi nazo azipeleke badala ya kubeba picha kwenye mabegi ni bora angebeba computers
 
Katika ilani ya CHADEMA ya 2010 - 2015 kulikuwa na kipengele hiki:

''Tanzania imegeuka taifa omba omba na hotubu nyingi za Rais zimekuwa ni za kusifia na kupongeza misaada na wahisani, badala ya nini tufanye kama taifa''

Nilitegemea CHADEMA angalau wangeweza kuonesha mfano kwa kutokuwa tegemezi katika hatua za awali kabla haijaingia ikulu.

Lakini kama wameshindwa kujitegemea katika kuendesha chama, ni kweli wataweza kufanya hivyo watakapokuwa na serikali?!
 
mzee slaa ameona kubeba hizo picha ni mtaji wake kisiasa.
 
Vipi ameongozana na mchumba wake au? Akirudi abanwe aweke hadharani matumizi ya fedha za M4Change.
 
Wameishia kunibambikizia zigo la kupeleka computers ahadi ambayo ilitolewa na CHADEMA UK.

Ningejua alikofikia babu germany ningempelekea hizi computers arudi nazo azipeleke badala ya kubeba picha kwenye mabegi ni bora angebeba computers
Cris inabidi uwe makini jamaa unavyowabomoa siku wakikuoona watakutia sumu.
 
Eddie,
Walafi daima hufikiria nafsi zao na posho. Wana mageuzi hufikiria namba ya kukomboa mataifa Yao.
Nikuhakikishie, hakuna posho coyote iliyotolewa na hakuna sent hata mmoja ya chadema imetumika katika ziara hii. Dr. Slaa amesafiri na ndege kwa kutumia Economy Class kwa kutambua kuwa ukombozi sio sherehe bali kupitia milim a na mabonde kwa ajili ya watanzania wengi walioweka matumaini yaeo kwa Chadema.

Tarehe 5June, nimekuwa na mikutano mbalimbaeli Karlsruhe na viongozi wa ngazi mbalimbali. Nimejifunza mengi hasa kuhusiana na mfumo wa Utawala wa Local Government, Karlsruhe ipo katika State of Baden Wurtenburg.

Kuanzia Tarehe 6 June nimehudhuria Breakfast Prayer iliyoshirikisha viongozi Wabunge, Maspika, Mabalozi na viongozi wa Vyama kutoka nchi 100 kutoka Dunia nzima, na wajumbe zaidi ya 1,000. Huu ni Mkutano wa 18 tangu Breakfast Prayer Gatherings imeanza. Mkutano umeandaliwa na wabunge wa Bundestag (Bunge la Ujerumani). Kati ya waliohudhuria ni Wabunge wa Iran, Sudan na Southern Sudan. Ilifurahisha sana kuona Spika wa Sudan na Southern Sudan kukaa meza mmoja baada ya mazungumzo ya pamoja kuhusiana na mgogoro baina ya nchi zao mbili. Huu ni mkutano unaounganisha madhehebu yote ya Dini, bila kubagua mataifa, rangi, na au dini zao. Dini zote zinaamini kuna Mwenyezi Mungu, na kumekuwa na themes mbaelimbali katika mkutano huu wa siku tatu.

Kuanzia kesho Nina mikutano kadhaa katika Lander ( States mbalimbali) kwa mikutano na MinisterPresident ( Mawaziri wakuu wa States hizo pamoja na maofisa mbalimbali. Kila nitakapopata nafasi nitakuwa nikiwajulisha matukio mbalimbali. Wenye nia njema wanaweza kuniuliza wanavyopenda kuliko kufanya posts za upotoshaji. Nawatakia nyote neema na baraka tele. Yako mengi yanayotuunganisha watanzania katika swala la dini zetu mbalimbali kuliko yanayotutenganisha. Nimejifunza mengi kwa Iran, ambayo ni takriban 99% Islamic lakini Bunge Lao Lina wabunge Waislamu, wayahudi na Wakristu.

Jahazi inazama huku uchaguzi wa kata 25, katibu kaitosa meli anakimbizia posho.....
 
CHADEMA omba omba, dah, hawa jamaa ni waajabu sana!

Serikali ikiomba msaada dhambi, ila kwa wao ni sawa tu. Hapa wataendelea kuwadanganya VILAZA tu wenye akili hatudanganyiki.

Tena mbaya zaidi CHADEMA haisemi kiasi cha mapato wayapatayo kwenye kuomba omba kwao huko. Na wanachama hawapaswi kuhoji matumizi, hapo hapo wanajiita chama cha demokrasia.

CHADEMA ni chama cha wapiga dili, hili halina ubishi.
 
Back
Top Bottom