Dr Rioba, uelewa wako una walakini

Dr Rioba, uelewa wako una walakini

Dr Rioba alichosema sio sahihi.Reli ya kati ilijengwa na Wajerumani kati 1914-1918.Mwaka wa 1800 Africa ilikuwa haijagawanywa na wakoloni wakina Carr Peters 1884 mkutano wa Berline Conference
 
Nimesikia katika kipindi TBC DK 15 zilizopita, Dr Rioba akisema Central Railway ilijengwa katika miaka ya 1800 hadi miaka ya 1920 na kitu , na wajerumani ????

Mimi ni muhandisi na historia yangu ya msingi najua ujenzi wa Cetral Railway ilianza 1905 hadi 1914, na utawala wa wajerumani ulikoma 1918 baada ya vita kuu ya kwanza.

Dr unanitia wasi wasi elimu yako!
Hivi kuwa na kumbukumnbu sahihi ya kitu fulani marginal, au miaka Reli ilianza kujengwa na kumalizika, ni usomi au ni swala la kumbukumbu tu? Kwa mfano, mimi hapa nilipo, sikumbuki hata tarehe na mwaka wa kuzaliwa kwangu, japo wazazi wangu waliwahi kunitajia. Pia nikiwa shule ya msingi, niliwahi kufundishwa miji mikuu yote ya Nchi za Afrika lakini sasa hivi nakumbuka Dodoma tu. Je, hii kitu itaniletea shida kazini kama mwajiriwa, si ndiyo?
By the way, huyu Rioba mbona huwa anakaa anaandamwa andamwa sana? Ana nini cha zaidi? Mti wenye matunda.....
 
Hapakua na ulazima wa kutuambia kwamba wewe ni muhandisi.
Tatizo la humu jf, kila mtu ni msomi na ana degree kama Mwajuma nichokonoe
Mzee humu jukwaani wala hatuhitaji degree za watu, tunahitaji hoja tu basi. Hapa nilipo mimi sina hata digrii moja, nina ki-diploma changu tu cha Uhasibu kutoka pale TIA. Lakini ndugu yangu naomba nikuhakikishie kwa uhakika kabisa, mtu yeyeote akiingia kichwa kichwa kwangu kwa kuleta hoja ambayo haina miguu wala kichwa, I will blast them hata kama ana digrii 500, nina uhakika huo. Issue hapa ni hoja, siyo digrii! Uko sahihi mkuu
 
Nimesikia katika kipindi TBC DK 15 zilizopita, Dr Rioba akisema Central Railway ilijengwa katika miaka ya 1800 hadi miaka ya 1920 na kitu , na wajerumani ????

Mimi ni muhandisi na historia yangu ya msingi najua ujenzi wa Cetral Railway ilianza 1905 hadi 1914, na utawala wa wajerumani ulikoma 1918 baada ya vita kuu ya kwanza.

Dr unanitia wasi wasi elimu yako!
Ukosahihi lakini nadhani ni ile hali ya kuamini aliteuliwa kwa sababu anajua sana! Anajikuta analazimisha ajue hata mambo ambayo hana ufahamu nayo. Ila ni ustaarabu mdogo. Hata mwalimu anatakiwa akili yote asiyoyajua.
 
Hivi kuwa na kumbukumnbu sahihi ya kitu fulani marginal, au miaka Reli ilianza kujengwa na kumalizika, ni usomi au ni swala la kumbukumbu tu? Kwa mfano, mimi hapa nilipo, sikumbuki hata tarehe na mwaka wa kuzaliwa kwangu, japo wazazi wangu waliwahi kunitajia. Pia nikiwa shule ya msingi, niliwahi kufundishwa miji mikuu yote ya Nchi za Afrika lakini sasa hivi nakumbuka Dodoma tu. Je, hii kitu itaniletea shida kazini kama mwajiriwa, si ndiyo?
By the way, huyu Rioba mbona huwa anakaa anaandamwa andamwa sana? Ana nini cha zaidi? Mti wenye matunda.....
Kumbukumbu ndo ufahamu au usomi na pamoja na utashi ndo maana ya binadamu. Hali uliyonayo nahisi ni mwanzo wa Alzheimer. Ugonjwa unaokuondolea kumbukumbu. Kifuatacho utasahau kujisafisha chooni na itakuwa aibu kwa familia. Chukuwa hatua.
 
Kumbukumbu ya vitu ambavyo ni marginals? Umesoma vizuri nilichoandika? Hapo wewe ulipo kwa mfano, una ulazima gani wa kufahamu mji mkuu wa Norway unaitwaje? Wa Tanzania sawa, ila huo mwingine is something marginal. Wagonjwa tuko wengi
 
Wote hata babu zenu walikuwa hawajazaliwa,mnasoma vitabu vya history kama hadithi,inategemea pengine wewe umesoma kitabu tofauti na alichosoma Dr Rioba,watunzi tofauti,si kwamba elimu yake inamashaka

Kwa hiyo unaamini kuna kitabu cha historia kinachodai Wajerumani walikuwa wanatawala Tanganyika miaka ya 1920 na kikawa sahihi?
Hii nchi ina matatizo makubwa kuliko tunavyodhani!
 
Now sasa ndio nimeelewa kumbe tunazungumza vitu viwili tofauti, Dr. Ayub yuko very right kwenye general picture ya reli nchini Tanzania ilianza kujengwa lini, its on 1800s, wewe uko very specific kwa Reli ya Kati only, kitu ambacho usichojua na naomba nichukue fursa hii kukujulisha wewe na wengine wasiojua ambao walidhani wanajua, reli inayoitwa Reli ya Kati, ni jina tuu, reli ya Tanzania ilianza kujengwa 1800s, na ilianzia Tanga, reli ya kati, ilipounganishwa, jina la reli likabaki kuitwa reli ya kati as just a name, lakini ukisema reli ya Tanzania, unamaanisha ni reli ya kati.
p
Reli ya kwanza ilikuwa Unguja, kabla ya bara. Soma zaidi:
Reli ikipitia maeneo ya makazi ya watu. Picha

Reli ikipitia maeneo ya makazi ya watu. Picha na Charles Kayoka. Picha ya Kituo cha treni Bububu

Kwa ufupi
  • Awali reli hiyo ilikuwa inavutwa kwa punda, lakini mwaka 1881 Sultani aliinunulia kichwa cha gari moshi (steam engine). Reli hii ilifungwa mwaka 1888 baada ya kufa kwa Sultan aliyeianzisha. Baadaye reli ya usafiri wa kawaida ilifunguliwa mwaka 1905 na kufungwa tena 1930.
Chanzo: Historia ya reli ilianzia Unguja
 
Dr Rioba alichosema sio sahihi.Reli ya kati ilijengwa na Wajerumani kati 1914-1918.Mwaka wa 1800 Africa ilikuwa haijagawanywa na wakoloni wakina Carr Peters 1884 mkutano wa Berline Conference
Kuna tofauti kati ya 1800 na 1800s, 1800 ni mwaka wa 1800 na 1800s ni karne ya 18. Tanganyika reli ilianza kujengwa karne ya 18, Dr. Rioba yuko right.
Halafu huwezi kum discredit mtu wa Ph.D kwa kitu kidogo kama hicho ambacho sio cha uelewa ni cha kumbukumbu tuu, it's not about understanding but remembering.
P
 
Wote hata babu zenu walikuwa hawajazaliwa,mnasoma vitabu vya history kama hadithi,inategemea pengine wewe umesoma kitabu tofauti na alichosoma Dr Rioba,watunzi tofauti,si kwamba elimu yake inamashaka
Wewe unamtetea Dr Rioba wa TBC ? kabla ya kuanza kushabikia kwanza sibitisha Kati ya taarifa ihizo mbili NI ipi sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia katika kipindi TBC DK 15 zilizopita, Dr Rioba akisema Central Railway ilijengwa katika miaka ya 1800 hadi miaka ya 1920 na kitu , na wajerumani ????

Mimi ni muhandisi na historia yangu ya msingi najua ujenzi wa Cetral Railway ilianza 1905 hadi 1914, na utawala wa wajerumani ulikoma 1918 baada ya vita kuu ya kwanza.

Dr unanitia wasi wasi elimu yako!
Hapa ni kwa kuongezea tuu, wewe na Dr. Rioba mnazungumzia vitu viwili tofauti. Dr. Riiba amezungumzua reli ya Tanganyika in general ilianza kujengwa karne ya 18 hivyo he is right kuita 1800s, wewe unazungumzia specific reli ya Kati. Japo reli kuu Tanzania ni reli ya Kati, lakini ujenzi wa reli haukuanza na reli ya Kati ulianza na reli ya Tanga karne ya 18, ndipo ikakaja kuunganishwa na reli ya kati karne ya 19 na reli yote kuitwa reli ya Kati.

Pili ni hili ndilo muhimu zaidi, huwezi kum discredit msomi wa Ph.D kwa kutilia shaka usomi wake kwa jambo dogo kama hili la kumbukumbu tuu, ambalo has nothing to do with understanding, but only memory!.

Kama unaweza kum discredit Ph.D huyu kwa kitu ambacho yuko very right, ungesema nini kwa Ph.D wetu wa kemia aliyesema Saadam Hussein ni rais wa Kuwait,, alipoingia alikuta kilo ya sukari ni TZS 5,000!

Vitu vingine ni vikosa vidogo vidogo total immaterial not worth even to be mentioned!.
P
 
Reli ya kwanza ilikuwa Unguja, kabla ya bara. Soma zaidi:
Reli ikipitia maeneo ya makazi ya watu. Picha

Reli ikipitia maeneo ya makazi ya watu. Picha na Charles Kayoka. Picha ya Kituo cha treni Bububu

Kwa ufupi
  • Awali reli hiyo ilikuwa inavutwa kwa punda, lakini mwaka 1881 Sultani aliinunulia kichwa cha gari moshi (steam engine). Reli hii ilifungwa mwaka 1888 baada ya kufa kwa Sultan aliyeianzisha. Baadaye reli ya usafiri wa kawaida ilifunguliwa mwaka 1905 na kufungwa tena 1930.
Chanzo: Historia ya reli ilianzia Unguja
Kwenye hili dada yangu FF uko very right, kwa vile Tanzania ni nchi moja ya Jamhuri ya muungano, ambayo inajumuisha Zanzibar, tunapozungumzia historia ya reli ilianza lini, tunapaswa kuanza na reli ya Zanzibar, kama tunavyozungumzia Tanzania ilipata uhuru wake 1961 ni Tanzania yote na kwa upande wa historia ya Television, Tanzania ndio nchi ya kwanza barani Africa Kusini mwa jangwa la Sahara kuwa na TV ya Rangi, tuliipata mwaka 1971 huko Zanzibar, japo kwa Tanzania bara TV ilianza mwaka 1994.

P
 
Hapa ni kwa kuongezea tuu, wewe na Dr. Rioba mnazungumzia vitu viwili tofauti. Dr. Riiba amezungumzua reli ya Tanganyika in general ilianza kujengwa karne ya 18 hivyo he is right kuita 1800s, wewe unazungumzia specific reli ya Kati. Japo reli kuu Tanzania ni reli ya Kati, lakini ujenzi wa reli haukuanza na reli ya Kati ulianza na reli ya Tanga karne ya 18, ndipo ikakaja kuunganishwa na reli ya kati karne ya 19 na reli yote kuitwa reli ya Kati.

Pili ni hili ndilo muhimu zaidi, huwezi kum discredit msomi wa Ph.D kwa kutilia shaka usomi wake kwa jambo dogo kama hili la kumbukumbu tuu, ambalo has nothing to do with understanding, but only memory!.

Kama unaweza kum discredit Ph.D huyu kwa kitu ambacho yuko very right, ungesema nini kwa Ph.D wetu wa kemia aliyesema Saadam Hussein ni rais wa Kuwait,, alipoingia alikuta kilo ya sukari ni TZS 5,000!

Vitu vingine ni vikosa vidogo vidogo total immaterial not worth even to be mentioned!.
P
Ulichoongeza mkuu ni kwa uelewa wako tu.
Hujaisaidia mda wala kumsaidi Dr Rioba kisawa sawa.
Dr Rioba alibugi kwa kutoweza eleza kiufasaha ujenzi wa reli ya kati, na si reli za Moshi wala reli ya karanga, Mtwara.
 
Hivi kuwa na kumbukumnbu sahihi ya kitu fulani marginal, au miaka Reli ilianza kujengwa na kumalizika, ni usomi au ni swala la kumbukumbu tu? Kwa mfano, mimi hapa nilipo, sikumbuki hata tarehe na mwaka wa kuzaliwa kwangu, japo wazazi wangu waliwahi kunitajia. Pia nikiwa shule ya msingi, niliwahi kufundishwa miji mikuu yote ya Nchi za Afrika lakini sasa hivi nakumbuka Dodoma tu. Je, hii kitu itaniletea shida kazini kama mwajiriwa, si ndiyo?
By the way, huyu Rioba mbona huwa anakaa anaandamwa andamwa sana? Ana nini cha zaidi? Mti wenye matunda.....
Kumbukumbu ni muhimu sana katika usomi.
Kama daktari ange prescribe dawa ambazo hata hajui au hana kumbukumbu zake ingekuwaje mkuu.
Kama kumbukumbu ni kaput, just frankly how do you function?
Jijibu mwenyewe!!
Rioba hapigwi madongo kwa sababu ni msomi bali kwa sababau haonyeshi kiufasaha huo usomi.
 
Uko sahihi kabisa ndugu yangu wla sipingani na wewe, ila swali langu linaanza hivi: Hivi kuwa na kumbukumnbu sahihi ya kitu fulani marginal,.............................................
 
Nimesikia katika kipindi TBC DK 15 zilizopita, Dr Rioba akisema Central Railway ilijengwa katika miaka ya 1800 hadi miaka ya 1920 na kitu , na wajerumani ????

Mimi ni muhandisi na historia yangu ya msingi najua ujenzi wa Cetral Railway ilianza 1905 hadi 1914, na utawala wa wajerumani ulikoma 1918 baada ya vita kuu ya kwanza.

Dr unanitia wasi wasi elimu yako!

Historia ya kundikwa na binadamu wenye akili za kibinadamu mara nyingi huwa ni potofu siku zote....

Mfano ni huu tunaoambiwa binadamu hatukuumbwa ukiwa hivi ulivyo leo kisura na nafsi yenye utashi...

Bali tulikuwa Manyani ama Masokwe ama Chimpanzees na taratibu tuka "evolve" na kuwa hivi tulivyo leo.....

Uongo, uongo mtupu!!

Maana kama ñi kweli, ni kwanini basi Nyani wa leo, Sokwe wa leo na Chimpanzees wa leo hawabadiliki na kuwa binadamu wenye akili na utashi wa nafsi kama tulivyo mimi na wewe leo??
 
Mkuu evolution is a matter of contention going back millions of years away, na ni subjective.
Tuache hiyo hivi ilivyo.
Lakini historia ya miaka hata 2000 iliyopita bado bado waweza kuifuatilia na kuijua kinaga ubaga.
 
Back
Top Bottom