Huyu Mzee ni kama Nabii Fulani, he has "powers from within", ukimtibua... safari!.
- Alianza na wamiliki wa DTV na CTN kuhusu haki za kuonyesha kombe la dunia, vituo vyote viwili vimekufa!.
- Akatishiwa kifo, kawataja wamiliki wa DTV, Shabbir na Murtaza Dewji wakatiwa ndani!.
- Alitibuana na Katibu Mkuu, Mambo ya Ndani, Silvanus Adel, kwa kuamrisha wahindi hao waachiwe, Adel alimwaga unga wake!.
- Akatibuana na Gazeti la Mtanzania kutoa siri kuwa anadaiwa na mabenki, Mtanzania likafilisika hadi kuuzwa!.
- Akatibuana na mmiliki wa Channel Ten, Muitaliano, Franco Tramontana, Franco alitimuliwa nchini!.
- Akatibuana na Lowasa, Mengi akiwa Mwenyekiti wa NEMCI, Lowasa akang'oka!.
- Alipishana kauli na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Shamin Khan, Shamim aling'olewa!.
- Alipishana kauli na Masilingi, wakati wa "mchezo mchafu", Masilingi aling'olewa!.
- Alipishana kauli na Iddi Simba kwenye mambo ya Uzawa, Iddi Simba alimwagwa!.
- Alipishana kauli na Basil Mramba akiwa waziri wa fedha kuhusu kodi ya Jack Pot Bingo, Mramba aling'oka!.
- Alipishana kauli na Adam Malima, malima amemwagwa!.
- Alipishana kauli na Tido kuhusu TV inayolipwa na kodi za wananchi kugombea matangazo na TV binafsi!, Tido aling'oka!.
- Akapisha kauli na Yusuph Manji, sasa Manji yamemkuta ya kumkuta na soon anafilisiwa!.
- Akapishana kauli na Waziri wa Mambo ya ndani, Masha, Masha kang'olewa!.
- Akatibuana Rostam Aziz, kwenye fisadi papa, Rostam sasa ameikimbia nchi!,
- Alipishana kauli na Balozi wa Uingereza kwenye kashfa ya Silvadale!, Balozi wa Uingerezwa aliondoshwa!.
- Mwandishi Eric Kabendera, alitoa ushahidi kule UK, jinsi Mengi anaingilia editorial ya media yake, Eric Kabendera alipata misukosuko ya kuhojiwa uraia wake
- Alipishana kauli na wandeshaji wa Kipindi cha "Kiti Moto", Kiti Moto kilikufa!
- Alitibuana na Ze Comedy, kipindi kimekufa!
- Ndipo sasa amekuja Prof. Mhongo!, tusubirie tuone Muhongo atadumu kwa muda gani kabla ya kumkuta, hayajamkuta!.
Watu wa karibu na Mhongo, mshaurini atubu na kwenda kuangukia mapema, watu wa Mungu sio wa kuchezea!.
Vinginevyo!.
Paskali