Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,343
- 17,887
Namna ambayo Harbinger Singh alipata hisa za Mechmar kupitia Piper Links na hatimaye PAP inaonyesha ilikuwa ya udanganyifu.
1. Wakati Piper Links ikipata hisa 70% za Mechmar katika IPTL mwaka 2010 Kampuni ya Mechmar ya Malaysia ilikuwa tayari mufilisi (Under receivership).
2. Inawezekana baadhi ya wanahisa wa iliyokuwa Mechmar waliizunguka Serikali pamoja na Mahakama Kuu ya Malaysia mpaka wakauza hisa zao
3. Inasemekana kwanza Mechmar walimuuzia Piper Links (Mali ya Harbinger Singh) ambayo ni kampuni ya kufikirika ambayo ilizitunza hisa hizo kwanza kwenye visiwa vya Virgin Island.
4. Wafilisi wa Mechmar wanasema Mkurugenzi mmoja wa iliyokuwa Mechmar Fatuk Baharudwn bin Abdul Najid alikiuka amri ya Mahakama ya tarehe 03/ 10/ 2010 kwa kuidanganya Mahakama kwa kuingia Mkataba wa u
Umiliki Hisa (Share Purchase Agreement) ya USD 9.0 Million na Piper Link Investments Ltd mnamo 09/ 09/ 2010.
5. Wafilisi walifanikiwa kufungua kesi kwenye Mahakama ya BVK ya Malaysia na waliweza kushinda kesi ya kurudisha hati za hisa.
6. Swali, Je Piper Links waliwezaje kuuza hisa kwa PAP (Mali ya Harbinger Singh) wakati kulikuwa na amri ya tarehe 03/ 04/ 2011 inayowakataza Wakurugenzi wa Piper Links kufanya miamala yeyote ya hisa za Mechmar?.
7. Je ni nyaraka zipi ambazo PAP walizitumia kuwasilisha Wizara ya Nishati na Madini kuonyesha umiliki wao wa hisa 70% za IPTL?
8.Nyaraka zinaonyesha kuwa Piper Links walinunua hisa kutoka Mechmar kwa USD 9.0 Milion na kuziuza siku hiyo hiyo kwa PAP kwa USD 300,000 siku ya tarehe 05/ 12/ 2013 ambayo ni siku moja baada ya BOT kuziachia fedha za ESCROW kwa PAP.
Harbinder Singh ana kesi ya kughushi na kuiba kisha kutakatisha fedha. Kuna haja ya kuwaunganisha Jaji Fredrick Werema (Aliyekuwa AG) na Prof Sospeter Muhongo (Aliyekuwa Waziri wa Nishati) kwa kuwa wao ndiyo waliothibitisha nyaraka za PAP na kumshawishi James Rugemalira wa VIPEM kuuza hisa zake 30% kwa PAP.