Dr. Nchimbi kaniacha kinywa wazi

Dr. Nchimbi kaniacha kinywa wazi

Hivi utamwambiaje mtu aliyefungwa kamba mikono na miguu "pambania uhuru wako"?

Hao wanajua fika nguvu ya dola iko wapi. Huku kutuambia tupambane ni kutuchosha tu ili mwisho wa siku tuseme kazi imeshindikana halafu wao wabaki salama.
 
Tunaongozwa na vichaa!
Kinacholeta matokeo sio Katiba bali kiongozi bora. Marekani wana Katiba nzuri lakini wanalia na uongozi wa Trump, wanalia na tume ya uchaguzi. Pale Kenya tunawasifu wana Katiba nzuri lakini kelele zao zinatuzidi sisi.
Hii Afrika ni kapu la mjinga wajanja wengi wanatia mikono yao. Hata wazungu wamefika kule waliko leo sio kwa demokrasia na haki kwa watu wao. Demokrasia na haki inapunguza uzalishaji na faida, hivyo walianza kwa watumwa, ajira za mpaka watoto kwa masaa mengi ya siku na wiki. Hata sasa wanapata faida kwa kuiba kutoka mataifa mengine. Yaani demokrasia na haki zao kwenye mataifa yao zinagharamiwa kwa wizi wa mafuta madini na rasilimali nyingine kutoka mataifa mengine. Kenya demokrasia inawashindisha barabarani wakiandamana kila wiki na kuchoma mali zao wenyewe. Hawamjui adui wao halisi wanadhani ni Katiba na Ruto, wanataka kuandika tena.
 
Shida nyingine ni kwamba hatujui tunataka Katiba nzuri kama ya nchi gani. Hakuna mtu nchini ambae Katiba hii imemzuia kutajirika, kusali, kuoa, na kujenga nyumba. Tuna Katiba ambayo inamhakikishia kila mtu kulala nyumbani kwake kuamka na kushinda salama bila hofu. Katiba ambayo kila mtu anaweza kutoa ahadi ya kutimiza mwaka kesho. Kuna vitu vichache sana vya kuondoa na kuongeza kwenye Katiba hii ambavyo havihitaji watu kupambana, kuumizana na kuuana.

Tunahitaji Katiba ambayo itamnusa kwelikweli mtu ambae anataka kuwa kiongozi wa nchi pamoja na chama chake.
 
Mkuu katiba sio suala la kula na kulala tu, ni kweli haituzuii kujenga nyumba, lakini ina nguvu ya kuamua kama hiyo nyumba yako itabomolewa kesho bila fidia stahiki kupitia sheria za hovyo. Katiba nzuri haikuhakikishii utajiri, bali inatengeneza uwanja sawa wa kiuchumi ili ukifanya biashara usiumizwe na kodi za kinyonyaji au ukiritimba unaolindwa na wakubwa.

Katiba yetu ya sasa inampa Rais madaraka makubwa kupitiliza. Anaweza kuteua kila mtu, kuanzia majaji wa mahakama hadi wakurugenzi wa uchaguzi. Hii ina maana gani? Mfumo wetu hautegemei taasisi imara, unategemea tu wema wa mtu mmoja aliyepo madarakani. Akiamka vibaya leo, maisha ya mamilioni yanaweza kuvurugika na hakuna chombo cha kumuwajibisha kisheria.

Hii ni mbaya sana.
 
Huna akili ya kunizidi mm wewe, hata kwa robo tu, unaendeshwa na mkumbo, mm sina upande wowote naongea facts tu kwakutumia uelewa wangu na uzoefu wangu tu baaasi.
Wewe huna haha ya kujieleza.
Maandiko yako yanakuelezea uwezo wako.
Ikiwa mkubwa au mdogo.
 
Athari ya katiba ipo palepale tu bila kujali unaijua au huijui.
Athari hutokana na kutoijua katiba. Tuhakikishe kila mtanzania au angalau ¾ ya watanzania wanaijua katiba iliyopo. Ili wakati tunajadiri mapungufu, iwe rahisi kulibeba kwa pamoja.

Leo hii mtanzania wa kawaida haoni umuhimu wa kudai katiba kwasababu hata haelewi katiba ni nini. Ndio maana unaona wanaachiwa wanaharakati na vyama vya siasa kwasababu wao wanafuatilia kuhusu haki zao.

Mtanzania wa kawaida anapambania hela ya madawa hospitalini, hela ya chakula kwa familia, hela ya mahitaji ya shule kwa mtoto wake. Kula yake anaipata kwa siku. Akitoka ndo ale. Ukimuambia habari za kudai katiba anakushangaa kwasababu anadhani sio hitaji lake la msingi
 
Mchakato utafia palepale kwenye aina ya muungano ulipofia wakati ule.

Katika stage hii ya uchumi wetu huwezi kuwa na katiba ambayo inaruhusu uchaguzi mkuu kufutwa na mchakato kuanza upya. Hatuna hela hiyo bado.
Katiba itakayopatikana huku ccm wakiwa wamenuna na kukunja uso huku wakiwa wanasonya hiyo ndio katiba bora
 
Kama Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dr. Samia anataka Katiba mpya, Makamu wa Rais anataka Katiba mpya, sasa ni nani anapinga Katiba mpya kiasi cha Makamu wa Rais Dr Nchimbi kuwataka wananchi wapambane kudai katiba mpya?.

Angalau sasa tunajua ni nani aliyechomekeza kwenye Ilani ya CCM agenda ya Kuandika katiba Mpya. Ambacho ameniacha mdomo wazi ni kuhusu:

1. Nani hataki katiba mpya pale CCM na serikalini kama Rais na Makamu wake wanataka Katiba mpya?
2. Kama mwenyekiti wa CCM anataka Katiba mpya nani pale CCM hataki Katiba Mpya?
3. Wananchi wapambane dhidi ya nani ili wapate Katiba mpya?
4. Wananchi wapambaneje ili kuwazidi nguvu hao wasiotaka katiba Mpya?
5. Tunataka Katiba mpya nzuri kama ya taifa gani Afrika ili tuone wao ni bora kiasi gani wapi kuliko sisi?
6. Je, ubaya wa Katiba hii ya 1977 ni nini?

Nionavyo mimi kama mimi, watu wetu, uchumi wetu, uelewa wetu, kiwango cha elimu cha watu wetu, mila na ustaraabu wetu kupanua kiwango cha demokrasia na haki za watu wetu kuliko hivi tulivyo sasa kutaenda kulitumbukiza taifa kwenye migogoro mingi itakayoidumaza Tanzania. Tunakwenda kutanua uchochoro ambao wakoloni watapitia kuichukua tena Tanzania.

Mwl. Nyerere alikataa kuruhusu wazungu kuchimba sana madini yetu kwakuwa alikuwa anawafahamu watu wake kuwa hawakuwa na utaalamu wa kuyachimba wala elimu ya kujadiliana kuhusu mikataba ya uchimbaji. Watu wetu hawa wengi wao bado hawana uelewa mpana kuhusu demokrasia na haki. Bado kuna maeneo watu wanaona ni haki kwa mwanamke kunyimwa kumiliki hiki na kile, bado mpaka leo kuna watu wanaamini viungo vya binadamu vinaleta utajiri kwa njia za giza. bado kuna watu asubuhi kabisa wanakunywa pombe na kucheza pool siku za kazi.

Sipingi kuandika katiba mpya lakini Makamu Rais Dr Nchimbi ndiye aliyeniogopesha zaidi.

View: https://youtu.be/Y30BPBHftaE?si=E11qcCE9cMml3Wfw

Kisamia ndiyo hakitaki katiba mpya, kilishasema Katiba ni “kijitabu” tu
 
Mkuu katiba sio suala la kula na kulala tu, ni kweli haituzuii kujenga nyumba, lakini ina nguvu ya kuamua kama hiyo nyumba yako itabomolewa kesho bila fidia stahiki kupitia sheria za hovyo. Katiba nzuri haikuhakikishii utajiri, bali inatengeneza uwanja sawa wa kiuchumi ili ukifanya biashara usiumizwe na kodi za kinyonyaji au ukiritimba unaolindwa na wakubwa.

Katiba yetu ya sasa inampa Rais madaraka makubwa kupitiliza. Anaweza kuteua kila mtu, kuanzia majaji wa mahakama hadi wakurugenzi wa uchaguzi. Hii ina maana gani? Mfumo wetu hautegemei taasisi imara, unategemea tu wema wa mtu mmoja aliyepo madarakani. Akiamka vibaya leo, maisha ya mamilioni yanaweza kuvurugika na hakuna chombo cha kumuwajibisha kisheria.

Hii ni mbaya sana.
Aaa kaka unaijua thamani halisi ya ardhi wewe kama ukitaka nyumba yako isibomolewe na serikali? Nyumba ngapi zimejengwa kwa viwango vya kihandisi?

Watanzania wangapi wanataka katiba mpya. Siwabezi wale wanaopinga kuandika Katiba mpya. Wanaodai Katiba mpya leo ni wale wanaodhani Katiba hii inawazuia kwenda Ikulu tu baasi. Na kama wangefanikiwa kuingia Ikulu kwa Katiba hiihii wasingeibadilisha pia na CCM wangeisoma namba vilevile pia. Hii ni survival of the fittest. Nitashangaa kama CCM watakubali kirahisi kuwa the weakest kwenye survival battle kwa hiari yao.
 
Kisamia ndiyo hakitaki katiba mpya, kilishasema Katiba ni “kijitabu” tu
Wewe hata hujui, Samia alikuwa muumini mkuu wa demokrasia pana kwasababu yeye ana exposure kubwa kuliko baadhi ya wahafidhina ndani ya CCM. Hata aliposema anavifungulia vyama vya upinzani walimpinga sana. Samia alitaka ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa aanze mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya. Hata hivyo wahafidhina ndani ya chama chake walipata nguvu baada ya mazoba kufanya vurugu siku ya uchaguzi na kuichoma nchi ambayo wamejabidhiwa kuilinda kwa nguvu zote. Watu waliokosea kupitiliza ni wale waliofanya vurugu kutaka kumpindua. Hata angekuwa mm kwa kutumia common sense nisingekubali kukaa meza moja na mtu aliyetaka kunipindua kuandika Katiba hadi hapo ukweli wote utakapokuwa wazi na wahusika kuadhibiwa.
 
Aaa kaka unaijua thamani halisi ya ardhi wewe kama ukitaka nyumba yako isibomolewe na serikali? Nyumba ngapi zimejengwa kwa viwango vya kihandisi?

Watanzania wangapi wanataka katiba mpya. Siwabezi wale wanaopinga kuandika Katiba mpya. Wanaodai Katiba mpya leo ni wale wanaodhani Katiba hii inawazuia kwenda Ikulu tu baasi. Na kama wangefanikiwa kuingia Ikulu kwa Katiba hiihii wasingeibadilisha pia na CCM wangeisoma namba vilevile pia. Hii ni survival of the fittest. Nitashangaa kama CCM watakubali kirahisi kuwa the weakest kwenye survival battle kwa hiari yao.
Mkuu kwani wanaotaka Katiba Mpya ni akina nani? Sio wanasiasa pekee yao Mkuu, nenda kawaulize wakulima wa korosho au pamba wanaopangiwa bei na serikali na kukatwa kodi bila ridhaa yao. Nenda kawaulize wafanyabiashara walioporwa akaunti zao za benki kupitia kesi za mchongo za plea bargaining miaka ya nyuma. Hawa wote hawawazi kwenda Ikulu, wanawaza usalama wa jasho lao kwanza, mfumo wa sasa unamfanya kila mtu awe hatarini wakati wowote anapotokea kiongozi asiyejali kama huyu wa sasa.

Halafu hii sio vita ya CCM na Wapinzani, ni ya Wananchi na Mfumo, ukisema CCM wasikubali kuwa dhaifu, hapa unakuwa unaangalia kama vile mchezo ni wa timu mbili tu uwanjani. Lakini mmiliki wa uwanja ni mwananchi. Katiba sio duka la mtu binafsi ambalo CCM wanatufanyia hisani kutupa, ni mali yetu. Nchi inapokosa mifumo imara ya haki, hata hao wana-CCM wenyewe wanakuwa hatarini. Kumbuka jinsi viongozi na wafanyabiashara wengi wa CCM walivyonyoroshwa na kuteseka kwenye awamu zilizopita kwa sababu tu hakukuwa na katiba ya kuwalinda dhidi ya mamlaka ya mtu mmoja.
 
hata huyo ana bosi wake pia, hivyo ni kosa na kujidaganya kuamini kwamba ni inchaji wa chochote hapa tanzagiza, anatumika tu ...
Mbona inasemwa sana kwamba yeye ndiye mastermind wa yanayoendelea?

Boss wake ni yupi huyo anaemtumia 'mastermind '?

Ni yule swaiba wake wa miaka na miaka?
 
Kinacholeta matokeo sio Katiba bali kiongozi bora. Marekani wana Katiba nzuri lakini wanalia na uongozi wa Trump, wanalia na tume ya uchaguzi. Pale Kenya tunawasifu wana Katiba nzuri lakini kelele zao zinatuzidi sisi.
Hii Afrika ni kapu la mjinga wajanja wengi wanatia mikono yao. Hata wazungu wamefika kule waliko leo sio kwa demokrasia na haki kwa watu wao. Demokrasia na haki inapunguza uzalishaji na faida, hivyo walianza kwa watumwa, ajira za mpaka watoto kwa masaa mengi ya siku na wiki. Hata sasa wanapata faida kwa kuiba kutoka mataifa mengine. Yaani demokrasia na haki zao kwenye mataifa yao zinagharamiwa kwa wizi wa mafuta madini na rasilimali nyingine kutoka mataifa mengine. Kenya demokrasia inawashindisha barabarani wakiandamana kila wiki na kuchoma mali zao wenyewe. Hawamjui adui wao halisi wanadhani ni Katiba na Ruto, wanataka kuandika tena.
Propaganda kama hizi zilipitwa na wakati kitambo sana. Amka, hakuna wajinga tena.

Wahenga walisema wakati ni ukuta. Ccm kwa sasa inapumulia mbeleko ya vyombo vya dola tu, haitakiwi. Ina survive kwa kuteka, kuuwa wananchi wasio na hatia na kuwabambikia kesi za uongo
 
Athari hutokana na kutoijua katiba. Tuhakikishe kila mtanzania au angalau ¾ ya watanzania wanaijua katiba iliyopo. Ili wakati tunajadiri mapungufu, iwe rahisi kulibeba kwa pamoja.

Leo hii mtanzania wa kawaida haoni umuhimu wa kudai katiba kwasababu hata haelewi katiba ni nini. Ndio maana unaona wanaachiwa wanaharakati na vyama vya siasa kwasababu wao wanafuatilia kuhusu haki zao.

Mtanzania wa kawaida anapambania hela ya madawa hospitalini, hela ya chakula kwa familia, hela ya mahitaji ya shule kwa mtoto wake. Kula yake anaipata kwa siku. Akitoka ndo ale. Ukimuambia habari za kudai katiba anakushangaa kwasababu anadhani sio hitaji lake la msingi
Nakuunga mkono 100%. Kama tusipokuwa makini tunaweza kutengeneza Katiba yenye manufaa kwa wanasiasa wachache tu wanaotaka kwenda Ikulu kwa sababu zao na shida za wananchi zikabaki zilezile au kuongezeka zaidi badala ya kupungua. Unatengeneza Katiba ambayo kila sehemu inashikwa na kabila moja tu.
 
Propaganda kama hizi zilipitwa na wakati kitambo sana. Amka, hakuna wajinga tena.

Wahenga walisema wakati ni ukuta. Ccm kwa sasa inapumulia mbeleko ya vyombo vya dola tu, haitakiwi. Ina survive kwa kuteka, kuuwa wananchi na kuwabambikia kesi za uongo
Huwezi kumdanganya kijana kwamba Katiba mpya itamnyang'anya bodaboda na kumpatia lori la kubebea mizigo. Kelele za Katiba hazitoki kwa wananchi ambao ndio wengi, zinatoka kwa wanasiasa wanaoenguliwa kugombea wakati wa uchaguzi. Uandishi wa katiba wa aina hiyo ni upumbavu kabisa.

Tangu tume ya Warioba iundwe imeshapita miaka 15 sasa, hivyo hata findings zake zimeshapitwa na wakati. Miaka 15 iliyopita kuna watu wazima wengi wameongezeka sasabambao miaka 15 iliyopita walikuwa watoto, hawakutoa maoni yao. Hivyo lazima mchakato wa Katiba uanze upya ili kuja na matokeo ya hivi karibuni (uptodate findings). Yaani elimu ya Katiba lazima itolewe upya kwa watu wote ili kupata maoni mapya na kuondoa maoni yaliyopitwa na wakati.

Kamanukisema tunaanzia pale tulipoishia kuna watanzania wengi sana ambao hawakuwepo/walikuwa watoto wakati huo ama watatushangaa au tutawaacha nyuma sana kwenye zoezi.
 
Mkuu kwani wanaotaka Katiba Mpya ni akina nani? Sio wanasiasa pekee yao Mkuu, nenda kawaulize wakulima wa korosho au pamba wanaopangiwa bei na serikali na kukatwa kodi bila ridhaa yao. Nenda kawaulize wafanyabiashara walioporwa akaunti zao za benki kupitia kesi za mchongo za plea bargaining miaka ya nyuma. Hawa wote hawawazi kwenda Ikulu, wanawaza usalama wa jasho lao kwanza, mfumo wa sasa unamfanya kila mtu awe hatarini wakati wowote anapotokea kiongozi asiyejali kama huyu wa sasa.

Halafu hii sio vita ya CCM na Wapinzani, ni ya Wananchi na Mfumo, ukisema CCM wasikubali kuwa dhaifu, hapa unakuwa unaangalia kama vile mchezo ni wa timu mbili tu uwanjani. Lakini mmiliki wa uwanja ni mwananchi. Katiba sio duka la mtu binafsi ambalo CCM wanatufanyia hisani kutupa, ni mali yetu. Nchi inapokosa mifumo imara ya haki, hata hao wana-CCM wenyewe wanakuwa hatarini. Kumbuka jinsi viongozi na wafanyabiashara wengi wa CCM walivyonyoroshwa na kuteseka kwenye awamu zilizopita kwa sababu tu hakukuwa na katiba ya kuwalinda dhidi ya mamlaka ya mtu mmoja.
Hata sijui, sisi huku kijijini naona vumbi linatimka tu watu wanachimbia nguzo za kusambaza umeme kwenye vitongoji. Wananchi akiwemo bibi hasemi chochote zaidi ya kutaka matibabu ya mgongo wake.

Katiba mpya tunaiona youtube tu akina naniliu wakisema. Vipaumbele vyetu huku hafifanani na vipaumbele vyao.

Baada ya kuona vurugu huko mijini tumepata woga wa kila kitu.

Kama Museveni yuko kwa miaka yote ile kumbe hata CCM ina afadhali kubwa kwa kubadilisha viongozi kila miaka 10. Serikali ya nusu mkate kati ya CCM na Jeshi nadhani ndilo suluhisho kwasasa hadi 2050 tutakapokuwa tumekomaa zaidi kisiasa

View: https://www.youtube.com/live/CWeTDEkFWwI?si=9SfBmfBaxAh7Dupz⁸
 
Back
Top Bottom