Dr. Nchimbi kaniacha kinywa wazi

Dr. Nchimbi kaniacha kinywa wazi

Kuna namna umeongea ukweli Mkuu, lakini hemu jiulize. Hivi kama katiba ingeruhusu mgombea binafsi, ungepoteza muda wako kusikiliza hivyo vyama unavyoviita vya kidini au kikabila?

Tatizo lililopo sio upinzani kwenda Ikulu au CCM kubaki madarakani Mkuu. Ishu ni jinsi mifumo inavyomlinda mwananchi wa kawaida asiyekuwa na chama wala cheo.
Uko sahihi mkuu, lakini shida yetu kuu ni kuwasikiliza watu ambao wanatamani CCM ishindwe tu na mtu yeyote bila kujali huyo mtu ana sera gani kwetu tofauti na CCM, yaani wameichoka tu CCM. Hii inaweza kuwa hatari kubwa sana kwakua hakuna mgombea binafsi anaeweza kushinda uchaguzi bila kupewa msaada na watu wazuri au waovu kufika Ikulu. Anaweza kupata msaada wa kwenda Ikulu kutoka kwa wauza madawa ya kulevya, wahalifu au watu wa nje ya nchi wenye agenda zao.

Jamani Kabla ya kuichalenge hii Katiba yetu iliyopo hebu tumfikirie kwanza Nyerere ambae aliiandika. Nyerere hakuwa mjinga wa kiasia hiki. Nyerere ni levels za akina Abraham Linkon, Henry Kisinger, Mao, Fidel Cartrol, Mnrumah, nk. Tusimlinganishe Nyerere na Heche, Nchimbi, Bagonza au Warioba. Tutafanya kosa la kiufundi kama tutafikiria hivyo.

Nyerere alijenga taifa linalofanana na China na Soviet kwa muonekano, sisi tunataka kujenga taifa linalofanana na Marekani, Vatican, Ubelgiji na Canada kama ilivyo Kenya. Hii itakuwa ni U-Turn kubwa sana ambayo kwavyovyote vile haitatuacha salama. Role model wetu sisi ni China na Russia sio Marekani na Ulaya.

Tuangalie mapito na mwelekeo wa ⁸ Nyerere zaidi kuliko mapito na mwelekeo wa Oscar Kambona. Tuangalie mapito ya China kuliko mapito ya Ulaya na Marekani.

Sorry to say this, kama ukiwasikiliza Kanisa na chadema ya Mzee Mtei utagundua kuwa wanaendeleza mapambano yaleyale ya akina Nyerere dhidi ya Kanisa na ubepari. Nyerere alitofautiana sana na Kanisa, Mtei na Kambona juu ya kuachana na ubepari na kuelekea Uchina na soviet. Hebu sasa sikia Jumuiya na Ulaya ndiyo eti inatuonea huruma sisi. Waliokoka lini?

Tunajua Kanisa ni zao la ubepari, limeletwa na watu wanaoamini kwenye ubepari, na watendaji wake wanapata mafunzo kutoka nchi za kibepari Itay.
 
Mkuu China ya Mao Zedong haikuwa na uchumi imara hadi alipokuja Deng Xiaoping miaka ya 1980 na kufanya mabadiliko makubwa ya mifumo ya kiuchumi. Waligundua kuwa huwezi kuendesha nchi ya kisasa kwa kutumia sheria za zamani. Hata sisi, kudai Katiba Mpya sio kwa sababu tunaiiga Marekani au Ubelgiji, tunataka kuboresha mifumo yetu ili iendane na soko la sasa na teknolojia.

Mkuu umejiuliza ni mfumo gani unaoweza kumdhibiti mlafi asihonge akifika Ikulu? Ni Katiba imara yenye taasisi huru kama TAKUKURU, Polisi, na Mahakama zisizofungamana na upande wowote. Chini ya katiba ya sasa, kama mhalifu akifanikiwa kuingiza mtu wake Ikulu kwa njia yoyote ile, huyo mtu anakuwa na nguvu zote na hakuna chombo chochote kinachoweza kumzuia. Tunataka katiba mpya ili hata akija kiongozi mbaya, taasisi zimfunge asiweze kabisa kuiuza nchi.

Nyerere mwenyewe alikubali mabadiliko. Tukumbuke kuwa mwaka 1992, Nyerere huyu huyu ndiye aliyesimama na kuishauri CCM ikubali mfumo wa vyama vingi baada ya kuona upepo wa dunia umebadilika, ingawa asilimia kubwa ya wana-CCM walikataa. Nyerere aliamini katika kujifunza na kubadilika kulingana na wakati. Kama angekuwepo leo, akiona jinsi rasilimali zinavyopotea na jinsi wananchi wanavyolalamika chini kwa chini, yeye mwenyewe angekuwa mstari wa mbele kushauri tuboreshe katiba yetu ili kulinda kile alichokiasisi.
 
Sawa nalijua hilo kwamba Xi ndiye aliyekuja kuleta mapinduzi ya sasa. Hivyo na sisi tungekwenda China leo tukajifunzi nini kimo kwenye Katiba yao hakimo kwenye Katiba yetu, nini wameachana nacho na kipi wameongeza kwenye Katiba yao kinachoweza kufaa kwetu ili tukiongeze ili tuwe kama China ya leo. Tunachotaka kukosea ni kwamba tunataka kuachana na China na kuelekea EU, Jumuiya ya Madola na marekani kama akina Kambona na wahuni wengine. Sisi ni mashahidi mataifa ambayo baada ya uhuru yalielekea upande wa wakoloni wao yanahangaika vibaya sana. Mfano ni Kenya, malawi,. DRC, Sahel countries, Nigeria, Congo, Cameroon, Senegal, nk wanahangaika kutaka kujitenga nayo lakini hawawezi.

KATIBA yetu ndiyo iliyotupatia ahueni hii tunayoiona sasa. Hakuna Katiba ambayo haina kasoro duniani, lakini katiba yetu ina nafuu kubwa sana; kila mtu anaweza kumiliki ardhi na kujizalishia chakula chake mwenyewe. Kwetu huku hatuna homeless kama ilivyo kwa marekani na Ulaya ambako watu walala kwenye mitaro na ,magari mabovu ya zamani.
 
Mkuu Kwenye katiba na mifumo ya China, huwezi kuwa kiongozi au mkurugenzi wa taasisi kubwa kama bodi ya umeme, reli, au madini kisa tu wewe ni kada maarufu wa chama fulani. Lazima uwe mtaalamu uliyesomea na aliyefanya vizuri kuanzia ngazi ya chini kabisa. Kwetu sisi, katiba inampa Rais nguvu ya kuteua mtu yeyote kuwa mkuu wa taasisi yoyote hata kama hana ujuzi nayo, mradi tu ni mwanachama mtiifu. China waliondoa huu ukada kwenye utendaji ndiyo maana wanaendelea sana.

Xi Jinping amesifika sana duniani kwa kampeni yake ya Kuwawinda wala rushwa wakubwa na wadogo. Kwenye katiba na sheria za China, kiongozi yeyote hata awe rafiki wa kiasi gani na Rais akigundulika amehujumu miundombinu au kuiba hela ya umma, adhabu yake ni kifungo cha maisha au kifo. Mifumo yao ya uchunguzi haisikilizi maagizo kutoka juu. Kwetu sisi, mapungufu ya katiba yanafanya taasisi za kuzuia rushwa zisiwe huru 100%, zinasubiri kibali cha Rais kuwashitaki wakubwa.

Mkuu ni kweli katiba yetu inamlinda mwananchi kumiliki ardhi kishamba. Lakini shida iliyopo sasa hivi, sheria zetu zinaruhusu viongozi wa mikoa au wilaya kuwanyang'anya wakulima ardhi zao na kuwapa wawekezaji wa nje bila wananchi kuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo kisheria. Katiba mpya tunayoitaka inalenga kuandika wazi kuwa ardhi ni mali ya wananchi, na sio mali ya kiongozi fulani.
 
Ametuchana tu ukweli kwamba bimdash anapotezea suala la katiba ili asilipotezee basi wananchi tunatakiwa tutoe mihemko vinginevyo katiba mpya tutaiskia kwenye vitabu na kuisoma kwenye radio
 
Kaka kosa la Nyerere na wenzake ni kukopi Katiba ya China lakini akaacha vifungu vinavyomuadhibu mwizi wa mali ya umma bila kujali cheo. Wasomi wetu unaowasema ndio wezi wakuu wa mali za umma, wanatumia ujuzi na uzoefu wao kutuibia. Pale bandarini ilikuwa hata umfukuze nani anaekuja hata awe nani alikuwa anatuibia. Adhabu zetu ni legelege sana na watu wamejipa kinga ya kutokushitakiwa. Tunaweza kuongeza adhabu hizi kwenye Katiba bila kupoteza muda na fedha nyingi tunazozihitaji kujenga reli ya umeme kwenda Kigoma.

Ni kweli tz tunahitaji kuwa na plantations ambazo zitalima kisasa na kuajili vijana wengi badala ya kila mtu kuwa na pori ambalo anasema ni lake lakini halilimi na hata akilima analima kizamani kwa jembe la mkono. Ardhi ni mali ya serikali hadi sasa ndio maana hata gharama zetu za kufanya maendeleo ni ndogo pia. Ni rahisi kujenga reli na barabara mpya tz kuliko Kenya. Tuitumie hiyo fursa kupiga hatua za kimaendeleo haraka kabla hatujachelewa. Kenya kila kipande cha arshi ni mali ya mtu ambae anaweza kugoma bomba lisipite kwake au nguzo ya umeme isikitwe kwake.
 
Muda huongea...

Cc: Mahondaw
Tunachotaka kufanya ni kumkufuru mwenyezimungu kwa hiki alichotupatia kupitia Katiba hii ya 1977. Tunadhani kuwa hivi tulivyo sasa ni kwa sababu ujinga, woga, upole na uzuzu wetu watanzania. Hatuamini kama Nyerere alikuwa zawadi pekee ambayo tulipewa sisi tu kutoka kwa MwenyeziMungu. Watu wanahoji kwanini hatupigani wanataka tupigane ili kuonyesha kuwa hata sisi sio wajinga na wapole kama wenzetu Kenya, DRC na Ulaya.
 
Ametuchana tu ukweli kwamba bimdash anapotezea suala la katiba ili asilipotezee basi wananchi tunatakiwa tutoe mihemko vinginevyo katiba mpya tutaiskia kwenye vitabu na kuisoma kwenye radio
Katiba mpya haijengi viwanja kama hivi. KATIBA ni muhimu sana lakini sio kipaumbele namba moja kwetu kwa sasa. Kanzu tunayo tunatafuta kilemba tu.

Nchi haijawahi kupata kuwa na Rais mchapakazi kama Samia tangu tupate Uhuru.

View: https://youtu.be/Sb8F8LwIuww?si=p3Z6nVmsHASevZxf
 
So you need plastic mouth surgery reconstruction

Mandible or maxilla where should they start
Mabadiliko hayazuiliki muda wake ukifika. Tuendelee kula mtori nyama tutazikuta huko mbele ya safari. Huu ni muda wa kuwabembeleza watawala waongeze vyuo na fedha za mikopo kwa vijana wengi ili idadi ya watanzania wenye elimu ya kutosha iwe kubwa kuliko sasa. Kijana akiwa na elimu ya kutosha huwezi kumdanganya achome ofisi ya serikali yenye mafaili yao ya viwanja vyao akakukubalia kiboyaboya. Kijana akiwa na elimu anajua anachokitaka na asichokitaka kwenye Katiba na lhakuna mtu wa kumzuia kupata Katiba aitakayo.

Kelele za sasa za Katiba zinatoka na kuongozwa na watu wanaolenga ibara za Katiba zinazohusiana na Tume ya uchaguzi ili iwe rahisi wao kwenda Ikulu hata kama hawana cha kufanya watakapofika huko; wanataka maslahi kama wanayopata CCM sasa, baaasi.
 
Ametuchana tu ukweli kwamba bimdash anapotezea suala la katiba ili asilipotezee basi wananchi tunatakiwa tutoe mihemko vinginevyo katiba mpya tutaiskia kwenye vitabu na kuisoma kwenye radio
Kwani kuandika katiba mpya mpaka ikamilike kunaweza kutugharimu Tsh ngapi?
 
Hicho kinywa kipo wazi saza tunaweza ingiza ndizi au tango...kirahisi kabisa
Wapi umewahisikia Katiba mpya inakamata wezi? Trump alipoingia madarakani kwenye awamu ya pili alikuta upigaji mkubwa wa pesa hadi akaamua kuyafuta mashirika ya misaada yote. Alikuta mfuko wa social security unalipa mtu mwenye umri wa miaka 220, pesa zinaliwa.

Ni mjinga pekee atakubali kwamba Katiba yetu ndiyo sababu ya tz kuwa na maendeleo duni na watu kukosa haki zao. Kelele za Katiba zinahanikizwa zaidi na watu wenye mgogoro na tume ya uchaguzi wanaodhani tume ndiyo inayowazuia kwenda Ikulu na watu wasioutaka Muungano, baaaaasiiiiiii!!

Wananchi hawana shida na Katiba, tena hata kuiona hawajaiona sembuse kuisoma.
 
Nachomaanisha ni kwamba hata hii katiba iliyopo sasa uzuri na ubaya wake unatuathiri wote bila kujali wenye kuijua au kutokuijua, hata kama mimi siijui hii katiba iliyopo ila yale yenye kuelezwa kama mapungufu ya hii katiba inabaki kuwa ndio ukweli huo hata kama mimi sina uelewa nalo hilo, na endapo ikija katiba mpya ambayo imerekebisha yale mapungufu yaliyokuwepo kwenye katiba ya sasa faida zake tutazipata wote na si kwa wale wenye uelewa na hiyo katiba tu.

Kwahiyo inawezekana kabisa katika hayo ambayo mtanzania wa kawaida anayapambania kila siku akaja kuona mabadiliko katika hayo mambo anayoyapambania kama athari ya mabadiliko ya katiba.
Sawa, hata kama wewe hujui uzuri wa hii Katiba basi angalia hapa. Afrika na dunia inabaki vinywa wazi. Eti mtu anataka tuache kufanya haya ili tutumie fedha za kujenga hii tuandike Katiba.

Chondechonde Samia wewe tujengee reli wajao akina Dr. Katiba wataandika Katiba.

View: https://youtu.be/m1V4GDBBcQw?si=CpmzkArZk2qEfy3h
 
Back
Top Bottom