Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Pale kosa la chama linapohalalisha kosa la mtukufu yohana wa chato
Hakuna kosa la Chama lililofanyika. Anachofanya Mwakyembe ni kuhalalisha uvunjwaji wa Katiba anaofanya mkuu wake kwa kutoa visingizio vya kitoto. Kumkaribisha Mhe. Lowasa katika Chama kulifuata taratibu zote za vikao vya kikatiba. Naomba Mwakyembe kama yumo humu athibitishe ni vipengele vipi vya Katiba ya Chadema vilivunjwa.
 
Ukiwaangalia wasomi kama Dk. Mwakyembe na Profesa Lipumba utagundua kuwa Elimu yetu imeshuka sana thamani.
 
kwa taarifa yako watawala hawaogopi mahakama bali nguvu ya umma huku Africa. Huku kwetu mahakama zinatekeleza sheria kwa utashi wa mtawala. huo ndio ukweli.

"Tindo" nguvu ya umma karne hii! Kuharibiana mali (km Pemba), matusi, uwongo na uchochezi, nk vitendo vinavyopelekea uvunjifu wa amani, ndio nguvu ya umma. Mimi nasema HAPANA.

Kwa mtazamo na imani yako hiyo "tindo" sina la kukujibu zaidi ya kukushauri, wenye fikra kama za kwako, njia sahihi ni kusubiri Katiba mpya ya JMT labda itatoa uhuru zaidi wa mahakama.

Hivyo basi, maneno na vitendoni vya kuhamasisha kupinga uvunjifu wa Katiba iliyopo, inayoipa madaraka mahakama kusikiliza na kulitolea uamuzi suala lolote lihusulo uvunjifu wa Katiba, ni batili.
 
Akili ni nywele,kila mtu ana zake.Sasa kama watu wanakuwekea "sumu" unanyonyoka nywele zote unabaki kichwa kama shingo ya kuku aina ya kuchi...Huwezi kufikiri vizuri.

Kuna majizi sana nchi hii....Huyu anapata moral authority gani wakati alinunua mabehewa feki?Huyu si ndio alimleta yule "muhuni" wa Marekani na mradi wa train ya mwendokasi ya Posta hadi Airport halafu kumbe ni tapeli tu.

Huwezi kumuita Dr(PhD) wakati anakata bandiko lake juu ya Serikali 3 lililompa sifa ya kuwa Dr...Kuomba maandamano kwa kibali ni kuvunja katiba?!!Kweliii!!!Yaani Rais kuzuia mikutano ya siasa na vikao vya ndani vya vyama vya siasa sio uvunjaji wa katiba?

Magazeti yaliyofungiwa na Serikali yake ya Mwanahalisi na dada yake Mseto ndio yale aliyoyatumia kama "Hadidu za Rejea" kutengeneza ripoti ya Richmond iliyomuondoa mmbaya wake Eddo kwenye u-PM...na ndani ya Report ile Mwakyembe anayashukuru magazeti haya kwa kuwasaidia kupata habari za report yao kwa % kubwa.

Leo anashabikia uminyaji wa vyombo vya habari vilivyompa huo "umaarufu njaa" aliokuwa nao.If that is the case...Basi hata yeye ile report yake imepoteza "uhalali" wake.Watu wanajiita wasomi lkn wamejaa ukurutu wa unafiki mwanzo mwisho!!Nyakati zitawahukumu....Leo JK na mambo yake yote,lkn wakati unampa nafasi ya kumuona kama "Mwanademokrasia" na "Mwanadiplomasia" mzuri ktk uongozi wake.Huyu akirudi kufundisha akiulizwa nini maana ya "Freedom of Speech",sijui atasema "kuzuia maandamano ya vyama","kufungia magazeti","kuzuia vyama vya siasa kufanya vikao" au nini?Hovyooo kabisaa wasomi aina hii
Na alaaniwe Mwakyembe, na watu wote waseme, Amina
 
Time will tell Ndg Waziri kila kitu kitakuwa kwenye maandiko na historia itawahukumu wengi. Ufike wakati viongozi muwe wakweli na zaidi muwe na huruma kwa nchi yenu sio kupakana mafuta na mgongo wa chupa wakati ukweli upo wazi!
 
Haingii ajili kuwa Dr mzima kama huyu a naweza kuongea kama hivi,masking Tanzania yangu
 
siye maamuma wa mambo ya sheria tumeambiwa (na tumeamini) kuwa rais amevunja katiba kwa jinsi anavyoi-treat opposition camp, nk.

sasa hii ya Mwakyembe kusimama bungeni na kutamka bayana kuwa rais hajavunja katiba siyo suala la kulifanyia mzaha. kwa nafasi ya bunge katika katiba yetu tamko la Mwakyembe kupitia chombo hiki is a very serious "declaration" (it's tempting to term it an "allegation" but maybe it is not until legally (un)proven).

so response ya opposition isiishie kujibizana na Mwakyembe kupitia majukwaa bali kwa kupitia process iliyoainishwa kikatiba ili ku-prove kuwa kweli rais ameisigina/hajaisigina katiba. what is the problem with this approach? kuna wanasheria wabobevu kwenye eneo la katiba wengi tu - watumike hawa!
Nakubaliana na wewe asilimia mia. Wakinyamaza kabisa itakuwa ni kweli Rais hajavunja kipengele chochote cha Katiba, hivyo matamko yoyote nje ya Bunge yatakuwa ni kelele za uanaharakati usio na maana. They must act now, and act accordingly.
 
Watu wanajiondoa ufahamu kwa sababu ya msosi,katiba inavunjwa,sheria zinakiukwa lakini watu hawaoni kwa sababu ya kutetea msosi,wangekuwa ni wapinzani wamefanya hivyo ungemsikia Mwakyembe angefufua mpaka sheria zilizo kufa Ili kuwadhibiti wapinzani,sababu ya nini,msosiiiii,Yuda alimsaliti Bwana Yesu kwa vipande vya fedha thelathini kwa sababu ya msosi,watanzania tunasalitiwa kwa sababu ya msosi.
wacha domokaya. sema sheria gani au katiba imevunjwa wapi. mnamfuata lissu mnadhani huyo ni mzima? kwanza mjifunze kufuata katiba yenu ili msiokoteze wagombea urais.
 
Hta uzalendo unapungua, mtu akiona watu wanageuza nchi kuwa ya kwao binafsi sidhani kama watakuwa wanajali chochote kuhusu nchi hii, badala yake ni kukaa na kuwasubiria wafeli kisha kuwazomea, ndio wananchi wamekuwa hivyo siku hizi, kwa kuwa watu wanafanya wanachotaka na ukiwahoji wanakupuuza pengine hata kukufunga
Ni kweli kabisa uzalendo unapungua sana kwani ikiwa watu hawashirikishwi huku wakidhulumiwa haki zao za kiraia na kisiasa, unategemea nini isipokuwa kukaa pembeni na kusubiri anayejibinafsishia nchi ashindwe ili kila raia aseme, "Tulijua atashindwa, ila lilikuwa ni suala la muda tu"
 
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
Waziri anajibu kama sio waziri jaman tena bungeni utafikiri hana mamlaka. sisi aliyetuloga nahis kashafariki.
 
Ukiwaangalia wasomi kama Dk. Mwakyembe na Profesa Lipumba utagundua kuwa Elimu yetu imeshuka sana thamani.

Lakini wote wawili ni graduates wa richest and most powerful countries in the World, Mwakyembe(PhD) kasoma Ujerumani na Lipumba (PhD) kasoma USA, hivyo wewe na ombaomba wenzako ndiyo mtakuwa na matatizo!
 
Huyu mtu walimpima kwamba ubongo wake haukutikisika wakati ule?

Hivi kati ya Msigwa, Lema na Mwakyembe, aliyesema mwanzo, akapeleka rport bungeni kwa urefu, akisema Lowasa ni fisadi, na kwamba ajichunguze mwenyewe, aamue, huku akitanabahish akwamba kuna mengine mengi ameyaficha kwa malahi ya taifa, siyo huyu jamaa?

Hivi ana akil iza aina gani huyu mtu?

Si ajabu hata alipoandika paper yake akisema srikali tatu, paper ambayo iko library ikisomwa na kila mtu, kwa mategemeo ya kupata kitu cha kitaalamu, amekuja kuikana.

Na kwa nini asiondolewe PHD yake?

Hivi hawa watu wa ccm wakoje?

Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
 
Kweli "kalou" ni jina ila kila jina analochagua mtu, au kupewa na wazazi huwa na maana kubwa likiwakikisha uhalisia fulani.

Mwakyembe hatakiwi kujibu hoja ya uvunjaji wa Katiba, kwa kuwa yeye kama mwanasheria anajua sheria inamtaka mtuhumu kuthibitisha tuhuma za mtuhumiwa. Kwa hivyo basi:
1) Ni ukweli mtupu kwamba vyama vya upinzani vina wanasheria tena nguri, wameshindwaje kuandaa shauri la kimahakama lililosheheni vifungu vya Katiba vinavyodaiwa kuvunjwa!
2) Viongozi wa vyama vya upinzani vimeshindwaje kutumia wanasheria wake kuandaa Tamko la UKUTA, likinukuu vifungu vya Katiba vinavyodaiwa vimefunjwa, ili kuthibitisha ukweli huo! Au "kalou" kama unavijua hivyo vifungu, viainishe humu jamvini, tuvijadili!

Tuachane na mawazo yanayotawaliwa na kusukumwa na matamko ya "wanasiasa uchwara" ambao kila kukicha watafuta na kutumia njia za kujipatia umaarufu kisiasa.

tatizo kwa katiba yetu iliyopo Mkuu aliyeko juu analindwa kama Mungu, haguswi wala hagusiki kwa hiyo namna pekee iliyobakia ni kulalamika tu , ila kwa mwanasheria Mwakyembe kujifanya halioni hilo ni kuivunjia heshima Elimu yake ya sheria, angekaa kimya tu tungemuelewa zaidi.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa ufahamu. Afrika inaangamia kwa kukosa ufahamu. Nyerere alisema "watu wapaswa kufahaamu" Siku watu wote wakipata ufahamu waendesha farasi watatoa heshima kwa watu wote!
 
Mwakyembe (PhD) kaongea ukweli mtupu!
Mwakyembe ni hopeless.Badala ya kujibu hoja analeta siasa maji taka.
Katiba ina toa uhuru vyama kufanya mikutano ya hadhara.Rais anakataa vyama visifanye mikutano ya hadhara isipokuwa CCM.Sasa licha ya mikutano ya hadhara mpaka mikutano ya ndani imepigwa ban.
 
tatizo kwa katiba yetu iliyopo Mkuu aliyeko juu analindwa kama Mungu, haguswi wala hagusiki kwa hiyo namna pekee iliyobakia ni kulalamika tu , ila kwa mwanasheria Mwakyembe kujifanya halioni hilo ni kuivunjia heshima Elimu yake ya sheria, angekaa kimya tu tungemuelewa zaidi.

Naamini Dr (ni vizuri kutambua na kuheshimu wadhifa wake kitaaluma) Mwakyembe katumia njia na lugua ile ile wanayotumia "wanaharakati wapya kisiasa" na viongozi wa vyama vya upinzani, kile unachoita "namna pekee", kufikisha ujumbe.

Dr Mwakyembe, hivyo basi amelinda heshima yake kutokujibu tuhuma hewa, kwa kuwakumbusha wanasheria wenzake, upande wa upinzani, wawe wanaandaa tuhuma zenye kukidhi mahitaji kisheria.
 
Back
Top Bottom