Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Swala ni moral authority au kuvunjwa katiba kitu kizuri ni kwamba sheria hua hai enforce morality, pia angesema hajavunja kufungu gani angekua wa maana yani ni bora asie soma ana nafuu kuliko wasomi wa Tanzania hakuna free thinking....
mkuu wasomi watanzania njaa zinawasumbua. usiwategemee sana kwa mambo muhimu ya kulisaidia taifa letu.wengi wametanguliza tumbo mbele kuliko taifa.
 
Viongozi kama hawa sijui walifikaje bungeni anatudhalilisha wana kyela ingawa hatukumchagua alitanua goli.Full kujikomba ndiyo haya yanashiriki kuandaa miswada ya kidhalimu kama kutokuwepo kwa Fao la kujitoa,wao wameshiba,wamevimbiwa na bado wataendelea kushiba kwa sababu ya ujinga wet. Wafanyakazi tusikubali na Shangaaa akina Mgaya wapo kimya tuanze na hawa wasaliti wa wafanyakazi tukawatoe offisini,wamekuwa, wameshiba na sasa wamevimbiwa na michango yetu.Mtu aliyevimbiwa hana uwezo kufanya kazi bali muda anahangaika namna ya kupumua vizuri.Wafanyakazi tuwe pamoja tuishinde hii dhuluma,tusikae kimya tuwaonyeshe hasira zetu muda wa kuchezewa tuseme basi.
 
Mm kama mtanzania ninayejitambua sisubiri Lema au Msigwa aniambie kwamba katiba imevunjwa wakati mm mwenyewe ninaona jinsi mnavyotutawala kibabe...Maandamano ya Amani Ni haki kikatiba
 
Yaaani hawa wasomi wetu katika nchi hii jamani, Dr anaongea upuuzi waziwazi tena kwa majigambo.
Huyu hata si wakumshangaa alikana hadi utafiti wake uliompa u Dr. ndo ujue TZ kuna watu walipaswa wawe makumbusho wanaliingizia taifa hili mapato tokana na maajabu yao mfano Lipumba na nk
 
Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?

Moral Authority inaruhusu kuhoji Utashi wao wa kisiasa na kimaadili.

Ikiwa wewe unagonga Vibinti vidogo hutokuwa na Moral Authority kumkemea binti yako akiwa analiwa na Watu wazima
 
Akili ni nywele,kila mtu ana zake.Sasa kama watu wanakuwekea "sumu" unanyonyoka nywele zote unabaki kichwa kama shingo ya kuku aina ya kuchi...Huwezi kufikiri vizuri.

Kuna majizi sana nchi hii....Huyu anapata moral authority gani wakati alinunua mabehewa feki?Huyu si ndio alimleta yule "muhuni" wa Marekani na mradi wa train ya mwendokasi ya Posta hadi Airport halafu kumbe ni tapeli tu.

Huwezi kumuita Dr(PhD) wakati anakata bandiko lake juu ya Serikali 3 lililompa sifa ya kuwa Dr...Kuomba maandamano kwa kibali ni kuvunja katiba?!!Kweliii!!!Yaani Rais kuzuia mikutano ya siasa na vikao vya ndani vya vyama vya siasa sio uvunjaji wa katiba?

Magazeti yaliyofungiwa na Serikali yake ya Mwanahalisi na dada yake Mseto ndio yale aliyoyatumia kama "Hadidu za Rejea" kutengeneza ripoti ya Richmond iliyomuondoa mmbaya wake Eddo kwenye u-PM...na ndani ya Report ile Mwakyembe anayashukuru magazeti haya kwa kuwasaidia kupata habari za report yao kwa % kubwa.

Leo anashabikia uminyaji wa vyombo vya habari vilivyompa huo "umaarufu njaa" aliokuwa nao.If that is the case...Basi hata yeye ile report yake imepoteza "uhalali" wake.Watu wanajiita wasomi lkn wamejaa ukurutu wa unafiki mwanzo mwisho!!Nyakati zitawahukumu....Leo JK na mambo yake yote,lkn wakati unampa nafasi ya kumuona kama "Mwanademokrasia" na "Mwanadiplomasia" mzuri ktk uongozi wake.Huyu akirudi kufundisha akiulizwa nini maana ya "Freedom of Speech",sijui atasema "kuzuia maandamano ya vyama","kufungia magazeti","kuzuia vyama vya siasa kufanya vikao" au nini?Hovyooo kabisaa wasomi aina hii
 
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
Naona upinzani walivyokuwa kama tumbili alie tumbukia kisma kirefu asiwe na mtu wakumuokoa. Dr asante
 
Hapo ndo kajidhalilisha ameonyesha ni jinsi gani anavyomjali Magufuli kuliko watanzania eti hajavunja katiba...mi nasema hawa wanaojiita ma Dk. na ma Prof. wanadhalilisha elimu ya TZ
Halafu cdm siyo wa kuamini leo wamegeuka kupigia debe katiba waliyokuwa wakiiponda
 
Anasema jamaa kama walikwazwa na Raisi wangeenda Mahakamani kudai haki,namuuliza Mwakyembe kwa Mahakama zipi? Mwakyembe anaendelea namnukuu kama walimwengua Dr Slaa na kumweka Lowasa bila kufata Katiba kwa hiyo Chadema hawana Moral Authority ya kumnyooshea kidole yeye Mwakyembe na Mwanasheria Mkuu,'' kwa hiyo ata kama Chadema walivunja katiba yao kwa hiyo wakae kimya wasihoji kuhusu uvunjaji wa katiba na sheria unaoendela hapa nchini''?

Unauliza Mahakama zipi? Jibu ni Mahakama ile ile aliyokimbilia Mbowe kutetea Mali zake zisipigwe Mnada na NHC!
 
Moral Authority inaruhusu kuhoji Utashi wao wa kisiasa na kimaadili.

Ikiwa wewe unagonga Vibinti vidogo hutokuwa na Moral Authority kumkemea binti yako akiwa analiwa na Watu wazima
Hapana haiwi hivyo...bali inakuwa hivi "Wewe ukiwa unagonga vibinti vidogo,hutakuwa na uhalali wa kukemea jamaa yako anayekula vibinti vidogo vya aina ya unavyokula wewe"

Suala la kumlinda binti yako au mwanao wa aina yoyote dhidi ya wabakaji linabaki kuwa jukumu la msingi!!
 
Halafu cdm siyo wa kuamini leo wamegeuka kupigia debe katiba waliyokuwa wakiiponda
Waamini ccm wanaokuweka mjini ila CDM ni watu wanaojitambua na hupigilia msumari unaouma pale serikali ya ccm inapokosea
 
Huyo waziri kweli anayeongea hayo ni msemaji wa Simba au Yanga? Isije ikawa maneno ya huyu mmemhamishia yule...
 
Dr ni mwanasiasa, lazima afanye siasa.

Nikweli kubadilishia gia angani imewapaka matope mashabiki wa cdm
 
Njaa mbaya sana unaweza hata kujidhalilisha kwa ufahamu wako ili upate chakula tu..
 
Back
Top Bottom