Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
Mwakyembe hajui sheria kama anajua basi ni mwoga wa kusema ukweli, kama alivyosema Msigwa
 
Elimu ni zaidi ya kukaa darasani, Tazama PhD mzima anashindwa kusimama kwenye ukweli kwa sababu ya madaraka? Historia itakuja kuwaumbua sana, na sasa mpo mwisho mwisho kwenye siasa zenu, mmeshindwa kujifundisha kwa Sitta? Leo ni mstaafu mnafiki na hana heshima tena
 
Kumbe hawa ndio wanaomwalibia mkuu! Wanashindwa kumweleza wazi mheshimiwa kuwa unavunja katiba!! Badara yake kila kitu wanamsifia..Tatizo wasomi wa Tanzania wanapenda kweli kujipendekeza sijui kwanini?
 
Elimu ni zaidi ya kukaa darasani, Tazama PhD mzima anashindwa kusimama kwenye ukweli kwa sababu ya madaraka? Historia itakuja kuwaumbua sana, na sasa mpo mwisho mwisho kwenye siasa zenu, mmeshindwa kujifundisha kwa Sitta? Leo ni mstaafu mnafiki na hana heshima tena
Mwakyembe amesahau alivyopelekwa India almanusura, kwa ajili ya mtu ambaye hakumtendea haki. Anafanya hayo hayo ya kutouona ukweli. By the way, Sita yuko wapi? Nasikia Afya inaleta mgogoro?????! Do not quote me please
 
huyu mnafiki mwakyembe nilimdharau tokea alivyokuja na ripoti feki ya richmond na kuikana thesis yake ya serikali tatu sababu ya njaa...labda bado ni mgonjwa ule ugonjwa ulikula sana ngozi ya kichwa!!!!!!!!
 
Ivi bado kuna watu wanamsikiliza mwakyembe.
Jimboni kwake ugumu wa maisha umezidi maradufu hakuna anaemtaka kule. Uchaguzi 2015 alipita kwa bao la mkono.

Mwache aendelee kuropoka aone atakavyochinjiwa baharini 2020.
 
Wasomi ndio wanaliangamiza hili taifa
 
ningeshangaa sana kama mwakyembe asingesema haya. huyu tangu alipokataa maandishi yake juu ya muundo wa muungano wetu sina imani naye kamwe. mwakyembe kapoteza sifa zote za kulitetea taifa alizokuwa nazo. kwa mtazamo wangu waziri wa sheria na katiba pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali walipaswa kujiuzulu mara moja kwa kutolitendea haki taifa letu kwa nafasi walizo nazo.
 
Hivi bado kuna watu watu bado wanamwamini Mwakyembe? Pole yao. Mimi nilishampiuza kitambo sana, sio mkweli hata kidogo.
 
Kumbe hawa ndio wanaomwalibia mkuu! Wanashindwa kumweleza wazi mheshimiwa kuwa unavunja katiba!! Badara yake kila kitu wanamsifia..Tatizo wasomi wa Tanzania wanapenda kweli kujipendekeza sijui kwanini?
haa haa kama hajipendi ajaribu kumkosoa JPM kama atabaki ofisini ndani ya masaa 24.huyu analinda ugali wake.
 
Swala ni moral authority au kuvunjwa katiba kitu kizuri ni kwamba sheria hua hai enforce morality, pia angesema hajavunja kufungu gani angekua wa maana yani ni bora asie soma ana nafuu kuliko wasomi wa Tanzania hakuna free thinking....
 
Anasema jamaa kama walikwazwa na Raisi wangeenda Mahakamani kudai haki,namuuliza Mwakyembe kwa Mahakama zipi? Mwakyembe anaendelea namnukuu kama walimwengua Dr Slaa na kumweka Lowasa bila kufata Katiba kwa hiyo Chadema hawana Moral Authority ya kumnyooshea kidole yeye Mwakyembe na Mwanasheria Mkuu,'' kwa hiyo ata kama Chadema walivunja katiba yao kwa hiyo wakae kimya wasihoji kuhusu uvunjaji wa katiba na sheria unaoendelea hapa nchini''?
 
Yaaani hawa wasomi wetu katika nchi hii jamani, Dr anaongea upuuzi waziwazi tena kwa majigambo.
haa haa wasomi wetu uonyesha ujuzi wao kabla hawajaingia kwenye ofisi za umma, wakishaingia ofisini uufyata. mfano ni ndugu Ryoba kabla hajateuliwa TBC alikuwa mwanahabari nguli kwelikweli baada ya kuukwaa ukurugenzi TBC kaufyata. wasomi wetu bado hawajalisaidia taifa letu..
 
Hivi mama Gaudencia Kabaka hajawahi kuongea chochote tangu huu utawala wa mtukufu ushike dola?!
 
Back
Top Bottom