Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Ukitafakari kwa kina utagundua Lowasa ana KIBALI thatswhy katika kuhalalisha kauli au mambo mbalimbali jina lake lazima litajwe iwe kwa opposition au ruling party.Ni kama vile yeye ni ibara fulani ya Katiba
 
siye maamuma wa mambo ya sheria tumeambiwa (na tumeamini) kuwa rais amevunja katiba kwa jinsi anavyoi-treat opposition camp, nk.

sasa hii ya Mwakyembe kusimama bungeni na kutamka bayana kuwa rais hajavunja katiba siyo suala la kulifanyia mzaha. kwa nafasi ya bunge katika katiba yetu tamko la Mwakyembe kupitia chombo hiki is a very serious "declaration" (it's tempting to term it an "allegation" but maybe it is not until legally (un)proven).

so response ya opposition isiishie kujibizana na Mwakyembe kupitia majukwaa bali kwa kupitia process iliyoainishwa kikatiba ili ku-prove kuwa kweli rais ameisigina/hajaisigina katiba. what is the problem with this approach? kuna wanasheria wabobevu kwenye eneo la katiba wengi tu - watumike hawa!
 
Mzee wa mabehewa feki anapoongolea moral authority [emoji33][emoji33]
 
kingkil kullya na kimbendegu someni kilichosemwa na Mh Mwakyembe. Nukuu hizo hapo
 
Ni utumwa mtu mzima aliye kuwa anajitunzia heshima yake kuweka akili mfukoni, huyu Mwakyembe amechoka kimwili na kiakili hata Wananchi wake wamemchoka, rais anavunja katiba ya nchi waziwazi.
 
Mzee wa mabehewa feki anapoongolea moral authority [emoji33][emoji33]

Wewe ni mchovu wa kujibu hoja kwa hoja ila fikra zinazongozwa kwa hisia. Ulichobamdika ni ushahidi tosha huna "moral authority". Kama una ushahidi mpelekeni mahakamani.
 
Moral Authority inaruhusu kuhoji Utashi wao wa kisiasa na kimaadili.

Ikiwa wewe unagonga Vibinti vidogo hutokuwa na Moral Authority kumkemea binti yako akiwa analiwa na Watu wazima
kwa hiyo kama chadema wasipofuata katiba yao CCM ndio wasifuate katiba ya nchi? katiba ya nchi ina uhusiano na katiba ya chadema? CCM wasipofuata katiba yao ok, hakuna atakayewauliza ila sio katiba ya nchi
 
Wewe ni mchovu wa kujibu hoja kwa hoja ila fikra zinazongozwa kwa hisia. Ulichobamdika ni ushahidi tosha huna "moral authority". Kama una ushahidi mpelekeni mahakamani.
Hivi unajua hata maana ya moral authority ?
 
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
"Do not break the law,just bend it"
 
kwa hiyo kama chadema wasipofuata katiba yao CCM ndio wasifuate katiba ya nchi? katiba ya nchi ina uhusiano na katiba ya chadema? CCM wasipofuata katiba yao ok, hakuna atakayewauliza ila sio katiba ya nchi

Kama umeweza kunyofoa kipengele cha Ukomo wa Uongozi ndani ya Chama Utashindwaje kunyofoa hicho kipengele kwny Katiba ya Nchi kama ungetokoea Muujiza ukapewa dola?
 
Huyo waziri kweli anayeongea hayo ni msemaji wa Simba au Yanga? Isije ikawa maneno ya huyu mmemhamishia yule...
Ukweli uko pale pale.
Mwakyembe kawaingiza ndani ya boksi huyo Lema na Msigwa, watu wenye midomo, na wameipata kisawia.

Cha msingi mswaada umepita.
 
Ni utumwa mtu mzima aliye kuwa anajitunzia heshima yake kuweka akili mfukoni, huyu Mwakyembe amechoka kimwili na kiakili hata Wananchi wake wamemchoka, rais anavunja katiba ya nchi waziwazi.

King son (prince): tutakuheshimu ukitunza heshima na kuishi kwa jina hilo la ID yako. Mnaomtuhumu Rais anavunja Katiba hamnukuu ni vifungu vipi anavunja na wala hamtumii vifungu sahihihi vya Katiba kumshitaki ila kuhamasisha uvunjifu wa Katiba hiyo hiyo - soma Sura ya Tatu ya Katiba ya JMT hasa kifungu cha 29(5) na 30 (3).
 
Safi sana Mh mwakyembe kwa maelezo yako ,maana kuna watu wanatokwa na povu Oooo Rais anavunja katiba bila kufafanua kwa kina amevunja katiba ibara ya ngapi tatizo wanaishi maisha ya kukalilishwa na vilaza wa pande zile.
 
Hivi unajua hata maana ya moral authority ?

Wewe umetumia hayo maneno (moral authority) nikiamini unayajua, au ubishi tu! Maadili ya binadamu mstaarabu ni kutawala maneno na matendo yake. Bandiko lako, na wengi wenye mawazo kama wewe, huakisi kuwa na kiwango cha chini cha kutawala maadili yenu.
 
Wao waendelee.kumdanganya mfalme kuwa kavaa nguo wakati yuko uchi. Siku ipo na inakuja, mwendawazimu mmoja atamwambia ukweli mfalme kuwa yuko uchi, na hapo ndipo hao akina Mwakyembe watalipa kwa unafiki wao.
endelea kupiga kelele tu na 2020 Mnabutuliwa tena,hanzeni kutunga kwaya mpya hii ya Udikteta itakua ishachuja
 
Back
Top Bottom