Ni bahati mbaya sana maneno hayo yanatoka kinywani mwa mtu anayetambuliwa kuwa ni msomi mwenye phd, lakini ni bahati mbaya zaidi maneno hayo yanatoka kinywani mwa waziri wa sheria na katiba! Kweli, Mwakyembe anajenga hoja yake kwa kuegemea namna ambayo mtu ambaye yeye Mwakyembe aliamua kumtumia ili kudhofisha UKAWA! Nani alimwambia Mwakyembe kuwa Dk Slaa alikuwa mgombea kupitia UKAWA kabla ya Lowasa hajajiunga UKAWA? Ni nani asiyefahamu kwamba ni Mwakyembe ndiye alitumiwa kumtumia Dk Slaa afanye alichofanya katika kipindi kigumu kabisa cha kuelekea uchaguzi mkuu? Sio Mwakyembe aliyeonekana na Dk Slaa pale Serena wakielekezana namna ya kuichafua UKAWA kuelekea uchaguzi mkuu. Taifa hili liko shimoni limezama, hakuna namna!Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?
Upuuzi kusema chadema wanatoa wapi moral authority, katiba ya nchi ni ya kila mtu na ikivunjwa hata jambazi ana haki ya kuuliza...
Hivi CCM wanaweza kusema kuwa magufuli atawale miaka 20 halafu wakihojiwa waseme mbona Mbowe amekuwa mwenyekiti wa chadema miaka 20?
Kama wakosoaji wengi wangefuata mtindo wako huu wa kutoa hoja na mifano kama yako basi upinzani ungeshika dola miaka ya karibuni, lakini wengi wanaropoka na kufuata makundi tu. Safi sana mkuu. We shall give credit when it's due.Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?
Upuuzi kusema chadema wanatoa wapi moral authority, katiba ya nchi ni ya kila mtu na ikivunjwa hata jambazi ana haki ya kuuliza...
Hivi CCM wanaweza kusema kuwa magufuli atawale miaka 20 halafu wakihojiwa waseme mbona Mbowe amekuwa mwenyekiti wa chadema miaka 20?
Kwa alitegemewa atamke tofauti na hayo?Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.
Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.
Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.
"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.
"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.
Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.
"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.
Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.
"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.
Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.
Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
Hata Kama utaelezwa katiba iliyovunjwa ni ipi hutaelewa kwa kuwa na wewe ni miongoni mwa wale watetea msosi waliojitoa ufahamu kwa Sababu ya msosi.wacha domokaya. sema sheria gani au katiba imevunjwa wapi. mnamfuata lissu mnadhani huyo ni mzima? kwanza mjifunze kufuata katiba yenu ili msiokoteze wagombea urais.
Au alieitia hasara serikali kesi ya samaki wa wachinaKama lilivyoiva la mnunua kivuko Kibovu kipindi akiwa waziri
Hahahaha Mwakyembe ndiyo jicho la Mh Rais katika masuala mazima ya sheria sema tatizo ni kwamba hafanyi kwa ajili ya maslahi yako bali anafanya kwa ajili ya maslahi ya nchi,kuhusu wasomi kuwa makanjanja ni kweli ndiyo maana tunaona professor anakuwa tayari kuongozwa na Form Failure.mwakyembe hana ubavu wowote wa kumsaidia rais wetu kwenye mambo ya katiba na sheria. hatak
ikitokea kesho rais akasema chama kinachopaswa kupokea ruzuku ni ccm tu mwakyembe atasema rais yuko sahihi na hajavunja katiba wala sheria. kiufupi wasomi wetu ni majanga.
Hawa viongozi wa kiteuliwa na rais,hata akiwambia wamnyonye hawatasitaHapo ndo kajidhalilisha ameonyesha ni jinsi gani anavyomjali Magufuli kuliko watanzania eti hajavunja katiba...mi nasema hawa wanaojiita ma Dk. na ma Prof. wanadhalilisha elimu ya TZ
Ondoa hayo macho kwenye ugali...