Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,378
Reaction score
139,283
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
 
Watu wanajiondoa ufahamu kwa sababu ya msosi,katiba inavunjwa,sheria zinakiukwa lakini watu hawaoni kwa sababu ya kutetea msosi,wangekuwa ni wapinzani wamefanya hivyo ungemsikia Mwakyembe angefufua mpaka sheria zilizo kufa Ili kuwadhibiti wapinzani,sababu ya nini,msosiiiii,Yuda alimsaliti Bwana Yesu kwa vipande vya fedha thelathini kwa sababu ya msosi,watanzania tunasalitiwa kwa sababu ya msosi.
 
Kumbe hakuna katiba iliyovunjwa all this time!! basi Sawa
 
Watu wenye nuru ya ufahamu wa kiakili nchi hii wanateseka sana kuona haya yanayofanyika.

Huwezi amini kabisa Prof mzima anakuwa mtu wa kujikomba?

Sielewi ana hofu gani kusaidia hii nchi. Tuna bahati mbaya sana kama Taifa
 
MWAKYEMBE AWASHUKIA LEMA, MSIGWA, CHADEMA
*Asema hawana uadilifu wowote kuisema Serikali;
*Awaita vigeugeu waliomtuhumu Lowassa ufisadi, sasa wawa bubu;
*Asema CHADEMA si Chama bali kundi la uanaharakati

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.
 
Wao waendelee.kumdanganya mfalme kuwa kavaa nguo wakati yuko uchi. Siku ipo na inakuja, mwendawazimu mmoja atamwambia ukweli mfalme kuwa yuko uchi, na hapo ndipo hao akina Mwakyembe watalipa kwa unafiki wao.
 
Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?
Upuuzi kusema chadema wanatoa wapi moral authority, katiba ya nchi ni ya kila mtu na ikivunjwa hata jambazi ana haki ya kuuliza...

Hivi CCM wanaweza kusema kuwa magufuli atawale miaka 20 halafu wakihojiwa waseme mbona Mbowe amekuwa mwenyekiti wa chadema miaka 20?
 
Mimi shutuma zangu kwa Dr harrison ni hizi, huku jimboni kwako miaka yote uliyokuwa madarakani, umetufanyia nini wewe mbunge wetu, hata prof mwandosya na HEKIMA zake ana kila sababu za kusema amefanya kitu jimboni kwake...

2020 KUPATA KURA ZETU EHEEEE....
 
Hapo ndo kajidhalilisha ameonyesha ni jinsi gani anavyomjali Magufuli kuliko watanzania eti hajavunja katiba...mi nasema hawa wanaojiita ma Dk. na ma Prof. wanadhalilisha elimu ya TZ
Mbn unalalamika sana na hata siku moja hajasema kuvunja Katiba kifungu kipi, acha kukalili kijana
 
Na uchumi wetu utaendelea kudorora kwa sababu ya wasomi kama hawa.

Mwambieni Rais ukweli hata kama mtapoteza kitumbua chenu lakini angalau mtaiponya nchi yenu na wananchi. Huu mdororo wa kiuchumi unawaathiri zaidi wananchi wa kawaida (CCM and wasio CCM!). Huku tunapoangukia inaweza kuwa vigumu sana kuinuka!
 
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.

Sishangai kama ameyasema ila analinda ajira yake yawezekana ndio, ndio lilikuwa lengo lake la mwisho kitaaluma.
 
Back
Top Bottom