Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Dr. Mwakyembe: Rais hajavunja sheria wala Katiba

Wanahrakat watangoja sana kwenda Ikulu,kwann wasianze kufuata katiba ndan ya saccos yaoooo
 
Kwanini kusiwe na mjadala wa pamoja wa kuondoa prefix za baadhi ya wasomi wa TZ? Mfano kama jina lake lilikuwa linaanza na prof. au Dr. zitolewe.
 
Mkuu Mwengeso nimekusoma vizuri. Lakini unajua kuwa, "Two wrongs don't make a fight" CDM ikivunja katiba yao haihalalishi walioko madaralani nao wavunje katiba ya nchi. CDM ina wanachama wake na washabiki wake, lakini katiba ya nchi ni ya Watz wote bila kujali chama wala ushabiki. Tuwe wakweli na tuseme kile tunachoamini ni kweli bila kuangalia kuwa kuna mtu jana kadanganya kwa hiyo na sisi tufanye kama yeye.
Danny Jully: kama unasoma bandiko zangu humu, utangundua kwamba mimi ni mwumini mkuu na mfuasi wa sheria hasa sheria mama Katiba ya JMT.

Kwa kuwa hakuna kifungu chochote cha hiyo Katiba kilichovunjwa (kama kipo nitajie) kuninyima uhuru na haki zangu, kama zilivyoainishwa kwenye Sura ya Tatu, na ninatambua hivyo, na ni kweli, sikubali kudanganywa na viongozi wale wanaotaka kunitumia kufanikisha malengo yao kisiasa.

KWANGU JIBU NI HAPANA - wakafilie mbali.
 
Mwakyembe (PhD) kaongea ukweli mtupu!
Aisee kweli siasa ni shida,huyu mwakyembe si ndio alikuwa m/k wa kamati ya kuchunguza ufisadi wa Richmond? Si ndio huyu aliisoma taarifa pale bungeni ya kumshutumu Lowassa? Si ndo huyu sasa ni waziri wa katiba? Katiba ambayo inasema fisadi afikishwe mahakama? Sasa miaka yote hiyo serikali ilikuwa wapi isimfikishe huyo lowasa anaemtaja sasa mahakamini? KITUKO CHA MWAKA HIKI!!!!!!!!
 
Mimi shutuma zangu kwa Dr harrison ni hizi, huku jimboni kwako miaka yote uliyokuwa madarakani, umetufanyia nini wewe mbunge wetu, hata prof mwandosya na HEKIMA zake ana kila sababu za kusema amefanya kitu jimboni kwake...


2020 KUPATA KURA ZETU EHEEEE....
wengi hamkuwachangua so hawana uchungu na nyie
 
Hivi viongozi wa ccm hawawezi kujibu hoja bila kwanza kutamka jina la Lowasa? Mwakyembe angeongelea vipengele vya sheria vilivyompa rais mamlaka yanayobishaniwa na wapinzani. Hii ingetusaidia kuelewa nani anasema ukweli. Lakini suala lake la kufoka bila kutoa vifungu vya sheria hana tofauti na shabiki wa mpira anayebisha kila kitu kwa ushabiki tu. Elimu yake ya sheria inaitumiaje kumtetea rais?
 
Ukweli uko pale pale.
Mwakyembe kawaingiza ndani ya boksi huyo Lema na Msigwa, watu wenye midomo, na wameipata kisawia.

Cha msingi mswaada umepita.
Chekelea sana mswada kupita.........ila kilio chakeeee utalia kilio cha mbwa mdomo juu
 
!
!
leooooo ngojea nimsamehe nisije ongelea tabia ya watu wafupi wanavyopenda kuonekana warefu kwa matendo yao kwa jamii au mabosi wao. Watu wafupi khaaaa
 
Wanasema hivi,BANDU BANDU humaliza gogo.....Kuna siku Mwakyembe atajutia aliyoyaongea
 
Huyu mzee , Mungu aliyemponya kunyonyoka nywele na kucha kama kinda la ndege, anamuona !
 
Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Dr.Harison Mwakyembe(Mb) ameliambia bunge na watanzania kuwa Mh.Rais hajavunja sheria yeyote wala katiba katika utendaji wake.Waziri huo alitoa taarifa hiyo kufuatia madai ya wapinzani kuwa rais anavunja sheria na katiba.
========================================================

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe jumatano jioni aliweka diplomasia pembeni na kuwashukia wabunge wawili wa CHADEMA, Godbless Lema na Peter Msigwa kuwa hawana sifa yoyote ya uadilifu kuinyooshea kidole Serikali bali ugeugeu.

Akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha mjadala wa siku mbili kuhusu muswada wa sheria wa Haki ya Kupata Taarifa, Dk. Mwakyembe alisema Watanzania hawajawasahau Lema na Msigwa kwa kumtuhumu Lowassa kwa ufisadi lakini leo, alidai, wanalamba nyayo zake.

Kauli hiyo kali ya Dk. Mwakyembe ilichochewa na hotuba za wabunge hao wa CHADEMA juzi waliodai kuwa Rais anavunja Katiba na kumnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kumshauri vibaya Rais.

"Rais hajavunja Katiba wala sheria yoyote. Alichofanya ni kuheshimu kiapo chake: kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi ili siasa za shari za uanaharakati zisilisambaratishe Taifa letu.

"Kama CHADEMA walikwazwa na uamuzi wa Rais, basi wangeenda mahakamani au wangedai mazungumzo na Serikali, badala yake wakaamua kuvunja sheria kwa kuitisha maandamano nchi nzima", aliongeza.

Kuhusu tambo za Wabunge wa CHADEMA kuwa kuna siku chama hicho kitatawala nchi, Dk. Mwakyembe alisema ni ndoto kwa kikundi vya uanaharakati kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

"Viongozi wenu wenyewe wamekiri kuwa CHADEMA si chama bali kikundi cha uanaharakati. Mtasubiri sana kuongoza nchi kama fisi wa kwenye hadithi alivyosubiri mkono wa binadamu kudondoka," alisema.

Akionesha wazi kukerwa na shutuma za wabunge wa CHADEMA dhidi ya Serikali kila wakisimama Bungeni, Dk. Mwakyembe alihoji busara ya wabunge wa upinzani kutoka bungeni "wakiongozana kama kumbikumbi" bila kushauriana bali kwa amri ya kiongozi wa upinzani.

"Mlimwengua Dk. Slaa na kumteua Lowassa bila kuheshimu Katiba yenu, leo mnapata wapi moral authority kutunyooshea kidole mimi na mwanasheria mkuu kuhusu Katiba! Mnajua Katiba nyie?" Alihoji.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria aliwaomba wabunge waunge mkono muswada wake wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa aliyoeleza kuwa itaboresha mfumo wa uwajibikaji nchini.

Bunge, likiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Andrew Chenge, liliipitisha sheria hiyo ambayo itatungiwa Kanuni na Waziri wa Katiba na Sheria kwa utekelezaji wake bora.

Kwahiyo chadema wakivunja katiba yao, hicho ndicho kigezo cha serikali kuvunja katiba ya nchi? Mwakyembe has to rethink
 
Mbunge wa kyela ambaye hawezi kuthubutu kuitisha mkutano wa hadhara .
 
Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?
Upuuzi kusema chadema wanatoa wapi moral authority, katiba ya nchi ni ya kila mtu na ikivunjwa hata jambazi ana haki ya kuuliza...

Hivi CCM wanaweza kusema kuwa magufuli atawale miaka 20 halafu wakihojiwa waseme mbona Mbowe amekuwa mwenyekiti wa chadema miaka 20?
Ndiyo maana nimekuwa nikipendekeza kuwa hawa PhD holders wanaofanya mambo kinyume cha matarajio vyuo walivyosoma viwanyang'anye, maana ikiwa Dr. wa PhD ya Sheria anajitoa fahamu asijue kuwa kosa moja halifanyi jingine kuwa haki, basi mwenzake mbabe atauendeleza ubabe wake sana akijiaminisha kuwa anashauriwa na wabobezi kumbe wenzake wanajikomba tu ili wapate ugali wao. Jakaya alikuwa sawa aliposema, "akili ya kuambiwa changanya na ya kwako".
 
Siasa ni kama msumeno hukata pande zote. Aliye madarakani leo kesho atakuwa mtawaliwa, na vivyo hivyo. Siku ipo na inakuja, wanadai Katiba ya nchi inavunjwa, watakuwa madarakani tukashuhudia wakivunja Katiba waziwazi.

Kuna ushahidi dhahiri kwa sasa, viongozi wa upinzani wanavunja Katiba ya Chama chao (rejea mada kuu) na Katiba ya nchi badala ya kwenda mahakamani (kifungu cha 30(3)) wanahamasisha mikutano ya hadhara na maandamano yasiyo na mwisho.

kwa taarifa yako watawala hawaogopi mahakama bali nguvu ya umma huku Africa. Huku kwetu mahakama zinatekeleza sheria kwa utashi wa mtawala. huo ndio ukweli.
 
Sasa nyie CCM nawashangaa sana, nyie mnataka msihojiwe kuvunja katiba ya nchi kisa Chadema wamevunja katiba yao? kwa hiyo tuseme hata chadema wakifanya jambo lolote baya nyie mtalifanya pia kwa kuwa chadema wamelifanya?
Upuuzi kusema chadema wanatoa wapi moral authority, katiba ya nchi ni ya kila mtu na ikivunjwa hata jambazi ana haki ya kuuliza...

Hivi CCM wanaweza kusema kuwa magufuli atawale miaka 20 halafu wakihojiwa waseme mbona Mbowe amekuwa mwenyekiti wa chadema miaka 20?
This is the kind of argument I would like to see everyday here at JF. keep this up. Mwakembe amesahau kuwa bunge linasimamia serikali na siyo CCM.
 
Back
Top Bottom