Nyongeza ni kuwa Lowassa amekuwa mbunge kwa muda mrefu na alikuwa ni Waziri Mkuu; kama angetaka Bunge likae kama kamati maalum tena katika "closed session" angeweza kutoa hoja na kueleza sababu. Lowassa hakutaka kujitetea Bungeni kwa sababu alijua ni mahali pekee ambapo wenzake nao wanaweza kutumia haki hizo hizo. Watu wengi wanajifanya wamesahau alipotoa hoja ya "magazeti ya mitaani" alipojibiwa na Lucas Selelii mle mle Bungeni!
Lowassa hakuonewa na issue ya natural justice haipo. Alijiuzulu pasipo kuhukumiwa baada ya kujipima yeye mwenyewe na kuamua kuwa ni bora kujiuzulu kuliko kujitetea mbele ya Bunge ambako alituhumiwa na ambacho ndiyo chombo pekee ambacho kingeweza kumcondemn!
Nyongeza ni kuwa Lowassa amekuwa mbunge kwa muda mrefu na alikuwa ni Waziri Mkuu; kama angetaka Bunge likae kama kamati maalum tena katika "closed session" angeweza kutoa hoja na kueleza sababu. Lowassa hakutaka kujitetea Bungeni kwa sababu alijua ni mahali pekee ambapo wenzake nao wanaweza kutumia haki hizo hizo. Watu wengi wanajifanya wamesahau alipotoa hoja ya "magazeti ya mitaani" alipojibiwa na Lucas Selelii mle mle Bungeni!
Lowassa hakuonewa na issue ya natural justice haipo. Alijiuzulu pasipo kuhukumiwa baada ya kujipima yeye mwenyewe na kuamua kuwa ni bora kujiuzulu kuliko kujitetea mbele ya Bunge ambako alituhumiwa na ambacho ndiyo chombo pekee ambacho kingeweza kumcondemn!
Kwahiyo mwanakijiji naanza kukuelewa kuwa Lowassa kama PM alikuwa na fursa nyingi za kikanuni hata za kulazimisha ili hoja yake pia isikike. Hivyo basi inawezekana hoja ya Natural Justice inatumika tu kama kisingizio? au pia hii ''natural justice'' ilishapangwa kuja kutumika kama utetezi baada ya kuona haitawezekani kuikabili hoja ya kamati bungeni?
......................................................Thinking Independently....................................
Justice kwa lowassa haikucheleweshwa waka kunyimwa. Tena hakuna akiliyeoewa haki kana Liwassa kulinganishwa na wahusika wengine. KT ilionesha juwa ushahidi wote ulipoint kuwa WM anehusika moja kwa moja. Hi sawa na mtu kusema kuwa alimuona x akiingia na kutoka na vitu kadha wa kadha toka nyumba ya m. Wachunguzi wanakuja na kukusanya ushahidi wote na kutoka hapo wanaketa hoja kwa mwendesha mashtaka ambaye anajukumu la kupima ushahidi ili kujua mashtaka gani ayalete. Yule mwendsha mashtaka anaweza kumwambia mtuhumiwa uzito wa ushahidi dhidi yake na hivyo aamue kukubali hatia fulani au aende mahakamani na kuacha nahakama iamue. Sasa akijipima na kuona ushahidi ni mziti anaweza kukubali hatia na hivyo akienda mahakamani hakuna kesi itakayoendeshwa dhidi yake. Ushahidi wa KT ulionesha kwa kiasi kikubwa kuwa WM amehusika na richmond na ndio sababu ya kuleta hoja bungeni for further steps kwa chombo kingine. Lowassa alitakiwa kuanza hapo kujieleza kwa kutunia kanuni za bunge. Akajiuzulu badala ya kutumia haki yake kujitetea. Siyo mwakyembe wa kulaumiwa. Kiranga hakuna ubaya kumtetea liwassa kama unaamini hakutendewa haki. Hilo halina maaba unakubaliana naye. Kutetea kanuni hata kana inamnufaisha adui yako ni jambo la heshima. Tusitetee wale tunaowapenda tu lakini tukiona adui zetu wanaonewa basi tukae kimya. Ni alama ya kuwa mpenda haki.
Hata polisi kabla ya kupeleka shitaka mahakamani huwa wanamhoji mtuhumiwa kwanza.
Mwakyembe ni mnafiki mkubwa!
Bado ninasubiri kwa hamu atuambie yale aliyo yaficha kwa kulinda heshima ya serikali!
Sina shaka na uchafu wa LOWASSA,ila nina shaka na ripoti ya kamati teule ya mwakyembe!
Nahisi walisiliba matope juu ya mwili mchafu wa LOWASSA!
Asante Mwanakijiji.
Napenda unavyojitahidi kujiweka kati kati lakini wakina Sitta na Mwakyembe wanakuvuta zaidi.
Sio mbaya, ni mtazamo tu.
Hata polisi kabla ya kupeleka shitaka mahakamani huwa wanamhoji mtuhumiwa kwanza.
Hii issue tutake tusitake ilikuwa very political, na mimi ningemuona Mwakyembe smart sana kama angeondoa mianya yote ya shaka kwamba hii issue imepelekwa kisiasa kwa kumhoji Lowassa na wengine wote waliotakiwa kuhojiwa mapema iwezekanavyo ili sio tu kupata picha kamili mapema, bali pia kuonyesha kwamba kila mtu katendewa haki.
Wanasheria wenyewe wana msemo wao "Justice must not only be done, it must seem to be done"
Sasa Mwakyembe hata kama alichofanya ni sawia, kwa maana ya kwamba Lowassa alikuwa corrupt, lakini kwa kumnyima Lowassa nafasi ya kujieleza timely (justice delayed is justice denied), anakuwa hajakamilisha matakwa ya "Justice must not only be done, it must seem to be done"
Yaani kampa Lowassa mwanya wa kusema "Ile kesi ilikuwa ya kisiasa zaidi, ndiyo maana hata Mwakyembe hakutaka kunihoji kwa sababu alijua angenihoji ningempa ukweli issue ingeisha nguvu"
Mwakyembe kachemsha, kama mahakamani Mwakyembe ndiye prosecuter mtu anaweza kusema kuna ground for mistrial hapo. Luckily Lowassa alikuwa hataki fujo chamani lakini kuna siri ambazo Mwakyembe ameficha kingeweza kunuka zaidi.
Kwa hiyo Lowassa alinyimwa haki ya kujitetea na kuwa hakuwa na nafasi ya kuelezea upande wake baada ya kuambiwa ajipime na Bunge limpine kabla ya kumchukulia hatua. Ndicho unachosema?
Kiranga,
Hoja ya ripoti ya richmond haikuwa imekamilika kabla ya kujadiliwa na kupitishwa na bunge, ndio maana utaona kamati ya mwakyembe ilikuja na mapendekezo kama 14 hivi lakini baada ya mjadala na hoja za wabunge mapendekezo yakaongezeka hadi 23, kwahiyo wakati wa mjadala wa ripoti bungeni Lowasa alikuwa na fursa ya ku exercise hiyo natural justice unayosema hakuipata. Je huoni kwamba Lowasa naye ali contribute ku "delay justice" yake mwenyewe kama sio kujinyima kabisa hiyo fursa?
Kama angetumia nafasi aliyokuwa nayo bungeni (na kwa hakika alikuwa na nafasi ya kutosha kufanya hivyo) kuelezea mapungufu ya ripoti ya kamati ya mwakyembe, na kubainisha ukweli wa mambo ulivyo, basi pale pale bungeni ukweli ungebainika, na kama si mkosaji ingedhihirika, na kwahiyo hangelazimika kujiuzulu ili kukinusuru chama chake na mshikaji wake kikwete, Hivyo ripoti ya kamati ya mwakyembe ingetupiliwa mbali na bunge lingefanya maamuzi mengine kabisa.
Kitendo cha yeye kuamua kujiuzulu, na baadae anakwenda kulalamika kwenye vikao vya chama miaka mitatu baadae, na vikao hivyo vya chama havina mamlaka ya kutengua maamuzi ya bunge, si hapo inadhihirisha jinsi alivyoshiriki kikamilifu kujinyima "justice"?
Hapana. Haki ya kujieleza kwa kamati ya Mwakyembe kabla ya ripoti ya Mwakyembe haijakamilishwa.
Hili lingesaidia yafuatayo.
1. Lingempa Mwakyembe picha kamili zaidi ya kupata upande wa Lowassa wa mambo yalivyokwenda na sababu gani mambo yameenda hivyo. Lingesaidia quality ya information katika ripoti ya Mwakyembe.
2. Lingesaidia kuanza na habari kamilifu mapema katika mchakato wote. Mara nyingine, unapokuwa na mashauri kama haya, unatakiwa sio tu kupata input kamili, bali pia kupata input kamili mapema iwezekanavyo. Suppose wabunge wengi wanamuamini Mwakyembe kwamba ni mwanasheria makini, Mwakyembe kaandika ripoti inayo mu implicate Lowassa wrongly bila kumuhoji Lowassa. Bunge linatakiwa kupiga kura ya imani kwa Waziri Mkuu na Lowassa anapewa nafasi ya kujitetea, anajitetea, lakini kwa sababu wabunge walishapewa ripoti ya Mwakyembe iliyokuwa na bias, na wanamuamini Mwakyembe, wamekuwa biased na kumpigia Lowassa kura ya kukosa imani. Hapa haki isingetendeka. Na remedy ilikuwa ndogo tu, kuhakikisha input ya Lowassa inapatikana.
3. Kutomhoji Lowassa timely kabla ya kukamilisha ripoti kuna undermine credibility ya ripoti ya Mwakyembe. Inaonekana kama ilikuwa political zaidi na Mwakyembe aliogopa kumuhoji Lowassa kwa sababu angejitetea vizuri, wakati pengine Lowassa ndiye aliyekuwa set up awe "sacrificial lamb". Hapa ndipo tunakuja katika "justice must not only be done, it must also seem to be done". Leo polisi hata kama inajua fulani kakosa, inabidi maswala yote ya "due process" yakamilishwe, mtuhumiwa ahojiwe, aandike statement etc. Polisi wakimkamata mtu hata statement hajaandika, hajawapa side yake ya story, washampeleka mahakamani, due process haijafuatwa, wengine watauliza huyu mtu mhalifu kweli au polisi wanamjua mhalifu kweli ila wanamtumia huyu kama "sacrificial lamb" tu?
Kuna processes nyingine za kisheria, ukianza vibaya tu, unaharibu process nzima na hata kama mtu mhalifu anaachiwa aende scott free based on a technicality.
Sasa hapa Mwakyembe amempa Lowassa technicality hata kama Lowassa kweli yuko implicated.
Kiranga, huku nikiheshimu critical thinking yako, naomba kutowa maelezo yafuatayo ...Political environment ndani ya bunge ni kubwa zaidi na profesionalism ni tool katika masuala kama hili la Richmond & Dowans. Ndiyo maana alichaguliwa Dr Mwakyembe kuwa Chairperson wa hiyo kamati. Pamoja na ukweli kwamba Mh Prof Majimarefu anaweza kuchaguliwa kuongoza tume kama hiyo, lakini bunge linafahamu, wewe na mimi tunafahamu kuwa Prof Maji hana tools za kufanyia kazi hiyo.
- Tukubali kuwa ndani ya bunge kuna mazingira ya siasa na utaalam
- Wabunge karibu wote hupaswa ku-operate katika mazingira hayo pia
- Hivyo Kamati ya Dr Mwakyembe ilioperate katika misingi hiyo miwili pia, yaani profesionally and politically
- Wabunge wapo ndani ya bunge kwa sababu ya political affiliations zao na profesions baadae
Kwahiyo politics kwakweli ilikuwepo. Lakini pia, Mh EL alikuwa na fursa ya ku-exercise natural justice kama ambavyo imeelezwa kwa undani hapo juu. Ni dhahiri kuwa kama Mh EL angejieleza kwa ufasaha, huku akitumia data sahihi ndani ya bunge, wabunge wasingeweza kuwa influenced na imani juu ya umakini wa Mh Mwakyembe. Ukweli na uongo ungejitenga na Mh EL angepata haki yake. Lakini hakutaka kutumia hiyo fursa kwa sababu ni kweli alihusika na huo ufisadi na sasa anataka kutumia nguvu nyingine kujisafisha.
Hoja ya kutomhoji Mh EL timely... inadai ku-exercise full criminal methods of investigation, exhaustive legal procedures of criminal justice nk. Lakini ukweli ni kuwa hii unaweza kuipata katika mazingira ya mahakama zaidi kwa sababu huko political element ni kidogo zaidi kuliko bungeni..
Hoja ya sacrificial lamb inawezekana, lakini ukianza ku-disect zaidi assumption hiyo nayo unaweza kuishia kui-reject kwa sababu ya kukosa essential dots, circumstantial evidence za kusaidia hitimisho la namna hiyo. Kwa hiyo kinachobaki ni marumbano ya kitaalam juu ya namna ya kufanya uchunguzi, kuandika report, njia za kichunguzi zinazotowa haki zaidi nk. Lakini Mh EL hakuonewa, hakutolewa kama kondoo wa kafara...Na kinachomsumbua sana ni kuwa (1) yeye ameumbuka na wenzake wamepona (2) ndoto ya kwenda magogoni.
Na JK alitakiwa Kuhojiwa.