DR. Mwakyembe na Natural Justice

DR. Mwakyembe na Natural Justice

Lowassa kawapiga watu changa la macho, na aliyemfanikisha ni Mwakyembe kwani angeweza kumminya mpaka watu wapate criminal case, lowassa atupwe lupango, hakufanya hivyo, kamuachia amestaafu analipwa pensheni. Anajitetea kwa techicalities za "natural justice' ambazo zingeweza kutokuwepo kama Mwakyembe angefanya kazi yake kwa umakini.

watu gani wapate criminal case? nyie mnao msapot lowassa? kwa nini hujiulizi takukuru lini imetoa matamko ya uchunguzi wa watu wote wanao tuhumiwa na ufisadi? zaidi ya propaganda za akina mramba na yona na liyumba? epa wako wapi? kagoda wapo wapi, richmond? meremeta etc!! ungekuwa ww au mie tusingefungwa? double standards!, je wezi wengine wapewe muda warudishe pesa?

lowassa ni fisadi papa kiasi kwamba hata system nzima inamuogopa. kwangu mwakyembe TU!! alidhubutu, au unataka tukupe data za mkewe akihaha kwa mwakyembe nyumbani kuokoa hiyo skendo? acheni nyie jamani. LOWASSA HAFAI NI FISADI
 
Oyaah...Mkuu FP...heri ya siku kuu mazee

tatizo ni kukariri kuwa ili due process na due diligence ya natural justice kwenye hii skandali only ingekamilika kwa kumhoji Lowassa......

Facts zote za kum-criminate Lowassa hadi kumfikisha lupango zipo.......CCM imeamua kumkingia kifua kwani ilikuwa ni balaa lao kuelekea uchaguzi........Juzi Lowassa kakiri mwenyewe kikaoni..........

FP........... hivi uliisoma ile ripoti kweli?...........

Kuna mtu kaweka uzi hapa kwamba Lowassa kamzodoa JK live kwenye kikao cha CCM (NEC?) kwamba yeye Lowassa alimpigia simu JK kutaka mkataba uvunjwe, JK akatingisha kichwa kuashiria ni kweli.

Lowassa anajiosha kwamba yeye alimpigia simu JK ili mkataba wa Richmond usikubaliwe na serikali, sasa kama Mwakyembe angemhoji kikamilifu kabla ya kuandika ripoti hizi he say she say zisingekuwepo. Tungejua ukweli.

Lakini kwa sababu Mwakyembe hakufanya due diligence, tuna dilly dally kwenye trivial tricks and troubling technicalities.
 
Kiranga,

..hata mimi nilikuwa disturbed sana na statement ya Dr.Mwakyembe aliposema, "kuna mengine nimeyaacha..."

Hiyoi kauli ndio iliyokuwa silaha kuu ya kumtisha Lowassa na kujikuta akiufyata mkia maana hujui yaliyoachwa yana uzito wa aina gani ?
 
Kuna mtu kaweka uzi hapa kwamba Lowassa kamzodoa JK live kwenye kikao cha CCM (NEC?) kwamba yeye Lowassa alimpigia simu JK kutaka mkataba uvunjwe, JK akatingisha kichwa kuashiria ni kweli.

Lowassa anajiosha kwamba yeye alimpigia simu JK ili mkataba wa Richmond usikubaliwe na serikali, sasa kama Mwakyembe angemhoji kikamilifu kabla ya kuandika ripoti hizi he say she say zisingekuwepo. Tungejua ukweli.

Lakini kwa sababu Mwakyembe hakufanya due diligence, tuna dilly dally kwenye trivial tricks and troubling technicalities.
Mkuu labda hukuelewa.. Lowassa alimpigia simu JK kuufuta Mkataba ambao tayari ulikwisha pita kwa nguvu yake na JK alijua mipango yote hiyo..Hakuna mradi unaokuja nchini JK hajui hata kama sii wake maana yupo ktk kundi lao. Kikwete akamwambia anapata ushauri toka kwa makatibu wake hivyo hili swala hadi kufikia kuuziwa Dowans JK na Lowassa walijua kinafanyika nini..

Sisi sio wajinga kusema JK hahusiki, tunajua anahusika kivipi hili ndilo swala ambalo lingefahamika Bungeni kama kweli tulitaka kujua maana JK alitoa mwanya huo kwa bunge lijadili swala hilo hakulizuia..Swali ni kwa nini tumeshindwa kulizungumzia Bungeni hadi wakauziwa Dowans na JK akasema hawajui Dowans bado tukashindwa kulipeleka bungeni hadi wameuziwa wahuni wa Marekani..

Na wabunge wote iwe ndani ya CCM au nje wanajua fika kwamba kikwazo ni Lowassa na JK kisha ifanya kazi yake kumwondoa ktk Uwaziri mkuu mnaweza pambana naye. Lakini waliojaribu kupambana naye wamekutana na wakati mgumu na wananchi wamekuwa upande wa Lowassa zaidi ya Wapambanaji.. Hata mimi ningekuwa ktk vita hii nisingejiingiza maana unajikuta peke yako na watu wako radhi kukutoa roho.. Na Ukifa hakuna ulichokamilisha unakufa kama kuku maanake walitangulia mbele ya sheria hakuna hata mmoja aliyetunukiwa Ushujaa na wananchi wala kitaifa...

Leo hii Nnauye anachekwa tena na wapenzi na hata viongozi wa vyama vya Upinzani kwa sababu swala la CCM limekuwa kigezo kwao kwamba ukiwa mdogo lazima uheshimu wakubwa wako hata kama wamekosea.. na ndio siasa za Bongo.. Tumemshindwa Lowassa tukubali matokeo lakini sii kusema hana makosa au ati anafaa kuwa rais - He is Mubutu of our time..
 
watu gani wapate criminal case? nyie mnao msapot lowassa? kwa nini hujiulizi takukuru lini imetoa matamko ya uchunguzi wa watu wote wanao tuhumiwa na ufisadi? zaidi ya propaganda za akina mramba na yona na liyumba? epa wako wapi? kagoda wapo wapi, richmond? meremeta etc!! ungekuwa ww au mie tusingefungwa? double standards!, je wezi wengine wapewe muda warudishe pesa?

lowassa ni fisadi papa kiasi kwamba hata system nzima inamuogopa. kwangu mwakyembe TU!! alidhubutu, au unataka tukupe data za mkewe akihaha kwa mwakyembe nyumbani kuokoa hiyo skendo? acheni nyie jamani. LOWASSA HAFAI NI FISADI

Mwingine huyu hajui tofauti ya kum support Lowassa na ku support due process.

The woe of african politics, people steeped in personalities rather than policies.

Wewe unachosema data za mkewe akihaha nyumbani kwa Mwakyembe kuokoa hiyo scandal Lowassa anaweza kukuambia ilikuwa ni attempt yake Lowassa kupata audience na kamati ya Mwakyembe ili na yeye aweze kueleza side yake ya story, kwa nini Mwakyembe hakutaka kumhoji Lowassa.

The fact kwamba TAKUKURU haijafanya kazi vizuri ilitakiwa kumfanya Mwakyembe afanye kazi vizuri zaidi, kwa kumhoji Lowassa na kutupa wananchi nafasi ya kujua utetezi wa Lowassa fully, hata kwa a criminal case. Sasa hivi wananchi hatujui utetezi wa Lowassa fully, tunapata snippets za story anazotaka yeye kutupa, mie nataka aulizwe kila swali ambalo Watanzania wanalo, what's wrong with that? Huko ni kumtetea Lowassa?

Kati yangu mie ninaetaka Lowassa kushurutishwa kuulizwa maswali yote na hata kufunguliwa criminal charges ikibidi na wewe unayeridhika na Lowassa kujiuzulu bila kushurutishwa kujibu maswali, nani anamtetea Lowassa hapa?

Kama Lowassa ni fisadi papa na system nzima inamuogopa, mie ninaetaka ashurutishwe kuulizwa maswali yote na hata kufunguliwa criminal charges na Mwakyembe aliyeogopa kumhoji, nani anaendeleza kumuogopa huku? Mwakyembe kathubutu nini kwa kutomshurutisha Lowassa kujibu maswali na kumpa msemo kwa technicalities za "natural justice" ? Kama tunafikiri huku ndio kuthubutu no wonder CCM inatupeleka resi kila siku Tanzania.

Watu hawako curious, low standards is the order of the day, wanapenda majibu rahisi kwa maswali magumu, hawaoni cover up right in front of their eyes, indeed hawawezi kui recognise cover up kama samaki aliyeyazoea maji kiasi hayajui.

Mediocrity inashangiliwa kwamba ni ushujaa. This explains our poverty.
 
Kuna mtu kaweka uzi hapa kwamba Lowassa kamzodoa JK live kwenye kikao cha CCM (NEC?) kwamba yeye Lowassa alimpigia simu JK kutaka mkataba uvunjwe, JK akatingisha kichwa kuashiria ni kweli.

Lowassa anajiosha kwamba yeye alimpigia simu JK ili mkataba wa Richmond usikubaliwe na serikali, sasa kama Mwakyembe angemhoji kikamilifu kabla ya kuandika ripoti hizi he say she say zisingekuwepo. Tungejua ukweli.

Lakini kwa sababu Mwakyembe hakufanya due diligence, tuna dilly dally kwenye trivial tricks and troubling technicalities.

YES.....ungejua/wananchi wangejua ukweli wote kama mambo yote yangewekwa kwenye ile ripoti "iliyosomwa".........Hiyo habari ya Lowassa kumwambia JK kuwa mkataba uvunjwe haikujulikana juzi tu kwenye kikao..........hiyo habari ilijulikana hata kwenye kamati ya Mwakyembe FYI.........

..........Lowassa kwenye hii skandali alikuw akama Chatu aliyeingia kwenye banda la kuku na kumeza kuku kibao......saa mwenye banda anaingia chatu anaanza kutaka kutema kuku aliokwisha kumeza...........

.......chanzo cha tatizo ni Lowassa mwenyewe kujifanya mfanya maamuzi magumu.....baada ya kuona skandali ni chungu......akaanza kutaka kujiondoa.......akifikiri JK atam-cover.........Lowassa ana bahati na CCM (vikao vya juu) ndio maana anapata masurufu ya ustaafu badala ya kupelekwa mahakamani/lupango kwa matumizi mabaya ya PM's office.........damn CCM.........

Ile ngoma angeachiwa JK mwenyewe........story ilikuwa tofauti........FYI.......wewe unafikiri President Bush aliropoka tu kijinga jinga.......
 
Hivi kamati ya Mwakyembe haijawahi kutoa sababu kwa nini hawakumhoji Lowassa? Nakumbuka kama waliwahi kujibu swali hili....labda ingetupatia mwanga zaidi
 
......Mediocrity inashangiliwa kwamba ni ushujaa. This explains our poverty.

mediocrity ni pamoja na minds kukubali kubambika vitu mahala si pake.........and that further explains our inability to understand different scenarios under different circumstances.......thus it starts with Lowassa.....then inafuatia wale wasioelewa due diligence na due process kuhusu natural justice............specifically kwenye hii skandali..........
 
Hivi kamati ya Mwakyembe haijawahi kutoa sababu kwa nini hawakumhoji Lowassa? Nakumbuka kama waliwahi kujibu swali hili....labda ingetupatia mwanga zaidi

Hata kama walipata habari zote walizohitaji bila kumhoji Lowassa (sijui wangewezaje kufanya hili, being that Lowassa alikuwa PM and heavily implicated) bado kuna swala zima la fairness, kila habari ina pande mbili, kwa nini uchukue upande mmoja na kuandika ripoti bila kusikiliza upande mwingine?

Hata kwa sababu ya kuepuka tu hivi vilio vya "natural justice" kutoka kwa Lowassa, wangemhoji, ili kesho keshokutwa asije kulia "natural justice" ilikosekana.

Kwa kutomhoji Lowassa, hata kama Lowassa ana makosa kweli, Mwakyembe kampa msemo Lowassa. Mtu makini alitakiwa ku cover mianya yote ya malalamishi.

Justice must not only be done, it must seem to be done.
 
mediocrity ni pamoja na minds kukubali kubambika vitu mahala si pake.........and that further explains our inability to understand different scenarios under different circumstances.......thus it starts with Lowassa.....then inafuatia wale wasioelewa due diligence na due process kuhusu natural justice............specifically kwenye hii skandali..........

Ukimpa Lowassa technical disputations, obviously hujafanya kazi yako vizuri.

Kama hujafanya kazi yako vizuri, hujafanya due diligence.

Kama hujafanya due diligence, kazi yako ni mediocre.

Simlple like that, kazi thorough ingem nail Lowassa squarely and accordingly, hili halikufanyika, kaachiwa vi loophole vya kujiuzulu na kuendelea kupata pensheni badala ya kulia lupango.

Ukibisha hili ni kwa sababu tuna tabia ya ku simplify complex situations. Hata mwizi naye anahaki ya kujitetea, sio tu kujitetea, bali kujitetea timely in the process. Ukimnyima haki hiyo mahakama inaweza kutupa kesi, sio kwa sababu huyu mwizi anayejulikana si mwizi, bali ile process yako ya kumkamata ina holes.
 
Hata kama walipata habari zote walizohitaji bila kumhoji Lowassa (sijui wangewezaje kufanya hili, being that Lowassa alikuwa PM and heavily implicated) bado kuna swala zima la fairness, kila habari ina pande mbili, kwa nini uchukue upande mmoja na kuandika ripoti bila kusikiliza upande mwingine?

Hata kwa sababu ya kuepuka tu hivi vilio vya "natural justice" kutoka kwa Lowassa, wangemhoji, ili kesho keshokutwa asije kulia "natural justice" ilikosekana.

Kwa kutomhoji Lowassa, hata kama Lowassa ana makosa kweli, Mwakyembe kampa msemo Lowassa. Mtu makini alitakiwa ku cover mianya yote ya malalamishi.

Justice must not only be done, it must seem to be done.

Mkuu lakini kumbuka kuwa mwisho wa siku ktk ripoti ile Lowassa hakuhukumiwa zaidi ya kuambiwa "apime mwenyewe" uzito wa sakata lile, na yeye akapima na kuamua kuachia ngazi!

Wasiwasi wangu ni wakati tunazungumzia natura justice kutotumika dhidi ya Lowassa hatuitumii dhidi ya tume ya Mwakyembe...
 
Kiranga,

..kwa kweli nikupongeze kwa moyo uliokuwa nao ktk kuitetea hoja yako.

..anayekupinga hapa ama ni mgumu wa kuelewa au ana lake jambo.

..hakuna maelezo ya kutosha kueleza kwanini Tume ya Mwakyembe haikumhoji Edward Lowassa.

..ni bahati tu kwamba Lowassa naye alikurupuka akajiuzulu. kitendo hicho kimeficha a big flaw ikaonekana Mwakyembe na timu yake wamefanya kazi nzuri.

..Lowassa angeweza kukomaa ktk nafasi yake kwa kisingizio kwamba hakuhojiwa, na "amejipima" akaona hana sababu ya kujiuzulu.
 
Mkuu lakini kumbuka kuwa mwisho wa siku ktk ripoti ile Lowassa hakuhukumiwa zaidi ya kuambiwa "apime mwenyewe" uzito wa sakata lile, na yeye akapima na kuamua kuachia ngazi!

Wasiwasi wangu ni wakati tunazungumzia natura justice kutotumika dhidi ya Lowassa hatuitumii dhidi ya tume ya Mwakyembe...

Kwa hiyo kumuachia mtuhumiwa "apime mwenyewe" ndio due diligence?

Watuhumiwa wote wangeambiwa hivi kungekuwa na mtu gerezani?
 
Kiranga,

..nakwambia Lowassa alifura tu na kupelekea kujiuzulu.

..angeweza kuichunia tu hiyo ripoti kama alivyofanya Attorney General Mwanyika na kuendelea ktk nafasi yake.

..kile kitendo cha ripoti ya Tume ya Mwakyembe kusema "waziri mkuu ajipime mwenyewe" kina maana gani? was it a ploy to Lowassa premiership, something that Lowassa himself failed to take advantage of??

..kwanini Mwakyembe asimhoji na baadaye kukandamiza kabisa kwamba Waziri Mkuu ajiuzulu na zaidi ya hapo achukuliwe hatua za kisheria?
 
Ukimpa Lowassa technical disputations, obviously hujafanya kazi yako vizuri....

Ndio maana nilikuambia....Lowassa na wengine....mna-throw vitu sio mahala pake mnadai technical dispute.....thats alone shows mediocrity......in people who believe that to be so

Kama hujafanya kazi yako vizuri, hujafanya due diligence.....

.......kazi ya kamati unaipima na kui-nullify kwa kutomhoji Lowassa!........where is your due diligence......uliisoma ripoti kweli?......your due diligence ingekufanya utambue kuwa Lowassa alipiga changa la macho.........

.....Kama hujafanya due diligence, kazi yako ni mediocre.......

.....na kama hukufanya due diligence as stated above......thinking level/understanding yako ni mediocre...........

........Simlple like that, kazi thorough ingem nail Lowassa squarely and accordingly, hili halikufanyika, kaachiwa vi loophole vya kujiuzulu na kuendelea kupata pensheni badala ya kulia lupango....

hivi ulielewa majukumu ya ile kamati kweli?

.......Ukibisha hili ni kwa sababu tuna tabia ya ku simplify complex situations. Hata mwizi naye anahaki ya kujitetea, sio tu kujitetea, bali kujitetea timely in the process. Ukimnyima haki hiyo mahakama inaweza kutupa kesi, sio kwa sababu huyu mwizi anayejulikana si mwizi, bali ile process yako ya kumkamata ina holes.....

....hakuna ubishi......hapa tunaelimishana...........mnaona complex situation kwa sababu Lowassa kawaingiza kingi i.e. kawapiga changa la macho......nanyi mmeingia kichwa kichwa......kung'ang'ania kitu ambacho haki-apply kwenye environment ya skandali yenyewe......
 
Ogah,

..hebu tueleze basi kwanini unafikiri kulikuwa hakuna umuhimu wa kumhoji Lowassa.

..je, ni key figure gani mwingine ktk scandal ile ambaye hakuhojiwa lakini kamati ikapendekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yake, au kujichukulia["kujipima mwenyewe"]??
 
Mkuu JokaKuu,
Awali ya yote ni muhimu kutambua/ku-acknowledge majukumu yapi kamati ilipewa.
Pili unatakiwa uangalie je kamati ilifanya kazi kulingana na majukumu iliyopewa.
Tatu, ndio ujiulize relevance ya due diligence kwa kamati kwenda beyond majukumu iliyopewa (ndio maana ulisikia kuna mengine yameachwa).....suala ni relevance ya hizo issue na majukumu yaliyokuwepo before the kamati.
Nne na mwisho, jiulize kwanini ripoti ile haikujadiliwa na bunge kama ilivyotakikana.

Ni waste of time and money na ni hatari kutofuata maelekezo ya majukumu uliyopewa.
Hatukuituma kamati kum-criminate Lowassa........Lowassa kajihukumu mwenyewe kwa nadhiri yake mwenyewe.....kwa sababu alijua kosa lake.....
 
Ukiondoa Lowassa, je hao wengine waliopendekezwa na tume wachukuliwe hatua mbona bado wanapeta?
Hivi kweli tunaamini imeshindikana kumchukulia hatua Lowassa sababu hakuhojiwa? Kama wamemfunga Liyumba kwa ajili ya jengo ambalo lipo limesimama imara wangeshindwa kumfunga Lowassa?
Hii serikali imefanya makusudi kabisa kutowachukulia hatua watuhumiwa wa Richmond ili kumpa Lowassa platform ya kuongea kwamba kaonewa! Wanajua wanachofanya hawa jamaa...wanajua mwishowe Mwakyembe na kamati yake ndio watageuzwa bangusilo na mzee wa monduli atapeta kiulaiiini!!
 
Hata kama walipata habari zote walizohitaji bila kumhoji Lowassa (sijui wangewezaje kufanya hili, being that Lowassa alikuwa PM and heavily implicated) bado kuna swala zima la fairness, kila habari ina pande mbili, kwa nini uchukue upande mmoja na kuandika ripoti bila kusikiliza upande mwingine?

Hata kwa sababu ya kuepuka tu hivi vilio vya "natural justice" kutoka kwa Lowassa, wangemhoji, ili kesho keshokutwa asije kulia "natural justice" ilikosekana.

Kwa kutomhoji Lowassa, hata kama Lowassa ana makosa kweli, Mwakyembe kampa msemo Lowassa. Mtu makini alitakiwa ku cover mianya yote ya malalamishi.

Justice must not only be done, it must seem to be done.

jamani jamani mbona hili hulielewi? kamati haina mandate ya kumhoji pm (not only lowassa but JMT PM) sasa hiyo side of story utaipataje kwenye kamati? yeye ni level ya bunge na ndicho akina mwakyembe walifanya na baada ya ripoti kusomwa na amekuwa implicated ilitakiwa aseme his side of the story bungeni lakini yeye akaishia kuonge a use..ge wa kuwa kaonewa sana, tatizo ni uwaziri mkuu!

na hiyo ingeweza kuwafumbua nyie macho akina kiranga kuona pm akidebate publically ambacho kipo kwenye sheria za bunge but hakijawahi kutokea! dual process ilikuwa ikamilike lowassa kujibu hoja pale bungeni na bunge lijadili kwa hiyo kungekuwa na comparison ya point za kamati na lowassa then ambae angeshinda tungemjua!

kazi kwako kamuulize kwa nini aliamua kujiuzuru! na kwa nini kama alionewa anayohaki ya kwenda bungeni leo na kusema alionewa kwa nini anasema na kulalamika kwa watu omba omba (makanisa)
 
Back
Top Bottom