Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Heshima mbele. Lakini kichwa cha thread yako hakiendani na kile kilichoko gazetini. Mwanahalisi halitaji Caspian wala Rostam katika headline ya gazeti isipokuwa ndani tu kuna habari kwamba gari moja linalomilikiwa na Caspian lilihusika katika kubeba watu fulani katika njama hizo.

Hata hivyo kama habari hii ni kweli, basi serikali ya JK ndiyo ya kulaumiwa kukaa kimya tu huku watu wanapanga mauaji. Idea hapa ni kwamba AlShabab wa Somalia ndiyo ilikuwa waonekane wahusika kutokana na hoja iliyojengwa kwamba akina Mwakyembe, Slaa etc wanatumiwa na kanisa kuwakandamiza Waisilamu humu nchini Tanzania.

Lengo kubwa hapa ni kuondoa ushahidi kwamba ni mipango ya watu wa humuhumu ndani. Bila shaka baada ya tukio, magazeti fulani yangelipwa yatangaze kwa bidii kubwa kwamba wahusika ni AlShabab -- kupoteza lengo.

Serikali ya JK ni lazima iamke kutoka usingizini na ichukuwe hatua sasa hivi -- iwakamate wahusika wote.

By the way -- IGP Mwema kisha toa ripoti ya uchunguzi wake kuhusu njama za akina Manji dhidi ya mtoto wa Mengi kumbabikizia madawa ya kulevya?
Hakufanya chochote kwani IGP aliufyata mbele ya akina Manji/Rostam clique.

Kwenye rangi: Kweli, hili limekuwa kimya sana kwani inasemekana hata baadhi ya maafisa vigogo wa polisi walihusika katika njama hiyo chafu. Ajabu ni kwamba eti polisi yenyewe iliunda kamati ya kujichunguza. Na vipi Mzee Mengi -- mbona naye kimya? Au kafumbwa mdomo kwa vitisho vya watu wa CCM?
 
[/COLOR][/SIZE]

Nami nikuulize maana maswali ya huyu Makyembe ni mengi, kwa nini yeye, na habari hii si ilichapishwa jana kwa nini kurudiwa na naona ya jana ilikuwa na info nyingi! Mwaka huu tutasikia mengi lakin hayapunguzi makali ya maisha so, go to hell sitaki habari hizi bora nikae pembeni niwahi Loliondo tu

Mkuu jana ilichapishwa kwenye gazeti gani? Maana huku Loliondo magazeti hakuna.
Ukifika Loliondo tutafutane mkuu, maana foleni ndefu hatujui tutakunywa lini hicho kikombe.
Pia usisahau kuja na kikombe chako cha chuma, maana babu ana vikombe vichache.
 
Siku hizi hatuna wasomi kabisa. yaani huyu daktari mzima anatoa pumba kama layman bwana.
Kwanini wakokodie Al-shabab hapa hamna wauaji kama wataka kukuua, au unataka kupata sympathy za wakristo wenzako?
Mara mganga wa Songea mara yahya Hussein--yaani ujinga mtupu!

Wewe kama wataka kuhamia kwenye chama chenu, hama kwa amani hautakuwa wa kwanza kunguru wee!
 
Heshima mbele. Lakini kichwa cha thread yako hakiendani na kile kilichoko gazetini. Mwanahalisi halitaji Caspian wala Rostam katika headline ya gazeti isipokuwa ndani tu kuna habari kwamba gari moja linalomilikiwa na Caspian lilihusika katika kubeba watu fulani katika njama hizo.

Hata hivyo kama habari hii ni kweli, basi serikali ya JK ndiyo ya kulaumiwa kukaa kimya tu huku watu wanapanga mauaji. Idea hapa ni kwamba AlShabab wa Somalia ndiyo ilikuwa waonekane wahusika kutokana na hoja iliyojengwa kwamba akina Mwakyembe, Slaa etc wanatumiwa na kanisa kuwakandamiza Waisilamu humu nchini Tanzania.

Lengo kubwa hapa ni kuondoa ushahidi kwamba ni mipango ya watu wa humuhumu ndani. Bila shaka baada ya tukio, magazeti fulani yangelipwa yatangaze kwa bidii kubwa kwamba wahusika ni AlShabab -- kupoteza lengo.

Serikali ya JK ni lazima iamke kutoka usingizini na ichukuwe hatua sasa hivi -- iwakamate wahusika wote.

By the way -- IGP Mwema kisha toa ripoti ya uchunguzi wake kuhusu njama za akina Manji dhidi ya mtoto wa Mengi kumbabikizia madawa ya kulevya?
Hakufanya chochote kwani IGP aliufyata mbele ya akina Manji/Rostam clique.

Kwani unavyopost thread yako ni lazima ufuate kichwa cha habari cha gazeti?? Acha kuingilia uhuru wa kutoa maoni weye
 
Hii habari ilikuwa itoke mwanahalisi leo, na imetoka. Walichokifanya Mtanzania ni kuihujumu habari hiyiyo......kama unataka uone haba hiyo kwa uzuri soma Mwanahalisi la leo.......wametaja hadi gari moja iliyotumika kuwa ni ya Caspian kampuni ya Rostam, wametaja majina ya watu woote woliohusika Kuanzia Shehe Yahaya bila kufichaficha! katajwa hadi mtoto wa Lowassa Fred kuwa alishiriki kuwapelekea chakula wauaji hao.....
Mtanzania waliihujumu hiyo habari baada ya kupata tetesi ya walichopanga kuandika Mwanahalisi.......na ndiyo maana mwisho wamesema eti wasomi wamemponda Mwakyembe! sasa wamemponda saangapi wakati habari ndiyo kwanza imetolewa! walijuaje!....Hicho ni kehoro cha Rostam na Lowassa.....habari yenyewe isomeni kwenye mwanahalisi....

Ungetusaidia kwa kuweka link hapo ili tuweze kusoma moja kwa moja..sometimes huwa tunapata usumbufu kupata articles kwenye baadhi ya magazeti.
 
Siku hizi hatuna wasomi kabisa. yaani huyu daktari mzima anatoa pumba kama layman bwana.
Kwanini wakokodie Al-shabab hapa hamna wauaji kama wataka kukuua, au unataka kupata sympathy za wakristo wenzako?
Mara mganga wa Songea mara yahya Hussein--yaani ujinga mtupu!

Wewe kama wataka kuhamia kwenye chama chenu, hama kwa amani hautakuwa wa kwanza kunguru wee!
sijawahi kuona member mpuuzi kama wewe,sijui umekuaje senior member au hata member wa JF, by the way idea zako zina udini,uchama na ushamba ningekutana na ww live ningeku@*(&^ kama kuku.........
 
If this is a true story then it is now obvious: It is ISLAM vs CHRISTIANITY. Ni dhahiri sasa UDINI hatimaye umeingia rasmi Tanzania. Tumekwisha! CCM na makuwadi wake wameuza nchi rasmi. Haiwezekani walengwa wote wa kuuwawa ni wa dini fulani tu na watuhumiwa ni watu wa mipango yote ni watu wa karibu na chama tawala.
Mkuu
Ukisema CCM wanatupeleka pabaya nitakuelewa...lakini Lowasaa na RA ni wa dini tofauti.

Kwa hiyo hilo la Islam vs Christianity ni pamoja na sisi hapa JF...mada nyingi hugeuzwa malumbano ya kidini hapa JF..kwa kutokuwa kwetu makini tunachangia kuingiza huo "udini" rasmi TZ kama ulivyoandika hapo juu. Tukilielewa hili na kuamua kwa makusudi kutokuwa vichocheo vya huo udini basi udini hautapata nguvu.

Mipango hii ina sura ya kimafia zaidi , hizo dini ulizozitaja kama tunataka kuziingiza, kuzihusisha basi tutazitafutia nafasi katika kadhia hii lakini mpango huu si udini, ni umafia na ujambazi.
It has nothing to do with Islam and Christianity.
 
sijawahi kuona member mpuuzi kama wewe,sijui umekuaje senior member au hata member wa JF, by the way idea zako zina udini,uchama na ushamba ningekutana na ww live ningeku@*(&^ kama kuku.........

Yaani kama na wewe unaungana na Mwakyembe kwenye upuuzi wake huu, future ya Tanzania iko hatarini.
Mtu msomi anasema ujinga ambao hata darasa la saba anamshangaa wewe unamshangilia!

Kweli ukipenda chongo utaita makengeza!
 
Siku hizi hatuna wasomi kabisa. yaani huyu daktari mzima anatoa pumba kama layman bwana.
Kwanini wakokodie Al-shabab hapa hamna wauaji kama wataka kukuua, au unataka kupata sympathy za wakristo wenzako?
Mara mganga wa Songea mara yahya Hussein--yaani ujinga mtupu!

Wewe kama wataka kuhamia kwenye chama chenu, hama kwa amani hautakuwa wa kwanza kunguru wee!

Hoja zinajibiwa kwa hoja. Zimetolewa facts za majina ya watu, tarehe za matukio, namba za magari, maeneo mbalimbali. Sasa kupinga hayo you need to bring some evidence. So tunakusubiri uje na concrete evidence kurefute hizo allegations, tunakusamehe na bla bla za hapo juu, at least for now.
 
HABARI YENYEWE NI HII NIMEPATA TOKA KWA MTU WA KARIBU SIJUI KATOA WAPI

Maelezo ya Barua ya Mwakiembe

“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.
“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.
“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.
“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.
“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Aelezea ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).

Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.
“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).
“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.
“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.
“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.
“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).
“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.
“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.
“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”
 
Aleleuyah !!!!
Onyo:
Mkiuua Mmoja wapo hakika Tanzania patachimbika!
Watanzania tumefunguka, kamwe hatutokaa kimya kama zamani!
 
Lowassa anataka kuwa Rais kwa gharama yoyote. Anataka kuwaondoa watu wote waliohusika katika kumtoa madarakani kuhusiana na kashfa ile ya Richmond. Hao ni akina Mwakyembe, Selelii, Sitta na wengineo. Anajua, akiwaua hao, atapeta bila bughuza katika kuwania Urais 2015. Lakini akumbuke kuwa, kwakuwa anatumiwa, naye pia hatakiwi na watu hao. Lowassa ni mbumbumbu kufa. He is just been used!!

Ila ukweli ni kuwa, watamwua Mwakyembe (labda), Slaa na wote walio kwenye list yao...lakini hawataweza kuua watanzania wote, na cha msingi hawataweza kuua ukweli. Na ukweli utawaumbua kama unavyowaumbua sasa.

Nina muamini sana Dr. Mwakwyembe, na sina shaka na taarifa yake (najua ameifanyia utafiti). Kazi iliyobaki ni kwa polisi ni kuchunguza na kuweka wazi. Je, itaweza? kwani hata maafisa wake na vitendea kazi vyake vinatumika; pia wakihusishwa na usalama wa Taifa.

Ole wenu mafisadi!! Mwisho wenu u karibu! nguvu ya umma itawaangukia! Pambaf!!
 
Hizi ni tuhuma nzito, ILA KUAMINI USHIRIKINA HAPO NAMUONDOLEA CREDITS

Hakuna sehemu hata moja ambayo Dr. Mwakyembe ameamini uchawi. Ameeleza tu kilichofanyika katika mlolongo mzima wa mpango wa kumtoa roho. Au ulitaka hili suala la hawa wauaji kwenda kwa mganga asilizumgumzie? Kuzungumzia na kuamini uchawi ni vitu viwili tofauti, I believe.

Tiba
 
Siku hizi hatuna wasomi kabisa. yaani huyu daktari mzima anatoa pumba kama layman bwana.
Kwanini wakokodie Al-shabab hapa hamna wauaji kama wataka kukuua, au unataka kupata sympathy za wakristo wenzako?
Mara mganga wa Songea mara yahya Hussein--yaani ujinga mtupu!

Wewe kama wataka kuhamia kwenye chama chenu, hama kwa amani hautakuwa wa kwanza kunguru wee!

Chama chako kipi mkuu?? maskini wa roho wewe ila mali najua unazo(fisi....adi)
 
Raia mwema nao wamelieleza hili!
SLAA Amesema kamwe hawawezi kumuua,yeye na mungu wake wapo fiti wakati wote.
 
HABARI YENYEWE NI HII NIMEPATA TOKA KWA MTU WA KARIBU SIJUI KATOA WAPI

Maelezo ya Barua ya Mwakiembe

“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.
“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.
“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.
“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.
“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Aelezea ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).

Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.
“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).
“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.
“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.
“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.
“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).
“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.
“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.
“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

Picha ninayoipata ni kwamba maelezo haya yaonyesha mhusika mkuu wa njama hizi ni RA! Arrest him at once!
 
Yaani siamini kama Loigwasa yupo mstari wa mbele kuchangia harambee za kujenga makanisa arusha kumbe ni unafiki tu, he is against christianity? na yeye yatamkuta tena throgh hao hao Shabaab na Taleban muslim brothers wanao sadikiwa kuwatumia.

Iwish hii habari ingekuwa sio ya kweli.

God have mercy on this country.
 
Back
Top Bottom