MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,510
MAJIBU YA MWAKYEMBE HAYA HAPA....Hahahahaha Kozi mwana mandanda kulala na njaa kupenda... Mzee Tupatupa; Mwakyembe hana ubavu wa kujibu mapigo ya Lowassa! Yeye wakati uli alibainika kuwa alikuwa na Kampuni ya kufua Umeme wa upepo Singida ambayo alitaka waingie Mkataba na TANESCO!!! Nani asiejua kuwa Kamati ya Mwakyembe walikwenda Marekani eti kuchunguza Kampuni ya Richmond! Walipofika wakaambiwa kuwa ile ilikuwa Deal la USA kupitia MNCs zake! Jamaa wakapewa Mshiko! Mwisho wa siku wakaja kumtuhumu PM ... Tambua kuwa Lowassa aliwahi kukatiza mkataba wa City Water ambayo nayo ilikuwa ya wakubwa wa USA!!! ... Clinton, Obama wamefika Ubungo kuzindua miradi yao na sasa watu kimyaa!! Wameumbuka hawana la kusema ...
Akihojiwa na mwandishi wa vyombo vya habari vya UHURU waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki ameonekana kufura kutokana na madai yaliyotolewa na Edward Lowassa leo kutokana na sakata la Richmond.
Dr. Mwakyembe amemfananisha Edward Lowassa na 'mshenzi' huku akidai kuwa anateswa na mzimu wa urais!
Hali halisi inaonyesha kuwa sasa CCM kumeibuka vita ya aina yake na inaweza kuisambaratisha vibaya CCM!
Lowassa leo ameonekana kuishambulia vilivyo serikali ya Kikwete kwa kudai kuwa yapo makosa yaliyofanywa katika serikali hiyo!
Hali sasa imefika pabaya!