Na waulizeni waliopo Dodoma wathibitishe, anaendesha Lexus! Huku watu wa Kyela, wanahangaika na maisha yao! Ametoka kuchekiwa afya yake Ujerumani!
Bwassa
Nonsense! Kuna Mbunge anaendesha Bajaj au baiskeli? Na ulitaka akachekiwe Mlingotini wakati viongozi wote wanarushwa nje? By the way, Lowassa karudi jana toka Ujerumani kuchekiwa afya yake. Mbona huongelei maishan ya Wamasai wanaohangaika na maisha? Lets be fair!JM
Re: Hivi Dk. Mwakyembe yuko Bungeni?
Nakubaliana na Engineer. Watu wanalishwa pumba nyingi na hawajui ukweli wa mambo ulivyo. Wananchi wa Kyela wana taabu kubwa katika maendeleo yao wakati Mbunge wao akihangaika na mambo yake binafsi na kutaka Uwaziri, ambao kwa kufanya hivyo anawakandia wenzake Nani alijua kuwa ana hisa nyingi, tena ni za thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni moja na nusu, zaidi ya vijisenti vya chenge, katika mradi wa "umeme wa upepo'?. Hata Bungeni alikataa kusema mpaka ilipobainika hadharani na yeye kukiri kibaguzi kuwa ni "mradi wa watu weusi"? Mwanzo hakusema, baadaye mambo yalipowekwa hadharani akakiri! Alishindwa hata kutangaza "interest" alipokuwa akijadili umeme Bungeni! Hayo mnayozungumza ya ushujaa wake, siyo lugha wanayozungumza Kyela! Engineer mwaga data zaidi kwa kuwa unajua hali halisi! Wanaoishi Marekani na kupata habari za udaku, wajirekebishe!
Bwassa
JM uko kazini ? Kuna mtu kakutonya juu ya habari hii ya Mwakyembe umeamua kumpandia huku huku ?
Tumehabarishwa yuko Arusha kukutana na Mh Edward Lowasa!
Tumehabarishwa yuko Arusha kukutana na Mh Edward Lowasa!
Duh, Mkuu Masanilo ya kweli hayo ?!
=Maxence Melo;https://www.jamiiforums.com/members/maxence-melo.html527841]Nimefanikiwa kuongea na Mwakalinga ambaye yupo Tanzania kwa mapumziko na ameshtuka kusikia haya, kwa kifupi anasema SI KWELI na yeye yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko na familia yake.
Anasema ni maneno ya kutungwa yasiyo na ukweli wowote na anashauri hoja ifungwe kwakuwa kathibitisha kwa kauli yake kuwa hana mpango wa kugombea Kyela.
Kwa sasa yupo Arusha.
Ndugu yangu Bwassa, tuulize tunaoishi na kufanyakazi Kyela ambao tutampigia tena kura Mwakyembe! Huyo anayejiita Engineer ni mmoja wa hao wababaishaji wanaolipwa na Lowassa kwa kumchafua mbunge wetu!
Mambo ya "ubilionea" wa Mwakyembe hayo mnayajua nyie mabilionea wenzake, lakini sisi hapa Kyela tunajua kuwa hakuna Mbunge aliyewahi kufanya mambo mengi makubwa wilayani hapa toka uhuru kama Mwakyembe. Nitataja machache: Amepokea kiti cha ubunge tukiwa na shule 7 za sekondari, sasa tunazo 24; hii lami kidogo katikati ya mji, kaileta Mwakyembe; mradi wa umeme kutoka Ipinda hadi Ntaba, Ipinda hadi Matema Beach, ni miradi ambayo Mwakyembe kaipigania sana na inatekelezwa; katujengea madaraja mapya makubwa mawili (Lusungo na Matema), madogodogo na suspension bridges zaidi ya 10; ameanzisha KDF ambayo imechangia ujenzi wa shule zote Kyela; alimwomba Kikwete ajengewe barabara ya lami kutoka Kikusya hadi Matema (38km), mchakato umeanza na Serikali kuu tayari imetumia zaidi ya sh. milioni 600 kuiboresha; amehamasisha wawekezaji wakubwa na sasa Kyela itakuwa na kiwanda kikubwa cha mpunga Kikusya; barabara mpya tatu kata za Matema na Makwale zimeanzishwa na kujengwa chini ya uongozi wake; ameanzisha vikundi vidogodogo vya ushirika (VICOBA) ambavyo vimeenea sehemu mbalimbali Kyela; na above all ameipa Kyela jina kubwa ambalo halikusikika huko nyuma. Hayo mengine anayoyasema huyo sijui Engineer kweli au Engineer wa maneno, sisi hatuyajui!
Duh amewachenga?nasikia nyie mkakurupuka kwenda Kyela yeye akaensda Arusha.Nimeambiwa mlikuwa mnamtafuta kyela ,kweli Kijana wa london kiboko,amewapiga chenga