Dr. Mwakyembe arejea Bungeni

Huyu jamaa ni mweupe mno kichwani jana nilimwita Engineer wa Udaku, Kuna ndugu yangu anajiita Sikonge na baadhi ya wafuasi wake hapa nusura wanitoe roho. Wanampamba eti Engineer anaishi London na ana kajihotel/Mgahawa huko Kyela...nashukuru na wewe umeliona hilo! Kama ana nia ya Ubunge wa Kyela ameisha shindwa heri atafute kwanza Udiwani Ubunge ni post kubwa sana kwake na mitazamo yake ya zama za mawe...

Masanilo,

Unafahamu kuwa George Mwakalinga ni Mhandisi aka Engineer wa IT na sasa kabobea kwenye mitambo ya simu? Naomba niseme SAMAHANI kwani ulipoandika Engineer, nilikuwa ninauhakika una maanisha Mwakalinga ni engineer wa Majungu. Baadaye nilipokusoma usiku nikajua ulimaanisha huyu jamaa aitwaye Engineer. Hapo nikakupa THANKS kama uliiona.
Ila wewe ndugu yangu neno KIJIHOTELI wala kusema jamaa alikuwa Arusha kwa safari zake binafsi hujaomba msamaha kwa kuandika habari isiyokuwa na ukweli pamoja na kuwa ilishasemwa hivyo.

Labda tu nimsahihishe FMes. Ni kuwa Monduli aliolea Marehemu kaka yake Mwakalinga ambaye aliacha watoto. Kuwa Monduli ni muhimu kwani huko kuna damu yao (watoto wa marehemu kaka yake).

Engineer ni mtu anayesema asilimia 55 kweli na 45 anaweka chumvi. Huyu huwa nakubaliana naye nusunusu kama asilimia zilivyo. Ila si kweli kuwa anaongea majungu tupu au ukweli tupu. Tumzoee.

(Masa ONLY: Walelo nanilya ugali wa MATINI na Matembele... tetetee....)
 
Last edited:
Mkuu, nimefuatilia sana hoja za huyo "Engineer", hazina mantiki, ni udaku tupu wa mtu ambaye hajaenda shule sawasawa. Huyu Dk. Mwakyembe alishajijengea jina na historia hata wanaomchukia wakiamua kumchafua usiku na mchana. Wiki iliyopita nilishuhudia Dk. Mwakyembe akipita Kariakoo kwa mguu: karibu kila mtu alitaka amshike mkono, amsalimie na wengine wasikie sauti yake tu. Sasa mwambie "Engineer" amlete huyo Rostam au Lowassa (paymasters wake) nao wapite Kariakoo kwa mguu, utajua wananchi wanavyojua kupambanua kati ya kiongozi na fisadi. Watazomewa na hata kupigwa mawe!

Huko Kyela kumetokea mauaji ambayo, ukisoma sana taarifa za magazeti yamesababishwa na Mkuu wa Mkoa ambaye kikwete alimweka pale kummaliza Mwakyembe na Mwandosya kisiasa. Kashindwa! Mwakyembe akienda Igunga kugombea ubunge, nakwapia atamshinda huyo mtu wa Iran anayetuchanganya Watz kama watoto! Mimi nimemtambua Mwakyembe kuwa kiongozi na jabali lenye akili, alipowatingisha wazungu NBC kupigania maslahi yetu wafanyakazi mpaka akajiuzulu. Hawa akina "Engineer" are just nincompoops. Akiandika upuuzi JF anakimbia kwa mawakala wa Rostam na Lowassa (ambao wako wengi Kyela) kwenda kulipwa!

Masa,
Halafu huyo hapo juu umempa asante. Sijui kwa lipi. Ni hilo la kusema kuwa "Mkuu wa Mkoa ambaye kikwete alimweka pale kummaliza Mwakyembe na Mwandosya kisiasa." Hii si ndiyo staili ya Engineer?

Kamau,

Unaweza kuthibitisha kuwa mauwaji yamesababishwa na Mkuu wa Mkoa? Je Mkuu wa mkoa aliwekwa pale ili kummaliza Dr na Prof? Una Ushahidi huo au majungu tu kama ya Engineer (according to ndugu yangu Masa).
Je Mwakipesile aliwekwa ukuu wa Mkoa wa Mbeya lini? Siku hizo nani alikuwa PM wa Tanzania? Mbona huyo PM aling'olewa na Mwakyembe? Na wengine wanasema kwa baraka za Muungwana? Kati yenu mnaosema Mwakyembe kawekwa na Kikwete ili kummaliza Lowassa na anayesema Mwakipesile kawekwa na Muungwana ili kuwamaliza Dr na Prof., MMOJA WENU ANADANGANYA.

NA hii ya kuwatingisha Wazungu, je WALITINGISHIKA? Au ilikuwa makelele ya CHURA, watu wakaingia na kula vitu vyao na wakajikata au wakaamua na kujenga? Hii nayo imekaa kidakudaku (Nifahamisheni sina uhakika).
 
Wazee wote lazima wang'oke mimi nitagombea igunga

MkamaP,

Sasa kijiji cha Igunga unataka uwe nani lakini? teteteteee

Mbunge amchongea DC bungeni
Na Sharon Sauwa
22nd July 2009

Nkayamba,.jpg

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Sijapata Nkayamba.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Sijapata Nkayamba, amemtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongella, kwa kutoa kibali kwa wamiliki wa maboti yanayotoa huduma katika kijiji cha Igunga ili yasafiri muda uliopigwa marufuku na kamati ya ulinzi na usalama.

Habari kutoka : :: IPPMEDIA
 
Masanilo,

Unafahamu kuwa George Mwakalinga ni Mhandisi aka Engineer wa IT na sasa kabobea kwenye mitambo ya simu? Naomba niseme SAMAHANI kwani ulipoandika Engineer, nilikuwa ninauhakika una maanisha Mwakalinga ni engineer wa Majungu. Baadaye nilipokusoma usiku nikajua ulimaanisha huyu jamaa aitwaye Engineer. Hapo nikakupa THANKS kama uliiona.
Sikonge

JF inachanganya sana! mimi namwita yule Engineer wa anayeweka post zake mdaku, mbeya na mweupe upstairs nadhani umenisoma, Kama Mwakalinga George naye ni Engineer basi tumechanganyana sana, Simjui George na nisingaliweza mwita mzee wa udaku na majungu kama yule Engineer mwingine ambaye hata wewe unamjua.... sasa hawa wapiga debe kama Engineer (si Mwakalinga) wataharibia wagombea maana wengine wanaharibu sana kwa mapenzi walionayo kwa wagombea wao.

Engineer ni mtu anayesema asilimia 55 kweli na 45 anaweka chumvi. Huyu huwa nakubaliana naye nusunusu kama asilimia zilivyo. Ila si kweli kuwa anaongea majungu tupu au ukweli tupu. Tumzoee.
Kila Laheri George
 
Sikonge

JF inachanganya sana! mimi namwita yule Engineer wa anayeweka post zake mdaku, mbeya na mweupe upstairs nadhani umenisoma, Kama Mwakalinga George naye ni Engineer basi tumechanganyana sana, Simjui George na nisingaliweza mwita mzee wa udaku na majungu kama yule Engineer mwingine ambaye hata wewe unamjua.... sasa hawa wapiga debe kama Engineer (si Mwakalinga) wataharibia wagombea maana wengine wanaharibu sana kwa mapenzi walionayo kwa wagombea wao.

Masa,

Kama ulivyosikia ni kuwa George hajatangaza kugombea. Sasa Engineer ambaye yuko Mbeya, sidhani kama atakuwa katumwa na George anayeishi UK. Huyu atakuwa alikosana na Mwakyembe na hivyo, kila akipata mwanya basi huanza kuandika kwa hasira na kuweka chumvi. Nafikiri huyu atakuwa upande wa Mpinzani yeyote wa Mkwanyembe hata kama utakuwa wewe au mimi. Sintashangaa Mkwanyembe akigombea Igunga, basi atakuwa upande wa Rostam. Kichukia roho SI DAWA??? Mhh sijui ipo hiyo?

Hilo la Udaku hata mie lilinishangaza. Anyway tuko pamoja kwenye lile joka letu ambalo Braza Karumanzila aka Braza K anasema "Njia chuma na renyewe Chuma...."
 
-umesikika baba!hata hivyo naomba umsamehe MASA BURE!unajua hili jukwaa la siasa hana uzoefu nalo.yeye ni mutu ya kule-kwingine kwa wale jamaa wa ule mlengo mwingine!wamejipa jina la mtandao wa simu za mkononi!alipitiwa tu,msamehe
Kha! Masanilo bro! usiingilie vitu ambavyo huna ujuzi navyo ona sasa unavyo umbuliwa hapa.Bwa ha ha ha
 
MkamaP,

Sasa kijiji cha Igunga unataka uwe nani lakini? teteteteee

Mbunge amchongea DC bungeni
Na Sharon Sauwa
22nd July 2009

Nkayamba,.jpg

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Sijapata Nkayamba.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Sijapata Nkayamba, amemtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongella, kwa kutoa kibali kwa wamiliki wa maboti yanayotoa huduma katika kijiji cha Igunga ili yasafiri muda uliopigwa marufuku na kamati ya ulinzi na usalama.

Habari kutoka : :: IPPMEDIA

Nautaka ubunge wa igunga, nipambana na Aziz Rostam
 
Huo ni ukabila sasa,kwani hata dereva naye lazima awe Mnyakyusa.Huo ni Ukaburu
 
Kila Laheri George

- Mkulu Masa, saaafi sana George hawezi kuwa ndiye Engineer no way, tufike mahali tujadili hoja muhimu kwa wananchi wa Kyela, waliyokwisha fanyiwa na ambayo hawajafanyiwa, either na viongozi wao hasa mbunge au na serikali yetu, badala ya kuugeuza mjadala kuwa Yanga na Simba.

- Kugombea ubunge sio vita wala ugomvi, wananchi wa Kyela should be proud kwa kuweza ku-create vichwa kama vya DK na George, regardless of what holds their political future ni vyema hawa wawili wakashirikiana kwa karibu sana kuwasaidia wananchi wa Kyela, badala ya kuvurugana au kuruhusu kuvurugwa na wapambe uchwara kama tunavyowaona humu,

- Hii mikwara ya kujaribu kumtishia tishia George kwa visingizio vya kwamba ati anatayarishwa na mafisadi, ni nonsense at best na sitaki kuamini kwamba zina baraka za DK, ninasema kama kuna mwananchi yoyote mwenye ushahidi wa kumuhusisha George na mafisadi, auweke hapa wazi wote tuuone, otherwise tusiharibu majina ya vijana makini kwa sababu ya tamaa za fisi, DK azungumzie aliyoyafanya Kyela toka awe mbunge wao, halafu alinganishe na majimbo mengine ili tuweze kuona ukweli wa kazi yake huko jimboni, JF hatujawahi kumhukumu kiongozi yoyote wa taifa bila kumpa haki ya kujitetea au kutetewa na wapambe wake, wengi hatuzijui siasa za Kyela lakini hatuna tatizo kujua tunapotaka kupotoshwa,

- Leo asubuhi sana nimeongea na George akiwa mbugani ambako alipeleka familia yake kuangalia wanyama katika mbuga zetu kabla hajaondoka jioni kuendelea na utalii sehemu zingine za Tanzania, na nimemhakikishia kwamba everything is under control maana jana alipata simu nyingi sana kutokana na majungu mengi yasiyo na msingi wala kichwa yaliyowekwa hapa, eti kiongozi wa kutaka kuwasiadia wananchi anaenda kukutana nao hotelini what a nonesense, as if hatujui kwamba mara ya mwisho kiongozi wetu alipoenda hotelini London aliishia kuyatosa madini yetu sasa leo ni kiongozi gani mwenye akili timamu atarudia kufanya business za wananchi hotelini tena?

- JF tutaendelea kusimamia mijadala yenye facts na dataz, lakini sio majungu na udaku, na hata siku moja hatutaruhusu majina safi kuchafuliwa mambo ya kujuana juana ndiyo yamelifikisha taifa letu lilipo sasa ndio maana ninasema kama kweli George ataamua kugombea basi wananchi tutafadikika sana na political debate ya hawa vichwa wawili I mean itakuwa ni a political debate of the century,

Mungu awabariki wananchi wa Kyela na aibariki Tanzania na JF pia, where we dare!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
Asante FMES, nilichukuliwa na wimbi kuaminishwa na hisia Engineer wa JF ndiye Mwakalinga, I am sorry for any inconviences might have been caused! Sina cha kuongezea zaidi kama ulivyoainisha hapo juu wananchi wa Kyela wachangue aliyebora...Eng Mwakalinga ama Dr Mwakyembe, na kama akitokea mwingine apewe kama atakuwa bora kuliko wote kwa maslahi ya taifa. Huu ni wito wangu kwa watanzania nzima hakuna mwenye hati miliki na Jimbo wala uongozi wowote! Sitegemei watu kama Mzindakaya, Makweta kuendelea kuongoza kwa miongo mingi.

Sikonge, nakubaliana na wewe Engineer yule mwingine anachuki ya kufa mtu na Mwakyembe ndo maana post zake nyingi anajaza chumvi na hamira ili mradi amchafue Dr Mwakye amabaye ameonyesha tayari ana nia njema na taifa ingawa ana mapungufu yake pia.

Peace and Love

Mzee Masa
 
Kha! Masanilo bro! usiingilie vitu ambavyo huna ujuzi navyo ona sasa unavyo umbuliwa hapa.Bwa ha ha ha

Najua Ukikuwa utaacha ni utoto tu unakusumbua! Ukiwa kijiweni na watoto wenzio unasema leo nimemjibu Bro Masa.....kaaa kimya tunakata issue zenye maslahi ya taifa sisi hapa ebooooooooooo CarthbertoLo
 
Kha! Masanilo bro! usiingilie vitu ambavyo huna ujuzi navyo ona sasa unavyo umbuliwa hapa.Bwa ha ha ha
Haya ya Dr. Mwakyembe, anaandaa mandamano Dodoma kupinaga na kushinikiza serikali ichungeze ajali aliyopata. Jamaa watu hawana kazi za kufanya, maandamano ndio maendeleo? Mungu ndiye mwenye kujua yote, ajali ni kwa watu wengine tu? na sio Mwakyembe? Wabunge wangapi wamewahi kupata ajali na hawakwenda Dodoma kuandamanan?
Huyu jamaa ni masanii kweli na hafai.
KGwamaka
 
Lakini yote sita, saba ni kwamba huyo Mwakalinga hasa ni nani kumtisha Mwekyembe mwenye sifa ambazo tunazijua?Maana naona hizi ni njama tu za mafisadi ambazo sasa ni too much.
 
Yaani leo mimi engineer nimekuwa ndiye George. Basi kumbe nimekuwa babu kubwa.

Sishangazwi na propaganda zenu maana hata hamjui nini kinatokea huku. Sisi tunamsubiri huyo George aje achangamshe Kyela.
 
Sishangazwi na propaganda zenu maana hata hamjui nini kinatokea huku

Engineer, Kuna wengine wanashangazwa pia na propaganda zako, hata kama hatujui basi usiongezee hamira na chumvi!
 
Lakini yote sita, saba ni kwamba huyo Mwakalinga hasa ni nani kumtisha Mwekyembe mwenye sifa ambazo tunazijua?Maana naona hizi ni njama tu za mafisadi ambazo sasa ni too much.

- Ndio maana tunashangaa sana a politician wa calliber ya DK, kuanza kuliliwa na wapambe hapa kuhusu kijana mdogo aliyeko likizo tu, je akiamua kugombea itakuwaje?

- Kwa nini usizimwage sifa za DK, jimboni maana sio siri kwamba kwenye taifa tunazijua, tatizo ni jimbo ndilo linaamua nani awe mbunge wake sio taifa, sasa weka sifa hizo za jimboni mkuu tuzichambue.

- Yaani unasema kwamba ni njama za mafisadi kina Rostam ambaye at one time DK, alitaka kufungua naye kampuni ya umeme? au?

Kuna watu wanajifanya hawagusiki na wala hawapingiki, mtu wao akiguswa anang'aka. Sasa Mwakyembe kama ni mahiri kwa nini tumbo limcheze kwa Mwakalinga kujitokeza? Asubiri wapambane hapo mwakani, kama yeye ame-perform Kyela atapita. Ni woga kufikiri kila mtu anayejitokeza kuwapinga hao waliopachikwa ushujaa kwamba ametumwa na akina Rostam. Wakati mwingine wanampa sifa za bure huyu RA.
 
Rostam
wanampamba tu wala hana jeuri yoyote,kwa miono yangu yeye katumiwa kupitisha hizo feza zakifisadi ma king maker wakubwa ni hawa viongozi wa juu kabisa.

Na huyu jamaa hana ushawishi wowote kumnunuwa mtu, ila imekuwa tabia mbofu sasa kwamba ukitofautiana na mawazo yao lazima utakuwa umenunuliwa na RA.

Inabidi ni kili kufanya kosa kwa ZITTO sikukutendea haki nilipokushambulia kuhusu DOWANS.Kwa namna moja ama nyingine nilifuata upepo fulani.
Japo msimamo wangu hadi dakika hii unapingana na wa kwako kuhusu Dowans lakini pia sichelei kusema msimamo wako ulikuwa huru.
 
Engineer, Kuna wengine wanashangazwa pia na propaganda zako, hata kama hatujui basi usiongezee hamira na chumvi!

Masanilo,

Wewe huna data bora ukae kimya. Umeniacha hoi kwamba kwasababu mwakalinga ni engineer basi ndiye mimi engineer.

Maandamano yaliyokuwa yanapangwa hayapo tena baada ya kuonekana vijana wa kuandamana hawapo tena, kuna msemo umetokea ghafla hapa kwamba tunataka maendeleo zaidi na si maandamano zaidi.

Leo niliambiwa Mwakalinga kaingia hapa mjini lakini wapambe wake wa karibu wameniambia sio kweli. Kuna uvumi kwamba Mwakalinga alikuwa anataka kuingia Kyela siku ya maandamano ya Mwakyembe. Sasa maandamano hakuna huenda na yeye akabadili ratiba yake.

Kulingana na wasifu wa mwakalinga niliouona leo, inaelekea sio kijana kama tunavyodai hapa. Ana miaka zaidi kidogo ya 40, ana degree kwenye computer science, ana M.Sc ya computer science, ana MBA ya technology management na ana postgraduate diploma ya business administration. Pia ana professional certificates kibao kwenye telecoms hata zingine sijui maana yake.

Pia wasifu wake unaonyesha kwamba kabobea kwenye telecom na kafanya kazi Lucent Technologies miaka zaidi ya kumi.

Nitaendelea kuwaletea mengine nikipata. nafanya mpango nionane naye na kujua anasimamia nini.

Pia kuna balaa lingine lilitokea jana, vile vyakula vya misaada vilivyotolewa kwa ajili ya mafuriko Kyela jana vilimwagwa na wafuga nguruwe kujizolea. Inasemekana hiyo misaada ilifichwa na hiyo NGO ya jamaa zake Mwakyembe ambao alikuwa anawatumia kugawa misaada. Badala yake walikuwa wanatumia chakula hicho kuwalisha wafanyakazi wanaofanya kwenye kampuni yao binafsi ya ujenzi. Matokeo yake wameshindwa kumaliza mpaka unga umeoza huku wananchi wengi walilalamika wakati ule kwamba hawakupata chakula cha misaada. Mwulizeni Dr wenu vipi alikuwa busy na Richmond mpaka wajanja wana abuse misaada?
 
Lakini yote sita, saba ni kwamba huyo Mwakalinga hasa ni nani kumtisha Mwekyembe mwenye sifa ambazo tunazijua?Maana naona hizi ni njama tu za mafisadi ambazo sasa ni too much.

Kaka njoo Kyela uje uone kwanini Mwakyembe tumbo moto. Hata mimi nashangaa kweli mtu mwenye jina kama la Mwakyembe kwanini ifike mahali awe na wasiwasi kiasi hiki?

Huko nyuma ilikuwa inasemekana Mwanjala anataka kugombea, dr akawa anacheka tu. Hata waliposema mwakipesile anagombea yeye akawa anasema mwache aje nimtupe chini mara ya pili. Lilipotokea jina la Mwakalinga ghafla dr. tumbo moto, anaanza kuandika habari kupitia magazeti ya Mengi kumchafua huyu kijana. Ukweli ni kwamba Dr. anamfahamu vizuri Mwakalinga maana walimwunga mkono mwaka 2005, hivyo kama ameogopa basi jua kuna mambo anayajua ambayo nyie hamyajui.
 
Back
Top Bottom