Dr Mpango akiri uchumi wa nchi kuporomoka

Dr Mpango akiri uchumi wa nchi kuporomoka

Hii ni baada ya kuliambia bunge kwamba hali ni tete hasa baada ya mapato kwenye sekta ya madini kupungua kutokana na baadhi ya makampuni kusitisha uchimbaji na kukosekana kwa mapato kutoka kwa sekta isiyo rasmi ( machinga ) kunakotokana na kukosekana kwa kumbukumbu za mapato kulikosababishwa na machinga kutokutunza kumbukumbu na kutokuwa na sehemu maalum za kufanyia biashara.

Dr Mpango amedai kwamba kushindwa kuongezwa mishahara ya wafanyakazi , na hivyo kupunguza mzunguko wa pesa ni sababu nyingine ya kuanguka kwa uchumi wa nchi .

Mytake , itafika wakati wote tutaongea lugha moja .
Eti anasingizia machinga...huku lile dikteta la kihutu liko like " we are in the laiti tlaki"
 
Kuna kitu kinaitwa ''AN ENTREPRENEUR AND HIS ENVIRONMENT'' hakija kaa sawa Kwenye uchumi wa Tanzania kwenye Kitabu changu ninacho kiandika nimejaribu kuelezea vizuri
Kwa hiyo sasa mkuu huu uzi ufungwe tusubiri kitabu chako ama? Wabongo bana😀
 
Hii ni baada ya kuliambia bunge kwamba hali ni tete hasa baada ya mapato kwenye sekta ya madini kupungua kutokana na baadhi ya makampuni kusitisha uchimbaji na kukosekana kwa mapato kutoka kwa sekta isiyo rasmi ( machinga ) kunakotokana na kukosekana kwa kumbukumbu za mapato kulikosababishwa na machinga kutokutunza kumbukumbu na kutokuwa na sehemu maalum za kufanyia biashara.

Dr Mpango amedai kwamba kushindwa kuongezwa mishahara ya wafanyakazi , na hivyo kupunguza mzunguko wa pesa ni sababu nyingine ya kuanguka kwa uchumi wa nchi .

Mytake , itafika wakati wote tutaongea lugha moja .

Jingalao et al njooni mpongeze juhudi za "Rais wetu mpendwa Dr John Joseph Pombe Magufuli".
 
Dr Mpango ni muongo,anamgombanisha Rais na wananchi atumbuliwe haraka sana,hali ya uchumi ni nzuri mno,Rais kafanya kazi nzuri sana kuinua uchumi.
By jingalao,Barbarosa,magonjwa mtambuka,muda wote,Rutashoborwa,stroke and other Lumumba crazies.
(Crazy? )Zombies would have suited em better.
 
Kinachotakiwa si kurudi kwenye figisu bali ni kuondoa urasimu katika kufanya biashara na kudeal na conflicts za wawekezaji kwa maarifa. Wakuu wa mikoa na wa wilaya wakae mbali na wawekezaji, maana baadhi wametoa picha mbaya. Mzee aanze kuamini zaidi mawaziri wake. Kabla ya kubomoa chochote kuwe na mbadala. Miradi ya umeme na Reli iendelee kuwa kipaumbele , ila kuamia Dodoma na manunuzi ya ndege yasitishwe.
 
Dokta Mpango atumbuliwe haraka sana hawezi kupingana na takwimu za dokta Abbas,Prof.Mukandara,Prof. Qorro,Prof.Mkumbo na wasomi wa hali ya juu duniani waliosema juzi pale UDSM kuwa uchumi unakua kwa kasi kubwa muno na tunatakiwa tutembee vifua mbere.
Ina maana yeye kasoma chuo gani,cha kata?
Usiache kumtag na CAG PolePole mkuu!
 
Back
Top Bottom