Dr. Mengi kujenga kiwanda cha kuunda magari nchini

Dr. Mengi kujenga kiwanda cha kuunda magari nchini

so sad aisee, nguvu zimemwishia mzee wetu
Kabisa mpaka anatia huruma, why hataki kupumzika? Haamini mtu au hakuna mtu anataka kusimamia shughuli zake? Na baada ya msiba wa aliekuwa mkewe ndio kzidi kwisha.
 
Kabisa mpaka anatia huruma, why hataki kupumzika? Haamini mtu au hakuna mtu anataka kusimamia shughuli zake? Na baada ya msiba wa aliekuwa mkewe ndio kzidi kwisha.
Huyu msanii..ila ni vizuri "wenyewe" washamfahamu kuwa si mkweli. Nadhani angeanza lipa mkopo yake michafu anayodaiwa na mabenki yetu kabla ya kurukia huku...Sidhani kama awamu hii udalali una nafasi...
 
Sidhani kama kuna mfanyabiashara mkubwa mwenye imani kubwa na Tanzania ya viwanda kama ndugu Reginald Mengi.
Mengi anatarajia kuanza kutengeneza/kuassemble magari hapa nchini.

Wakati wapinzani wakidai serikali inaua biashara,kwa kipindi cha miaka 3 ya JPM,mfanyabiashara Mengi amewekeza zaidi ya bil 100 kwenye ujenzi kiwanda cha madawa, anatarajia kufungua kiwanda cha simu na sasa anaingia kwenye Magari.

Swali la msingi tujiulize kati ya Mengi aliye kwenye game la biashara kwa zaidi ya miaka 40 na mchungaji Msigwa aliekuwa mchungaji kwa zaidi ya miaka 10 ni nani hasa anaweza kuona uchumi unayumba kwa usahihi?.

Tanzania ya viwanda.
View attachment 940512View attachment 940513
Ungejiuliza kwanza kwa miaka 40 ambayo mengi yupo kwenye game ya biashara mtaji alitoa wapi. Ingekuwa nchi nyingine wala mengi asingekuwepo ungesikia tu kuwa kuna mfanyabiashara moja alifungwa maisha kwa kuibia serikali. Kabla ya kuandika fanya tafiti kwanza. Usikurupuke tu kwaio mengi kufanya biashara ndio uchumi imekua duu maskini Tanzania nakulilia nchi yangu. ELIMU! ELIMU! ELIMU!
 
Tangu aseme atajenga Hospitali ya magonjwa ya moyo , miaka 20 iliyopita uliona hata mchanga au kokoto ?

Mzee Mengi badala ya kutuona mazuzu ni vema basi ukakamilisha miradi uliyotueleza mwanzo kabla ya kukurupukia mengine .
Mkuu mbona Foundation iliwekwa. Pia sio miaka 20 kwa sababu Mtie alifariki 2009 mwanzoni
 
Huyu mzee pamoja na mwenzake Mosha waliunda kampuni ya NIKO wakatapeli maelfu ya watanzania mpaka leo kampuni haijulikani iliko,hawa wachina wasipokaa sawa atawapiga
 
Utapata tabu sana awamu hii,Dada mange kimavi anasemaje kuhusu kuyumba kwa uchumi ambayo ndo ajenga kuu ya wakaazi wa kijiji cha pingapinga kata ya chaduma?
Utapata taabu wewe ambaye unaaambiwa nini cha kuandika na unaandika, hata kama ni utumbo wenye kunuka na kukuonyesha kuwa mtupu kichwani. Jitambue.
 
Kampuni ya automobile Ltd imesaini mkataba na Kampuni ya Youngsan Gloner Corporation ya Korea Kusini kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kuunda magari hapa nchini. Kiwanda hicho kitaanza kufanyakazi mwakani na gari la kwanza litetengenezwa Kati ya mwezi Septemba na Oktoba na kiwanda hicho kinatarajia kutoa Amira rasmi zaidi ya 500 na zisizo rasmi zaidi ya 1000.

Mwenyekiti mtendaji wa IPP, DK Reginald Mengi aliyasema hayo Jana jijini Dar es salaam wakati wa kutoa saini makubaliano na kampuni hiyo. Aliongeza zaidi ya shilingi bilioni 22 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya kwanza.

Habari hizi ni njema sana kwa Watanzania hasa kwa wapenda maendeleo kwani licha ya ajira zitakazo patikana kwa Watanzania, inatuweka katika taswira ya ushindani wa kimaendeleo na jirani hasa Kenya na Rwanda ambazo zimeripotiwa kuwa na viwanda hivyo!

IMG_1180.JPG
 
Hakuna kitu kama hicho. Mengi ni mjanja mjanja tu anataka kumpaka mafuta jpm kwamba na yeye anashiriki katika uchumi wa viwanda. Alisema anajenga kiwanda cha kutengeneza simu za smartphone mpaka lei kapiga kimya leo anakuja na swaga jingine. Watanzania msilishwe ujinga kubalini jpm nchi imemshinda na uchumi unaporomoka kwa kasi.
Uchumi unapimwa na;
C=consumption rate
I= investment level
G=government spending
X= exports
M=imports
X-M= net export ambayo sasa hivi ni negative
Hence uchumi tz unashuka kwa speed kali
 
Badilisha kichwa cha uzi sema Wakorea..........na si Dr Mengi.......watu hawa kwa kupeana ujiko na kuhadaa watz ni hatariiiiii
 
Kwa hiyo Mengi kufungua kiwanda cha ku-assemble magari na simu ni uthibitisho kwamba uchumi wa nchi hauyumbi? Nani amekuambia, Lumumba?
Akili yako finyu sana huwezi hata huisha hiyo meseji ki-mantiki. kwa uzoefu wa biashara na uwekezaji alio nao kwa zaidi ya miaka 40, Lazima ajue mazingira rafiki ya kuwekeza. hivyo sehemu inayo yumba hawezi wekeza.
 
Tangu aseme atajenga Hospitali ya magonjwa ya moyo , miaka 20 iliyopita uliona hata mchanga au kokoto ?

Mzee Mengi badala ya kutuona mazuzu ni vema basi ukakamilisha miradi uliyotueleza mwanzo kabla ya kukurupukia mengine .
Unataka ashindane na tasisi ya Muhimbili?
 
Kwa hiyo Mengi kufungua kiwanda cha ku-assemble magari na simu ni uthibitisho kwamba uchumi wa nchi hauyumbi? Nani amekuambia, Lumumba?
Lakini angeingia ubia na Toyota angekuwa kwenye sehemu nzuri zaid kuliko Hyundai
 
Back
Top Bottom