Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Kitu cha pekee ninachoamini ni kuwa Kitila hamjui Zitto wala hajui dhamira ya moyoni mwa Zitto. Ameburuzwa tu na bahati mbaya amekubali kuburuzika

...Unamjua vizuri Kitila Mkumbo ww au umemfahamia CDM???
 
so kitila mkumbo you need mbadala wa cdm na ccm, kwa hiyo mlitaka muangamize cdm ili muelekee kwa huyo mbala. Acheni uhuni bhana.

Wakati wa uchaguzi 2010 kampeni zinaendelea. Zitto alikuwa busy kutangaza atagombea urais 2015. Was it right timing? Acheni uhuni na kuaminisha wananchi ujinga.

Ndio zitto alitaka kugombea uenyekiti wa cdm, kitila nakwambia kwamba, huyo zitto wako angepata uenyekiti leo cdm isingekuwepo.

Endelea kutuletea porojo zako unadhani wote ni mabwege.......
tatizo la zitto hakumbuki nyuma huyu kaka yangu, nilimshangaa sana kutueleza kampeni za mwaka 2015 kwenye kampain za 2010 ni mbinafsi sana na kujiona anaweza kuwa peke yake na kuishi ,zitto anatakiwa kujua kwamba bila jitihada na uadilifu na uvumilivu wa viongozi wetu wa sasa hakika chadema isingekuwa na nguvu kiasi hiki.
 
Ndugu watanzania,na wana CHADEMA kwa ujumla,tuache ushabiki usiyo na mantiki,Dr Kitila na Zitto kuna makosa na siri kubwa wanazozijua dhidi ya uongozi wa CDM,na kwa kuliona hilo wakaamua kuandaa waraka,hivyo NAMKUBALI SANA DR. KITILA MKUMBO,HAKIKA UTASHINDA DR. ,NA MUNGU AKUSAIDIE .

Labda shetani amsaidie
 
Kweli Kabisa Kitila na busara Zako, nakuheshimu sana mwalimu wangu, ila you are messing with people's minds. You could have used a little bit of your psychology. You are right, but where were you Mkumbo? This is a shame. Zitto ana tuhuma za mda mrefu ambazo hajakanusha tangu enzi za -----------, leo unaandae naye mkakati? People won't beleave you even if you are right. May be you had a big picture. God bless you.
 
We' Dr kitila bora uendelee kulinda heshima yako kuliko kuendelea kutumika na mtu kama zitto ambae amekubali kutumika na mafisadi Nimegundua wewe na zitto niwalafi wamadara kwenye bandiko lako nimadaraka tu mnalilia sisi atutaki watu kamanyie wanafiki wasaliti kuusu kushabikia mtu iyo haipo ndomana tumekataa kuwashabikia wewe na zitto endelea kutulaumu lakini ujue mtanzania waleo sio waezi zile wanaona ujinga mnaofanya wewe ndio ulituambia chadema nimbadala wa ccm leo hii unatuambia kinatakiwa chama kingine sajawahi uona msomi mwenye Akili finyu kama wewe. Ole wenu mnao rudisha harakati nyuma.
Nina maswali matatu ya msingi kwa huyu Dr.Mkumbo...1. Akiwa mmoja wapo ya washauri wa cdm ni kwa nini hakuwa shauri wajitahidi kujenga chama badala ya ufuasi wa viongozi?2. Akiwa kama mjumbe wa cc kwanini hayo matatizo waliyo orodhesha katika waraka wao hawakuomba yajadiliwe na vikao rasmi ndani ya chama?3. Kama mwanachama hai wa chama cha cdm ni kwanini waliandaa waraka unaogawa wanachama kwenye makundi badala ya kujenga taasisi yaani chama?. Kwa kutaka mbadala wa ccm na chadema ni kutaka kutimiza matakwa yenu na shoga zako ya kuwa viongozi kwa njia za panya, nendeni Chauma....biblia ina sema 'watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu' naungana na le mutuz kuwa wewe ni mnafiki tu, ila zzk naye ana kiburi cha uzima na ndo maana amedai yeye hata kufa kama wangwe. Kwa le mutuz kumbuka mkapa alivyo sema kwenye kikao cha uteuzi wa mgombea wa ccm..' ccm haitafuti malaika bali kiongozi'. England kiongozi aki kutwa na kahaba kesho yake anajiuzuru, france kuwa na kimada ni sifa, tanzania kumbuka ya marehemu ditopile
 
Ipo siku Watanzania mtaanini tu,kwamba Uongozi wa juu wa CDM ndy tatizo

Tunatambua viongozi walioko ndani ya chama Achana na wasaliti walioko mahakamani Uwezi kuishi namwana mke alie kupueleka makamani.
 
Na system ilipendezwa naye baada ya kuondoka DARUSO bila kashfa yoyote tofauti na kina Kusaja...Mwaimu nk. Ogopa sana presidents walioitawala DARUSO bila Kunji.

Poleni sana mkuu, sikuweoo udsm kipindi chake ila mambo yake tukiyasikia sana. Kuna vijana wako ofcn wanamzungumzia sana. Akuwahadaa webzake sana maana nasikia alichomekwa pale baada ya kudondosha system mwingine Mutubgirei. Mkumbo huna nyimbo
 
Nina maswali matatu ya msingi kwa huyu Dr.Mkumbo...1. Akiwa mmoja wapo ya washauri wa cdm ni kwa nini hakuwa shauri wajitahidi kujenga chama badala ya ufuasi wa viongozi?2. Akiwa kama mjumbe wa cc kwanini hayo matatizo waliyo orodhesha katika waraka wao hawakuomba yajadiliwe na vikao rasmi ndani ya chama?3. Kama mwanachama hai wa chama cha cdm ni kwanini waliandaa waraka unaogawa wanachama kwenye makundi badala ya kujenga taasisi yaani chama?. Kwa kutaka mbadala wa ccm na chadema ni kutaka kutimiza matakwa yenu na shoga zako ya kuwa viongozi kwa njia za panya, nendeni Chauma....biblia ina sema 'watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu' naungana na le mutuz kuwa wewe ni mnafiki tu, ila zzk naye ana kiburi cha uzima na ndo maana amedai yeye hata kufa kama wangwe. Kwa le mutuz kumbuka mkapa alivyo sema kwenye kikao cha uteuzi wa mgombea wa ccm..' ccm haitafuti malaika bali kiongozi'. England kiongozi aki kutwa na kahaba kesho yake anajiuzuru, france kuwa na kimada ni sifa, tanzania kumbuka ya marehemu ditopile

Kuna watu ndani ya cdm hasa Mbowe na Lissu hawashauri hata chembe.
 
Teh teh teh! Kumbe hata Dr. anatemaga pumba. Maelezo meeengi but no point. Hiv unadhani kila m2 akiandaa kundi lake la kugombea uenyekit hicho chama kitakuwa na hali gan? Aibu yenu.
 
Dr. Kitila...
Unaweza ukafikiri uko sawa kwa maandishi wako na vile vile ukaendelea kusifiwa na maccm kutokana na andishi lako ila Wataka mabadiliko sehemu yeyot ile Duniani watakupuuza kwaandishi kama hili...
Ulitaka chama kiendelee kuwakumbatia kwa kukiuka misingi na taratibu za chama? hivi kweli hamuoni kuwa mlitenda kosa? ama ni ule Ununda mnataka muuonyeshe kwenye umma kuwa mmeonewa japokuwa umma unajua mmepata Haki stahiki za kuvuliwa uanachama?

Nadhani huu ungekuwa muda wako muafaka wa kukaa na kujitafakari upya ya namna utakavyoweza kuomba uanachama wa Chadema upya badala ya kuendeleza majungu yasiyo kuwa na kichwa wala miguu, Acha kuendelea kujifedhehesha, mnaweza mkadhani mnanguvu pale mnaposhangiliwa kwenye mitandao ama mahala popote pale kumbe ni Adui zenu wanawazomea bila nyie kujijua.

Kwaandika lako hilo linatuonyesha kuwa chama kilipaswa kuendelea kuwakumbatia hata kama mnafanya makosa kwakuwa eti nyie ni Maarufu siku mkiondoka chadema itayumba na itadhoofika, Hizi ni fikra finyu sana na dhaifu mno kuwahi kunenwa na wanaojiita wasomi duniani ama wataalum wa siasa duniani ama watakamabadiliko.

Kwaandiko lako hilo, kama CHADEMA nia yake ingalikuwa nikuwakumbatia wanaoenda kinyume na taratibu na misingi iliyojiwekea sidhani kama CHADEMA ingekuwa tofauti na LICCM, Wakati wote nimekuwa nikijifunza siasa ndani ya CHADEMA sijawahi kuona sehemu yeyote inayosema kuwa anayeenda kinyume na misingi ya chama ama Taratibu za chama kwakuwa yeye ni maarufu basi chama kikae chini kizungumze naye kiyamalize ilichama kisiingie kwenye migogoro.... hivi ni kweli CHADEMA kuwachukulia hatua stahiki wanachama wake kimeingia kwenye mgogoro mkubwa ambao unakiyumbisha? Unahitaji akili za kiuwenda wazimu kuwaza hivyo.

La msingi nikuwa Haitakaa itokee wala haitatokea kwa CHADEMA kuyumba eti kwakuchukua maamuzi kwa wanachama wake wanaoenda kinyume na taratibu za chama... bali CHADEMA itayumba endapo itaogopa kuchukua hatua sitahiki kwa mwanachama wake yeyote yule anaekwenda kinyume na taratibu zilizoweka.

Mbona Mbowe anakwenda kinyume na Taratibu stahiki lakini mnamwogopa?mifano hai ipo mengi sana Mojawapo ni Uteuzi wa kimagumashi wa wabunge Viti Maalum kukibambikia chama madeni feki na kujilipa kwa nguvu pesa za chama kisha nae kuwakopesha wana cc pesa ili kuwaziba midomo wasithubutu kumgusa masilahi yake anayoyachuma kimafia hapo CDM makao makuu na wote Mliopo hapo makao makuu lazima umwabudu Mbowe kinyume na hapo akina wapambe zake wanakuundia zengwe kwa mtiririko huu Mbowe nae anastahili kuwajibika kwani tayari amekwenda kinyume na katiba ya CDM
 
Mwalimu Kitila
Pole yaliyokukuta, ila naamini ulichelewa sana kutambua hilo. Kwa kweli kama umelitambua leo ama baada ya kukubwa na dhahama basi, siku nyingine ningekushauri utafute njia mbadala ambayo itakupa uwezo wa kuyabaini na kuyafanyia projection jinsi mambo yatakavyokua baadae. Kule kwetu, wavuvi kabla ya kuingia ktk mitumbwi na mashua yao hutimua kajivumbi fulani na kuweza kubashiri kwa hakika kabisa kwamba mda fulani upepo utakua wa kasi gani na utakuwa unavuma kutoka upande fulani kuelekea upande fulani, sasa swali kwanini tusijifunze busara za wavuvi hawa?. Lakini, bado nina uwalakini ya kwamba je ni kweli hasa tatizo umelibaini?

Mie naamini ni kweli tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA, lakini huo mbadala huo unaongelea unatakiwa uwa na attributes za namna zipi? Je ni mbadala wa kubadili jina la chama, ama mbadala wa kuandika katiba ktk makatasi ya chama kipya? Mbadala wa namna hii mie kwa muono wangu sio mwarabani.

Huko nyuma, niliwahi kukubishia kwamba tatizo lilopo sio CCM na wala mwarobaini wake sio CHADEMA, kwa namna fulani uliniita "MNAFIKI", nilikaa kimya nikasema mwalimu mzuri ni kumpa mda, mwalimu Kitila.

Mwalimu Kitila, kosa wapinzani wanalofanya na wewe naona unaelekea kulifanya ni lilelile la kuaminisha watu kwamba tatizo la Tanzania ni kwa sababu ya entity ambayo hai-exists kama vile:CHADEMA, CCM,CUF nk.

Mwl Kitila, ngoja nirudie tena kujaribu kurudia muono wangu, wenda leo kwa vile upo huru kama mie hapa, unaweza japo kuangalia huu muono ktk jicho tofauti. Na nasem kuwa tatizo la Tanzania linasababishwa na linaendelezwa na ile existing entity, hii existsing entity ni watanzania wenyewe . Tatizo lilomo na linasobabisha matatizo ktk Tanzania ni watazania wenyewe na tatizo sugu ilikiwa limejikita ktk ile dhana ya mindset ya mtanzania.

Mwl Kitila, unaweza tengeneza chama kipya mbadala chenye jina zuri na katiba ktk makaratasi nzuri sana na hiyo katiba ikawa nzuri sana kupita zote duniani, lakini kama wanachama na viongozi wake watakuwa ndo sisi hawa watanzania hawa hawa kwa mindset hii iliyopo hii hii, basi tegemea maumivu tu. Kwani nini kitachowafanya wasisahau kuchapa baadhi ya vipengele kwenye katiba yako nzuri?
Ngonja, niishie hapa kwa kuvipumzisha vidole, lakini nachelea kuamini kwamba wenda chanzo cha tatizo haswa hujapata kukiona, ila nafurahi kuwa umelishuhudia kwa maandiko yako ya kwamba vyama hivi vilivyopo na wanachama wake hawa hawana msaada wowote kwa mtanzania mnyongeu. Hivyo, ukombozi wa kweli bado sana kuwaidia. Maana, hata CCM kesho wakianguka sioni tofauti ya mpokea kijiti atachofanya cha ziada.
 
Binafsi angekaa kimya ningejilazimisha kumuona anabusara kidogo! bt kwa mashuzi haya kumbe nae kiwewe cha usaliti kinamsumbua.Maana kwa bandiko hili naona kwa mbaaali kama anataka kutuandaa waTz kisaikolojia kukisubiri chama chao kipya wanachotaka kuanzisha!, Hii inawezekana baada ya kupima uwezekano wa kukubaliwa kujiunga na vilivyopo na kupewa nafasi ya wanayoyataka ni mdogo! kama tunavyo wafahamu hawa mabwana ni wapenda ujiko na wabinafsi.Sasa huu si muda wa kuendeleza kelele bali ni muda wa yeye na wanakikundi wenzake waende wakaanzishe chama chao na wakiendeshe hivyo wanavyoona wao kinafaa.Wanaume wazima kilasiku kuwanung'unikia wanaume wenzako bila kuchukua hatua chanya ni udhaifu.
 
Mbowe hapaswi kuwa m/kiti tena ni FISADI KAMA CCM WENGINE,Anakula mamilioni kibao na kupiga kelele platforms kuwaaminisha watanzania uongo,wote na ZZK ni kitu kimoja.
 
Kwenye andiko hili la Mh Dr. Kitila nimeona kuna sehemu mbili au tatu kama kajichanganya

1.Anaposema uteuzi ni kwa wateule tu

na sio kama utaratibu ulivyo wa kujaza fomu na kurudisha

Swali katika waraka huo ambao waliuandaa je walipiga kura wenyewe wa nne kwa maana dr kitila,zitto,mwigamba na huyo mm2 na zito akashinda?au waliamua tu kumteua au alijiteua zito mwenyewe?


2.Chama hakijengi mfumo wa kushabikiwa ila viongozi wametengenexa mfumo wa kushabikiwa wao,viongozi

Je hapo haoni kama zitto nae amehusika kutengeneza mfumo huo mbona na yeye alikuwa na watu wanaomuunga mkono yeye kama yeye?

3.Hivi dr katiba yetu ya leo na hii rasimu ikipita umri wa MGOMEA URAIS UTAKUA NA NIKUANZIA MIAKA MINGAPI

JE zitto mungu akitujalia uhai atakua amefikisha umri halisi wa kupigiwa kura kama rais????

4.Hivi NCCR MAGEUZI NA CHADEMA mwaka 2010 waliopeperusha bendera ya kugombea urais walikuwa wenyeviti wa VYAMA VYAO????????


SHUKRANI MLETA UZI NA DR KITILA.

Acha kujidai hsujaelew ... kwani HECHE alimshinda vipi HANIB kams sio ubani wawakubwa!!!!


Well said dr, mimi nilikuafuasi wa CDM kupitia wewr...! Wamekufukuza nami nakufukuza
 
Back
Top Bottom