Makete Kwetu
JF-Expert Member
- Jan 8, 2012
- 531
- 166
Kwa andishi lililo kwenye warake ule, Dr huna Moral Authority ya kushauri kitu chochote hata kwa CCM, mwanasaikologia kama wewe usingeweza toa matusi kiasi kile
Sikubaliani na wale wanaosema Dr. Kitila aache siasa. Dr. Kitila amesema wazi vyama vyote vilivyopo vinaendeshwa kwa ... zidume fikra za mwenyekiti wa chama... So Kitila move forward tutoke hapo maCCM na maCHADEMA ni hayo hayo!
Katiba maana yake ni nn?? Kama unaenda kinyume na katiba ya chama lazima tuwe na wasiwasi hata ukipata nafasi ya juu unaweza kuvunja hata katiba ya nchi. Hapa Unaogea mkojo matokeo utazidi kunuka....
mkuu Mkwawa ukiona mtu haheshimu mamlaka iliyo juu yake basi huyo hafai.
Kumwita kiongozi wako hana elimu, eti yupo too local n.k huku ukifahamu fika huo uongozi amepewa na wanachama huo ni utomvu wa nidhamu wa hali ya juu
likewise kumpigia mtu kampeni kwa kutumia propaganda za kidini na muflisi tuu wa mawazo na fikra ambaye anaweza kuyatenda.
Dr. Ametenda yote haya why not to be kissed off?
MAADILI NI NGUZO MHIMU YA UONGOZI.
Kumekwepo na jitihada ama za makusudi, ama za kutokujua, ama za kile kinachoitwa kumsafisha mbowe.
Niweke wazi kwamba sikumkosoa mbowe kuhusu mambo ya mahusiano anayosemekana kuwa nayo na wabunge wake wa viti maalumu, bali ni kuhusu KUKIUKA KWAKE MAADILI YA UONGOZI.
1) Kitendo cha kukatisha ziara ya mbunge wake wa kazi maalumu ili wakakutane Dubai kwa kazi maalumu badala ya kazi ya nchi aliyotumwa tena arudi toka marekani mpk Dubai kwa fedha za serikali ni matumizi mabaya ya fedha za umma na ni ukosefu wa maadili ya uongozi. Angemrudisha kwa gharama zake yaani kwa fedha zake hapo ingekuwa mambo binafsi. Kufanya mambo binafsi kwa fedha ya umma haiwezi ikawa jambo binfsi. Hivyo sikukosoa mapenzi yao bali matumizi ya kodi za masikini kwa mambo binafsi.
2) Kumlazimisha Afisa wa bunge abadili tiketi ileile iliyokuwa aende kwenye shughuli ya bunge sasa ageuze aende kwenye kazi maalumu hili sio jambo binafsi ni matumizi mabaya ya madaraka. Ni kukosa huruma kwa hali ya juu kwa watanzania.
3) Kumlazimisha mbunge wake wa kazi maalumu kuachana na safari ya kikazi na kuacha nchi ikose mwakilishi kwenye kikao hicho huku tayari akuwa ameshagharamiwa safari hiyo, huku tayari akiwa ameshaziba fursa hiyo ambaye mbunge mwingine angeweza kwenda kuliwakilisha taifa halafu mbowe na mtu wake wakaenda kwenye kipaombele chake cha kuburudika dubai ni ukosefu wa uzalendo kwa Taifa na ni ukosefu wa maadili ya kiuongozi.
Tumeongea kwakuwa wametumia fedha za umma, tumesema kwa sababu wameacha kazi ya umma huku wakiwa wamechukua fedha kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania na tunasema kwakuwa wamewanyima fursa wabunge wengene ambao wangekwenda kuwakilisha Taifa endapo fursa hiyo hangepewa mtu elibadilishiwa safari ya ya taifa na kuitwa kwa kazi maalumu.
"Ukipewa kazi ya nchi lazima ujiheshimu" NITASHANGAA SANA NITAKAPORUDI BUNGE LIJALO NIKIKUTA MBOWE BADO NI KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI
Inahitaji Weledi wa hali ya juu kumuelewa Nguli Kitila Mkumbo, Pale tutakapoacha kushabikia Viongozi na badala yake kupenda CHAMA, tutaweza kuchambua hoja za msingi na kasoro zilizopo katika uongozi.
- Kaka huwezi kuwaita Viongozi wanapokea rushwa kuwa ni wastaarabu zaidi ya genge la wahuni, nasema tena waliomfukuza Kitila ni genge la wahuni wenzake kama yeye, walipokuwa wanafukuzwa wenzake yeye mbona hakusema haya, haya ameyajua lini toka majuzi tu walipomfukuza? siku zote hakujua haya? Please Kitila amefukuzwa na genge la wahuni wapokea rushwa, wajaza mimba wabunge wa viti maalum ambao anafanana nao sana, Zitto hafananai nao wewe hao kama sio wahuni kwa nini wanakwenda kujisafisha kwenye magazeti ya udaku?
- Wewe nitajie mwanasiasa unayemjua mkubwa duniani uluyewahi kumsikia anaedna kujiosafisha kwenye magazeti ya udaku kama alivyofanya Lissu, aibuu ndio maana ya genge la wahuni kaka!!
Le Mutuz
Hebu ngoja tusubiri tuone ila Politics ni dynamic sana! sometime history can be used to predict the future and vise versa is true!
Alaf kwenye siasa hakuna permanent group (kambi)! nadhan Kenya inaweza kuwa case study nzuri hapa na unaweza kuongezea mfano kutoka CCM! ile kambi ya wana mtandao wa 2005 sasa hivi ikoje?!
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA
ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.
Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.
Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.
Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.
Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.
Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.
Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.
Msaliti mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.
Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!
Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.
Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.
Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.
Source: Raia Mwema
Komredi ishu ya huyu jamaa ako kumega beki 3 iliishia wapi?
Kitu cha pekee ninachoamini ni kuwa Kitila hamjui Zitto wala hajui dhamira ya moyoni mwa Zitto. Ameburuzwa tu na bahati mbaya amekubali kuburuzika
Vita hii ninavyoi haianzii kwenye waraka. Waraka ni matokeo ya ugomvi ndani ya chama chenu wa muda mrefu, hata maamuzi ya viongozi wa chama chenu msingi wake sio waraka ni mafuriko ya muda mrefu yaliyokuwa yakitafuta mlango wa kutokea sasa yamepata pa kutokea ni vigumu kuzuia maji ya mafuriko kwa mikono. Yaache mafuriko apite utajipanga kiangazi kikifika.Uliweka mkakati wa kushinda uchaguzi. Hii ilikuwa ni mbinu yako ya kuwashinda viongozi waliopo madarakani sasa hivi. Lakini na wao pia wanahitaji kushinda uchaguzi. Kila mtu ni kwa kutumia mbinu wanazozijua. Moja ni kukuondoa kwenye ushindani. Unapohitaji kushinda vita usisahau kushambulia. Unaposhambulia usisahau kuwa utashambuliwa. Kabla ya kushambulia ni vizuri ukajua nguvu a adui wako. To know an enemy is to be half equiped to conquer.Dr. Ulisahau ukadhali utamshambulia adui ambaye asingeshambulia. Kofi la kushitukiza linauma zaidi kuliko kofi ulilolitegemea. Usinung'unike vita ulivianzisha mwenyewe usilaumu matokeo
We' Dr kitila bora uendelee kulinda heshima yako kuliko kuendelea kutumika na mtu kama zitto ambae amekubali kutumika na mafisadi Nimegundua wewe na zitto niwalafi wamadara kwenye bandiko lako nimadaraka tu mnalilia sisi atutaki watu kamanyie wanafiki wasaliti kuusu kushabikia mtu iyo haipo ndomana tumekataa kuwashabikia wewe na zitto endelea kutulaumu lakini ujue mtanzania waleo sio waezi zile wanaona ujinga mnaofanya wewe ndio ulituambia chadema nimbadala wa ccm leo hii unatuambia kinatakiwa chama kingine sajawahi kuona msomi mwenye Akili finyu kama wewe. Ole wenu mnao rudisha harakati nyuma.