Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti’ mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.


Source:
Raia Mwema

Dr Mkumbo, kwa uandishi huu unathibitisha ulijua mini unakifanya nahatima take sio kupata huo ushindi wenu mlio kuwa mnaundaa. Mlijua kama vile NCCR ndio litakachotokea ILA siolazima uwe dr kujua Hilo halitatokea!Inakuwaje kwa akili yako uunge mkono harakati ya mtu moja kutafuta cheo tena cha huu kibnafsi bila kufuata utaratibu na kanuni na kuhitimisha kunyimwa ridhaa yawazee. Mikutano yote mikuu iliyowahi kufanyika kulishawahi kutoka hoja ya kubadili mwenyekiti ikazimwa? CDM imeinuka aghalabu miaka kumi bado yangu uhai wake, huoni swala la uongozi WA huu Ni mambo nyeti Sana katika kuhifadhi mafanikio? Bila hoi ndio sababu iliyopelekea wazee walione Hilo na kushauri mabafiliko ya muda kuhusu muda WA uongozi! Kama msomi WA sayansi ya siasa hata Ni mambo ya kawaida kabisa katika mapambano. Mliona mmechelewa mini kataka kipindi kifupi hiki kama sio lengo lenye dhamira mbaya na chama.

Kwa Hilo hataujitetee vipi, hakuna WA kuwaeleweni. Matumizi ya mbinu za kijasusi ndani ya chama eti kutafuta ushindi Ni usaliti kwa vile hauna baraka ya chama basi. MM M1 M2 3 4....ya mini mlikuwa mnaficha kama Nia yenu ilikuwa njema, hiyo mwingine hadi Leo humtaji.

Usidanganye watu demokrasia ya vyama vingi Ni Kula mtu kuamka asubuhi na kutaka kuongoza. Vinginevyo tafsri ni kuwa chombo kiwe na sukani nyingi Kisha kiende mrama ndio lengo lenu! Hata CCM wanavyo zuia hizi Nia kutangazwa ni taratibu Tu na nidhamu na hasa kulinda umoja na mshikamano ndani ya chama mambo ambalo ninyi hamkuliona. Wazee wapi nawataendelea kuwapo hata sio ktk vyama Tu hata maisha ya Kula siku. Michango Yao haipimiki kwa kilo.

Kumbukeni watu wamekufa, wamefungwa wrnye kesi ndio usiseme, Leo CDM kuanza Tu kupata umaatufu na nguvu ghafla mnaona uongozi unawafaa nyie. Laana zitswatafuna milele..

Wengine tuliokuwa watazamaji sasa tunaunga mkono rasmi CDM. Ni mti eenye matunda kumbe kwa hayo mawe mnayokitupia

Mtaondoka na Mimi tutajiunga ishirini.

Huo sio usomi, CDM needs to be a Vanguard party at some stage no problem with that!
 
Kitila Mkumbo unajulikana wazi wewe ni system. Na Njoka akikuweks karibu na Zitto ummalize kisiasa. Zzk pole sana. Na Msacky naye kama mmoja wao anafanya kazi yake.

Na system ilipendezwa naye baada ya kuondoka DARUSO bila kashfa yoyote tofauti na kina Kusaja...Mwaimu nk. Ogopa sana presidents walioitawala DARUSO bila Kunji.
 
Tena wewe jamaa Mkumbo nimetokea kukuchukia sana pamoja na huyo @Zito ......eti mtaeleza watu waelewe ukweli ndani ya CDM...siku zote uko wapi usilekebishe ila leo baada ya kufukuzwa ndio ulete ujinga wako humu....ninaongea kwa hasira sana hapa ungejua potelea mbali mods kwa lugha kali niliyotumia kama matanipiga ban fine nitakuwa nimepunguza sumu za hasira mwilini mwangu, .....U wait in our days wasariti wote mtatulipa tu kwa huu upuzi, hata kama viongozi wengine wanamapungufu zipo njia za ndani nawe kama sehemu ya huo uongozi mngerekebisha. Ni aibu kuwa na mwalimu mp....z kiasi hiki
 
Ndugu watanzania,na wana CHADEMA kwa ujumla,tuache ushabiki usiyo na mantiki,Dr Kitila na Zitto kuna makosa na siri kubwa wanazozijua dhidi ya uongozi wa CDM,na kwa kuliona hilo wakaamua kuandaa waraka,hivyo NAMKUBALI SANA DR. KITILA MKUMBO,HAKIKA UTASHINDA DR. ,NA MUNGU AKUSAIDIE .

hizo siri aende kumpa Jack Nzoka na Mwigulu hatumtaki yeye na siri zake hatuziogopi. Usalama wa Taifa wanafukuzwa, CIA wanafukuzwa KGB wanafukuzwa ije kuwa ZZK
 
Tena wewe jamaa Mkumbo nimetokea kukuchukia sana pamoja na huyo @Zito ......eti mtaeleza watu waelewe ukweli ndani ya CDM...siku zote uko wapi usilekebishe ila leo baada ya kufukuzwa ndio ulete ujinga wako humu....ninaongea kwa hasira sana hapa ungejua potelea mbali mods kwa lugha kali niliyotumia kama matanipiga ban fine nitakuwa nimepunguza sumu za hasira mwilini mwangu, .....U wait in our days wasariti wote mtatulipa tu kwa huu upuzi, hata kama viongozi wengine wanamapungufu zipo njia za ndani nawe kama sehemu ya huo uongozi mngerekebisha. Ni aibu kuwa na mwalimu mp....z kiasi hiki

Wewe ndy lijinga kabisa,je wajua ukweli wowote kuhusu Mbowe?
 
Wewe Mkumbo Unamtisha nani hapa wewe ni Mwalimu na msomi lakini hujui tofauti ya majira, usifananishe CDM ya nyakati hizi za karne ya 21 na NCCR ya nyakati za VHS, analog ya karne ya 20. Yote aliyoandika yanaonyesha kuwa ana personal vendetta na viongozi wa CDM, Shut UP and swallow your arrogance.
 
Hivi kama kila mtu anayetaka uongozi wa juu wa chama angetumia mbinu hizo za kusimika watu wao kila kanda na mbaya zaidi kukashifu na kuwatukana msiokubaliana je ingekuwa chama au klanu ya ppmbe tena za kieji?

Kama mpaka leo hajaona madhara ya mipango yao hatamu basi kuna kitu anakipigania anachokijua yeye mwenyewe.
 
Iramba bado tunakuamini sana,tena sana.

Tunazungumzia mustakabali wa nchi na si Iramba peke yake wala kisehemu kidogo cha nchi, kwa ID yako tu inaonesha jinsi gani ulivyojaa ukabila , kwa kusema hivyo nihitimishe kwa kusema hata kauli inasadifu yaliyokujaa, maana hata maandiko matakatifu yanasema yamtokayo mtu ndio yaliyomjaa.......jichunguze mwenyewe....ni ushauri tu.
 
Dr Kitila mwalimu wangu,sisi vijana hatuelewi hizo hadithi zako bwana. Wewe jibu zile taarifa za kupokea sh.200000 wewe na Shibuda kutoka kwa Zitto kama sehemu ya mtandao wake.
 
Sin uhakika kama Watanzania vichwa vyetu vinafanya kazi vizuri au vipi,Aliyosema Dr Kitila ni ukweli mtupu kwa Uongozi wa sasa haujajenga ufuasi wa Chama bali umejenga ufuasi wa Viongozi.Huu ni ukweli mtupu na nitawapa mfano mdogo tu.Hivi karibuni Mwenyekiti wa Chadema alikatiza safari ya Mbunge wa Viti maalum aliyekuwa katika ziara ya kikazi Barani Ulaya akiwa ni miongoni mwa Wabunge walioteuliwa kwaajili ya ziara hiyo ya kimafunzo,Ikabidi Mbunge huyo wa jinsia ya kike akatishe safari yake na kuelekea huko Dubai kwaajili ya masuala yao binafsi tena wakizitumia kodi zetu,Ila kwasababu ya mahaba yaliyopitiliza waliyonayo baadhi ya WanaChadema kwa Kiongozi huyo hawakuliona hili kama ni tatizo na inaitia dosari Chama kinachojipambanua kwamba kinapigana kuleta mabadiliko.Kama WanaChadema wangekuwa na mahaba na Chama nadhani sasa hivi they would have been calling for Mbowe's head,Wangekuwa wanamshinikiza Mbowe aachie ngazi ili asiendelee kukichafua Chama lakini kiuhalisia Watu hawana mapenzi na Chama bali Viongozi
 
Hata kule Ujerumani Hitler alikuja na maneno kama haya, kumbe alikuwa nayake nyuma ya pazia. Huyu Dr katumwa na Shetani ila Hajui na Kwa nguvu za Mungu hawezi Kushida.
 
Kusema bado Dr Kitila anahitajika Iramba si ukabila wakuu,Mi si mchaga wala mnyakyusa waliojaa ukabila kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini.
 
Dr. Yuko right kabisa, kua kunawateule, nikirejea kauli ya MTEI kuwa makamu m/kiti aliyejiuzuru ndo alikua ameandaliwa, ila watakumbuka tu wale wenye kumbukumbu lakini wale mashabiki waviongozi!
 
Back
Top Bottom