Nimeisoma makala hii kwa umakini mkubwa. Nadiriki kukubaliana na mtoa mada kwa msingi huu; kuwa Demokrasia ya kweli katika nchi hizi zinazoendelea inaminywa sana, kuna kosa gani kupanga mkakati wa ushindi? Maana rahisi ya Demokrasia ni uhuru wa watu kuchagua viongozi wanaowataka, sasa kwa nini kuwa na ndoto za kugombea nafasi fulani ndani ya chama iwe usaliti? Na laiti kama CDM ingekuwa imeshika dola basi akina ZZK na Dr. Kitila leo wangekuwa gerezani kwa kosa linalosemwa ni Uhaini....Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa wakivutiwa na siasa za CDM lakini kutokana na kinachoendelea sasa ndani ya CDM kwa hakika sifikirii kama naweza kushiriki katika shughuli za chama hiki kama hapo awali.
Tusiwe na haraka ya kuwashambulia akina ZZK bila kuweka mambo katika mizania, kitu cha kujiuliza kwanini kila anayetoka CDM anatoka akisema ubaya ule ule kwa Viongozi? Alisema hayo Nakaaya Sumari, Shonza, Mwampamba, nk na pia sasa Zito na Kitila wanasema hayo hayo. Hivi hawa wote ------------ kweli? Ushauri wangu kwa CDM, imalize huu mgogoro kwa suluhu ndani ya Chama. Niliishasema hapo awali uwepo wa Dr. Slaa kama Katibu Mkuu ambaye alipita Mikoani na kufukuza fukuza hovyo Viongozi wa Chama wa Wilaya, Mikoa na hata Madiwani akidhani anaimarisha Chama kumbe laah ni mzigo. Hana sifa za kuwa mgombea wa Urais, hana jipya zaidi ya wimbo wake uliozoeleka wa ufisadi, nje ya ufisadi ana jipya gani??
Kwa Upande wa Mhe. M/kiti Mbowe amefanya aliyoweza kufanya lakini tunahitaji Mwenyekiti atakayekisaidia Chama kutoa ushindani wa dhati katika kuelekea kuchukua dola. Siasa za kuchukua fedha za mafisadi haziwezi kutusaidia kukishinda chama kilichoko madarakani. Heshima ya Mbowe itaendelea kuwepo kama atachukua maamuzi magumu kujiudhulu mara moja. Tusidanganyane, CDM kwa sasa si imara kama ilivyokuwa 2010, kunahitajika mabadiliko makubwa sana ili kurudisha imani.
Ni jambo la kusubiri na kuona lakini bila kutafuna maneno uongozi wote wa juu wa CDM umepoteza credibility unatakiwa ujitafakari na kuvua gwanda. Sioni kama kesho Mbowe anaweza kusimama kwa ujasiri ndani ya Bunge kukemea ufisadi wakati yeye mwenyewe amekiri kupokea fedha za mafisadi. Katu haiwezekani.
Bado fursa ipo, mjiuzuru mara moja.