Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Mkuu wabara

Bahati mbaya sana wafuasi wa Chadema wengi hawajitambui kabisa sijui kwa nini watu wamekuwa na tabia za nyumbu.

Nyumbu wapo lumumba fc aka buk 7,wao wanaendekeza ushabiki wao wa kijinga kwa chama chakavu huku elimu ya watoto wao ikifa,tembo wanatoweka,vijana wanakufa kwa dawa za kulevya,ardhi yao inaporwa na wageni,huduma za afya zinazorota,wakulima wanapunjwa bei,wafanyakazi wanalipwa kiduchu huku mabilioni yakifichwa uswis na maccm,viwanda ambavyo vingewapatia ajira vinageuzwa magodauni,reli yao inakufa ili malori ya maccm yapate kazi.JITAMBUE, ACHA USHABIKI MANDAZI!
 
Last edited by a moderator:
Huyu Dr anatapatapa kuficha aibu ya usaliti yake. Hasichojua masikini huyu ni jinsi anavyozidi kuonesha udhaifu na upofu wake ktk siasa. Haya ndio mapungufu ya wasomi ya nchi hii. Maanake wasomi wengi wa tz wamejaa woga ktk harakati za kuleta mageuzi hapa nchini na ndio maana ni rahisi kurubuniwa.

mkuu Jifunze kwanza kuandika then umkosoe msomi ambae ana haki zote za kuzungumza kwa uweledi wake
 
the write-up is TOO SUPERIOR compared to brains of chademe pro mbowe.
lakini hata hivyo KITILA ameandika kwa ajili ya wenye akili ambao hawapo kwenye kambi ya mbowe
 
Kama wewe Mkumbo na mamluki wenzako mnataka mbadala wa Chadema na hicho chama cha makaburu weusi, anzisheni chama chenu; mbona rahisi tu ndugu. Kwa nini upige kelele na kuhitaji huruma ya wa Tanzania wakati nia mnayo, uwezo mnayo na wafuasi mnao. Umehusika vp kutatua changamoto na matatizo ndani ya chama kwa kipindi chote ulipokuepo? Na kwa nini usubiri utimuliwe ndo uyaone na kuyasema hayo mapungufu? Chadema ni mbadala wa ccm daima itasonga mbele, hamuwezi shindana na nguvu ya umma.
 
Inahitaji Weledi wa hali ya juu kumuelewa Nguli Kitila Mkumbo, Pale tutakapoacha kushabikia Viongozi na badala yake kupenda CHAMA, tutaweza kuchambua hoja za msingi na kasoro zilizopo katika uongozi.

Ni kweli uko sahihi lakini kwa nyakati tofauti nilizokutana na Zitto nilimuona ni mtu wa kujikweza na kupenda umashuhuri pia anajiiweka mwenye akili ya juu sana kuliko mtu yeyote ndani ya chadema wakati mie namuona katika intellect hafikii uwezo wa Tundu Lissu wala Mnyika ila ni mwenye uwezo wa kati pia anayeweza kuthubutu bila woga jambo ambalo lisimfanye afikirie ana akili ya juu sana kuliko wenzake
 
....Wewe ulivyofukuzwa umetimka na washabiki wangapi?.

we chizi nn, umeambiwa zito lakini bado unang'ang'ania kuuliza 'mbona wewe?!' - kwani yeye hajioni au unataka ajibu kulingana na matakwa yako?!
chadema haipaswi kuongozwa kwa utamaduni wa chama cha mapinduzi, real democracy LAZIMA ifuate mkondo wake!!!
 
Nimeisoma makala hii kwa umakini mkubwa. Nadiriki kukubaliana na mtoa mada kwa msingi huu; kuwa Demokrasia ya kweli katika nchi hizi zinazoendelea inaminywa sana, kuna kosa gani kupanga mkakati wa ushindi? Maana rahisi ya Demokrasia ni uhuru wa watu kuchagua viongozi wanaowataka, sasa kwa nini kuwa na ndoto za kugombea nafasi fulani ndani ya chama iwe usaliti? Na laiti kama CDM ingekuwa imeshika dola basi akina ZZK na Dr. Kitila leo wangekuwa gerezani kwa kosa linalosemwa ni Uhaini....Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa wakivutiwa na siasa za CDM lakini kutokana na kinachoendelea sasa ndani ya CDM kwa hakika sifikirii kama naweza kushiriki katika shughuli za chama hiki kama hapo awali.

Tusiwe na haraka ya kuwashambulia akina ZZK bila kuweka mambo katika mizania, kitu cha kujiuliza kwanini kila anayetoka CDM anatoka akisema ubaya ule ule kwa Viongozi? Alisema hayo Nakaaya Sumari, Shonza, Mwampamba, nk na pia sasa Zito na Kitila wanasema hayo hayo. Hivi hawa wote ------------ kweli? Ushauri wangu kwa CDM, imalize huu mgogoro kwa suluhu ndani ya Chama. Niliishasema hapo awali uwepo wa Dr. Slaa kama Katibu Mkuu ambaye alipita Mikoani na kufukuza fukuza hovyo Viongozi wa Chama wa Wilaya, Mikoa na hata Madiwani akidhani anaimarisha Chama kumbe laah ni mzigo. Hana sifa za kuwa mgombea wa Urais, hana jipya zaidi ya wimbo wake uliozoeleka wa ufisadi, nje ya ufisadi ana jipya gani??

Kwa Upande wa Mhe. M/kiti Mbowe amefanya aliyoweza kufanya lakini tunahitaji Mwenyekiti atakayekisaidia Chama kutoa ushindani wa dhati katika kuelekea kuchukua dola. Siasa za kuchukua fedha za mafisadi haziwezi kutusaidia kukishinda chama kilichoko madarakani. Heshima ya Mbowe itaendelea kuwepo kama atachukua maamuzi magumu kujiudhulu mara moja. Tusidanganyane, CDM kwa sasa si imara kama ilivyokuwa 2010, kunahitajika mabadiliko makubwa sana ili kurudisha imani.

Ni jambo la kusubiri na kuona lakini bila kutafuna maneno uongozi wote wa juu wa CDM umepoteza credibility unatakiwa ujitafakari na kuvua gwanda. Sioni kama kesho Mbowe anaweza kusimama kwa ujasiri ndani ya Bunge kukemea ufisadi wakati yeye mwenyewe amekiri kupokea fedha za mafisadi. Katu haiwezekani.

Bado fursa ipo, mjiuzuru mara moja.
 
Umesema ukweli kabisa sisi tumewaonya sana na pia kama wameshindwa kutatua ndani kimnya kimnya na kutoa onyo na mashabiki wanashindwa kujua kuwa chama kimewatengeneza watu na watu ni maarufu kuzidi chama!! Ila chadema wanajidanganya sana kuona kama wako imara kumbe sio
 
hata tundu lisu anatatizo kubwa la kujiona yeye ndo yeye na ni mbishi kwel kwel, hata ktk mgogoro huu wa zito kakishauri chama (kamati kuu) vibaya kisheria na hatimaye kikashindwa kufuata katiba ya chama ktk kumfukuza zito...
kwa maoni yangu, yalikuwa ni makosa makubwa kumfanya tundu lisu kuwa mwanasheria mkuu wa chama!!
na nadhani mbowe amempa cheo hicho baada ya kumsoma lisu kuwa kibaraka wake ili kuhalalisha uzinzi wake ndani ya chama kama alivyokurupuka majuzi kwenda global publishers kumsafisha!!!!!!!!!!
 
Mh Dr. Pole tena kwa janga la KISIASA ulilokutana nalo maana niliwahi kuota your the next Katibu mkuu. Ila kubaliana na wanaoamini kuwa mkakati wenu wa USHINDI usingeuacha chama salama hata kidogo. Huwezi kuwa unataka uongozi Wa chama kwa mbinu ya kushambulia viongozi wa chama then ukataraji chama kitabaki Salama hakiwezi hata kidogo hapa ndio tafsiri ya mlikuwa na lengo la kukibomoa chama kwa tafsiri ya mabadiliko
 
Mh Dr. Pole tena kwa janga la KISIASA ulilokutana nalo maana niliwahi kuota your the next Katibu mkuu. Ila kubaliana na wanaoamini kuwa mkakati wenu wa USHINDI usingeuacha chama salama hata kidogo. Huwezi kuwa unataka uongozi Wa chama kwa mbinu ya kushambulia viongozi wa chama then ukataraji chama kitabaki Salama hakiwezi hata kidogo hapa ndio tafsiri ya mlikuwa na lengo la kukibomoa chama kwa tafsiri ya mabadiliko.
Zile lawama za kuhusu fedha za Mwigamba mmesahau kuwa yeye ndie alikuwa bursary? Amesahau yeye anajua mambo mengi ya fedha kuliko mwingine ndani ya chama? Ana uhalali Wa kushusha lawama zote zile?
Mwisho wa siku mtu mmliyemtaka awe m/kiti asingekiacha chama Salama hata kidogo.
 
Kwa mtazamo wangu, naona Dr alikua anajaribu kujitetea ili ionekana kama uamuzi uliofanywa na chama haukua sahihi. Nimesoma kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa utulivu lakini sijaona sehemu yoyote katika andishi lake akigusia kuhusu kufuatwa au kutofuatwa kwa katiba katika maumuzi yaliyotolewa na chama. Ningemuonea huruma endapo angetushawishi kwa kosa lililomnfukuza ndani ya chama halikua kosa kikatiba na hivyo hakustahili adhabu aliyopewa.

Kwa upande wa pili, ni vigumu sana kutenganisha chama na uongozi kwa sababu maamuzi ya chama hufanywa na uongozi na hivyo uamuzi wa viongozi (unaofata katiba) ni uamuzi wa chama. Uamuzi wa viongozi usiofata katiba si uamuzi wa chama na ndio mana unaweza kupingwa mahakamani na uamuzi huo ukafutwa. Kwa mtazamo huo, naona sio sahihi kuhusisha pande mbili za MM's na viongozi (sio chama) katika mgogoro uliotokea. Mi naona mgogoro ulikua wa pande mbili ambazo ni MM's na chama, kwa sababu matendo ya MM's yalikua kinyume na katiba.

Kwa mtazamo huo pia, naona wale wanaowatetea MM's waliingia kwenye chama kuwafata hao viongozi na kwa hiyo ni wafuasi wa viongozi hao na sio wafuasi wa chama. Wakati wale wanaotetea maamuzi yaliyofanywa na viongozi wanakitetea chama kwa sababu maamuzi hayo ni maamuzi ya chama.
 
Huyu Ndg. Kitila Mkumbo; anatafuta huruma ya wa Tanzania, kwanza ameidhalilisha sana hicho kinachoitwa (u Dr) sikutegemea yeye na kisomo chote hicho angeshiriki mkakati haramu ndani ya chama bila kufuata taratibu,kanuni na misingi ya chama. Hapa anataka tuamini kuwa njama na mkakati wao ulikua sahihi? Kukifananisha nccr ya enzi hizo na CDM ya sasa; kuwa akifukuzwa Zito, CDM itakufa....! Atasubiri milele. Hivi hawa wanaojiita wasomi wameisaiaje Taifa letu?

Nimeisoma makala yako na naamini nimeielewa. Nasasa naamin fika kuwa wewe na zito mmeshiriki kukivunja nguvu chama cha CDM.

Umekiri kuhusika kuandaa waraka wa kumuandaa zito kushika nafac za juu na hivyo kuunda kundi lenu la kumpigia zito campain. Dr. Hamkuona mnatengeneza makundi na hivyo kukigawa chama?

Dr. Umekiri kuwa watu wamewashabikia viongozi badala ya chama. Kutokana na ninyi kuunda makundi ndan ya chama, ni wafuasi wa kundi lipi wanaotetea kiongozi badala ya chama. Naomba nikukumbushe tu mabango ya wafuasi wa viongozi yalivyokuwa ZITO KWANZA CHAMA BAADAYE. Bango hilo linatoa ujumbe gani? Wewe na zito mpo mnachekelea bila kukemea.

Nashauri, zito kwahali iliyopo CDM amejenga au amebomoa chama. Na kuwa anang'ang'ania kubaki CDM wakati amejenga uadui na viongozi waandamizi wenzake atafanyaje kazi. Ni mawazo yangu tu!

Mm kma shabiki wa siasa ninafikiria hivi!
 
Nimeisoma makala yako na naamini nimeielewa. Nasasa naamin fika kuwa wewe na zito mmeshiriki kukivunja nguvu chama cha CDM.

Umekiri kuhusika kuandaa waraka wa kumuandaa zito kushika nafac za juu na hivyo kuunda kundi lenu la kumpigia zito campain. Dr. Hamkuona mnatengeneza makundi na hivyo kukigawa chama?

Dr. Umekiri kuwa watu wamewashabikia viongozi badala ya chama. Kutokana na ninyi kuunda makundi ndan ya chama, ni wafuasi wa kundi lipi wanaotetea kiongozi badala ya chama. Naomba nikukumbushe tu mabango ya wafuasi wa viongozi yalivyokuwa ZITO KWANZA CHAMA BAADAYE. Bango hilo linatoa ujumbe gani? Wewe na zito mpo mnachekelea bila kukemea.

Nashauri, zito kwahali iliyopo CDM amejenga au amebomoa chama. Na kuwa anang'ang'ania kubaki CDM wakati amejenga uadui na viongozi waandamizi wenzake atafanyaje kazi. Ni mawazo yangu tu!

Mm kma shabiki wa siasa ninafikiria hivi!
 
Dr. Kitila. Analalamikia ushabiki wa wanachama wakati huohuo makala yake na mkakati wao wa mabadiliko 2013, umeonesha pasina shaka kwamba Dr. Kitila ni shabiki namba moja wa ZZK. Na ni dhahiri kwamba yeye kama kiongozi kuwa 'shabiki' na hadi kupanga mipango haramu kiasi cha kutoa lugha kama "kiongozi Mkuu yuko too local" na nyenginezo za kuudhi huyu jamaa hakufaa kuwa kiongozi kabisa.

Sijui anatufundisha nini Sie tusio viongozi au wasomi walobobea kama yeye?
 
@ Nyanya Mbichi natamani Dr Mkumbo akubali au akatae kama hakuwa kwenye payroll ya TISS na CCM kupitia kwa ZZK??
Je hiyo sio kuhujumu chama kwa mbinu za MaCCM??
Dr mzima hakujua ma Paymaster wake ni nani???
 
Tunapoita viongozi wahuni na wazinzi tufunge macho turudi kwa wazazi wetu waliokuwa viongozi tukawafanyie tathmini.!!!!! Ngoja nianze na mzee wangu!!!
...sijui kama Le Mutuz atakuelewa.
 
anzisheni chama chenu mjinga sana utasema mengi sana chadema tunazidi kusonga mbele daima bora tubaki na viongozi 70 waaminifu kuliko kuwa na viongozi 670 wahuni :wasaliti kama wewe ; zitto na wenzako chadema daima tunafanya maamuzi magumu nenda kaungane na wale madiwani wanne wale wa arusha muanzishe chama chenu zitto awe mwenyekiti wenuu kama mnao mmeonewa
 
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti’ mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.


Source:
Raia Mwema

Wasomi wetu bwana!sijui anafikiria nini!
Mbona hazungumzii katiba ambayo ni msingi wa yote?
Msomi anaonekana amekata tamaa sana,yuko defeated na hili tetemeko.....he is not a good captain.
 
Back
Top Bottom