- Thread starter
- #141
Hoja yako ni nzito mkuu. Big up!
Mtauana bure vichwa vibovu wote. Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe wakati akitokea mkoani mbeya alipitapita mikoa ya ruvuma na iringa akasema" natarajia kuachia nafasi ya uenyekiti ili mtanzania mwingine mwenye uwezo wa kuongoza chama (CDM) agombee. Na ningependa sana mtu huyo asitoke ukanda wa kaskazini ili kuwatoa shaka wale wenye dhana ya kwamba CDM ni chama cha kichaga" mwisho wa kunukuu.
Mtoa mada alimaanisha aliyosema Mbowe. Na kwa kiingereza neno presidency au president sio lazima akawa kiongozi anayeongoza state au dola. ni kiongozi yeyote mwenye mamlaka, hata chairman anaweza akaitwa president kama akina madega wa yanga, papa msofe, marehemu abasi gulamali wa yanga na wengine kibao. maliyaga wa sinza.
mwisho, wana CDM fatilieni matamshi na hotuba wanazotoa viongozi wenu ili msitoane macho kwa ujuha. Mkianza kutafuta nani amrithi nani mtakuwa kama magamba mtakwisha. hamna uzoefu wa kuvumuliana nyie mna jazba nyingi mtashikiana mapanga. Chonde sitaki tusi.