Pamoja na yote mazuri na mabaya yanayosemwa na watu kumhusu huyu Dr. Ndodi, mimi nina angalizo;
1. Je nani anyeweza kutujulisha kilichotokea hadi akamwambia huo mgonjwa wa pdiddy alete mil.3? hapo lazima tukubali kwamba kulikuwa na mazungumzo, katika hali ya kawaida kama mgonjwa hakuridhika lazima atafute namna ya kumsema vibaya dk wake na hawezi kusema ya upande wake, kwahiyo sidhani kama ni jambo la busara kuanza kumshambulia mtu wa watu kwa maelezo ya upande mmoja. kama kungekuwa na maelezo ya upande wa pili hapo tungeweza kuwa fair katika mashambulizi tunayoelekeza kwa dr. ndodi.
2.Suala la uhai wa mtu ama kifo chake linabaki kwenye mamlaka ya MUNGU mwenyezi, tusijaribu kumrundikia ndodi tuhuma ambazo hastahili. Hata rais wa zamani wa Yugoslavia,bw.Tito alifariki dunia akiwa amezungukwa na madaktari bingwa wa kila aina lakini kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kutoa na kuchukua uhai alikuwa ameamua tito alifariki dunia akiwa amezungukwa na madaktari bingwa.
Kama kuna mtu katibiwa kwa ndodi na hakupona hilo sio jambo la ajabu kwakuwa yeye ni mwanadamu tu, siye MUNGU, hata huko mahospitalini watu wanakufa tena wakiwa wametumia gharama kubwa. Mwl. Nyerere alipelekwa uingereza kutibiwa lakini alifariki ni sawa na wengine waliokwenda sehemu mbalimbali kutibiwa na hawakupona. Na kuna wengine wengi wanatibiwa kwenye hospitali kubwa hapa nchini ama nje ya nchi, kwa waganga wa kienyeji na kwingineko na hupona ama vinginevyo, jamani tusimnyoshee kidole huyu muungwana kwa suala la kifo, maana tunasahau msururu wa watu waliopona kwa tiba yake na walikuwa wamekata tamaa huko mahospitalini.
3. Kwakuwa anakuwa na vipindi vya television na anatoa namba zake watu wanatuma sms na hata kupiga simu, mbona sijawahi kusikia mtu akituma sms ama kupiga simu kulalamika zaidi ya kusikia watu wakiulizia matatizo yao mbalimbali ili wasaidiwe? Mi nadhani kama kuna tatizo kwenye huduma zake watu wasingekuwa wanamiminika kila siku kwenda kwake, au kama ana customer care mbovu na bado watu wanamiminika kwenda kwake basi tatizo haliko kwake pekee.