Dr. Isaack Ndodi: Hisia mchanganyiko

Isaac Ndodi....Isaac Ndodiii!....same guy kila siku.../whyyyy?
Hakuna ishuzingine?
Akinenepa mnaulizana,...
Akikonda mnamshangaa..
Give him a break...kweeek!

Oooh Sorry Dr. Ndodi!!!!
 

Watu wengi wanampondea siku hizi, mimi naomba kutoa ushuhuda, amenisaidia sana, tena bure kwa kuangalia kwenye tv tu. Kuna siku aliweka mada ya kufanya mazoezi, kunywa maji kwa wingi, matunda na mboga mboga, nimefuata kanuni zake na zimenisaidia, awali nilikuwa nikiona mtu mwembamba nilikuwa natamani kweli wembamba, tatizo lilikuwa kwenye hivi vitu vinaitwa bear na nyama choma, lakini tangu nilipoangalia kile kipindi kwa kweli imenisaidia sana. Siku hizi bear nakunywa week end tu.

Huwa nakwazika anapojiita Mtume, wakati anauza dawa mpaka 400,000. Kuna aunt yangu aliwahi kwenda kwake kwa matibabu alikuwa hapati mtoto, hakumuuliza mambo mengi, ile kusema hapati mtoto tu 400,000/= hapo ndo alinichosha ni Mtume gani ambaye huwa anasaidia watu kwa kuwalipisha mijihela mingi hivyo? Kuna mwingine yuko huku Loliondo anatibu sana magonjwa ya aina zote ambayo hayatibiki kwa shs.500.00 tu, cancer, ukimwi, kisukari na mengine kibao ambayo unayajua wewe mwana jf.
 

Sio medical doctor..labda tuambie udokta mwingine wa mtaani
 
inabidi serikali impatie support ya kutosha ili dawa zake kila mtanzania awe na uwezo wa kuzipata kama vile babu wa loliondo! lkn dawa

ya maleria tu kwa ndodi ni tsh 400,000/=, je mtanzania wa kawaida atawezaje kumudu??

otherwise!! tunamuombea maisha mema na marefu!!!!!!
 
sasa hivi ni loliondo tu bei karibu na bure na tiba ya uhakika.
 
Sasa hivi ndodi 'kaiva ile mbaya! Kasakafia kupita maelezo. Si ndodi yule wa miaka minne iliyopita. Tusubiri na Babu naye anze kunawiri
 
me naona ni tapeli tu, kwa sababu hizo dawa zake anauza bei ghali sana halafu ukiacha kutumia ugonjwa unarudi kama kawaida hata kama dozi ni ya wiki mbili, hizo wiki mbili zikipita ukiacha kutumia ugonjwa unarudi kama vile hujawai kutumia dawa yoyote.
 

uko sawa mkuu!.
 
Huyu ni mfanyabiashara - sishangai mbinu anazotumia

Mkuu umenena katika mstari mmoja. Huyu jamaa anayeitwa Dindo naweza kumwelezea kama ni acabra dabra kama sio tapeli. Jamaa yangu alilipa hela hadi laki saba lakini hakuna kupona wala nini. mpwa wangu pia ingawaje kwa kipato chake laki 3 alizolipa ni sawa na milioni tatu - hakuna cha kupona wala mtoto wake. Kibaya anatumia Biblia kunyaka watu. Jamani tumwogope Muumba. Wanaomshabikia ni wale wanaopenda porojo zake. Waugue waende au wapeleke ndugu zao ndipo watakapozijua true colours za huyu jamaa.
 
Pwent? au pont, Any way sio kitu, mtoa mada amesema huyu bwana ni ghali sana, ukitaka kumuona ni Tsh 50,000/= hapo matibabu bado,

Ni vyema tukamuomba akaangalia kipato cha watanzania akapunguza kidogo.

Pont au point? any way wote mmeeleweka.
 
Ndodi ni mshenzi na tapeli mkubwa. Mwanaume gani anaongea kama malaya mitaani. Dawa zake ni bei kubwa sana na sidhani kama kuna tiba ya ghali kiasi hicho hapa nchini. Wanaomfagilia ndodi ni wale wanaopenda porojo. Wakitaka wamfahamu vizuri basi waende zahanati yake wakaulizie bei za dawa zake. Watashikwa na butwaa. Mshenzi sana huyo.
 
isack ndodi. Huyu jamaa ni kiboko. Sijajua yupo kundi gani. Dawa bure lakini kiingilio ni ghali kuliko dawa
 
To me he is boaring kwa kuwa hakuna mada asiyejua yeye na kuna muda anapotosha mambo asiyoyajua
 
Naunga mkono mada asilimia 100,hawezi kuwa mtume na ni mfanyabiashara,na kwa sasa wanakosa soko cos babu anatoa kikombe mia tano tu.
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…