Aliyeandika huu UPUUZI atakuwa si Mtanzania na tena hata ART hakusoma achilia mbali SCIENCE. Huwezi kuwa Mtanzania wa kweli ukaukimbia ukweli na kutaka uungwe mkono katika upuuzi wako eti kisa DINI. Hizi ni shield-guards mufilisi za wasio na hoja bali vioja. Na ukitaka kuwa domo la Wanasayansi ni vema utambue vizuri kanuni, taratibu na lugha za Ki-sayansi. Wanasayansi wa kweli hawaongei wala kuongelewa kwa hoja lojolojo kama za huyu Quemu.
Bahati nzuri naifahamu COSTECH kitambo na kiundani kiasi. Kabla ya Dr. Mshinda kuletwa hapa, COSTECH kilikuwa kijiwe kwa maana ya kijiwe cha uswazi; mahala pa watu kupata ghahawa na kashata. Ilikuwa kama anwani tu ya Wapi Utampata a, b, au c. Waliokuwa wajanja kama T. Mlaki wakatumia kijiwe ilivyo kujinufaisha kimaslahi. Vitu vingi ikawa ni shaghala-baghala. Kohi pamoja na elimu zake zote (U-Dokta, U-Profesa, n.k) na vyeo (Jenerali, DG, n.k) akafunikwa na Mlaki. T. Mlaki akawa kama ndiye DG wa COSTECH. Miradi mingi sana imeanzishwa na Mlaki huku DG akiwa hajui kitu. Na nchi wafadhili nyingi zilidhani Mlaki ndiye DG. Na Mchaga hakufanya kosa. Palipo na upenyo anafanya kweli.
Can you imagine:
- COSTECH litoe huduma kama ISP na hakuna mtu ndani ya shirika anajua nani analipwa?
- Jengo zima la serikali, hazina ya Tafiti za Kisayansi lipigwe rangi za matangazo ya Vodacom na bado waliomo wajione wana hadhi?!
Wengi mmeandika kuhusu uwezo mkubwa wa Dr. Mshinda kwa kurejea mafanikio yake pale Ifajara. Nami ninaafiki na siongezi wala kupunguza; salute kwa Dr. Mshinda.
Hawa wanaojiita wanasayansi 15 mie napenda tuwaite wanafunzi 15. Wanasayansi gani toka wamehitimu hizo PhD, MSc hawajawahi kushiriki au kuandika wenyewe Tafiti hata moja? Wakiandika basi wameshirikishwa! Ni Aibu Wanataka waitwe wanasayansi, wapewe na vyeo vya mseleleko na heshima wasiyostahili. Sasa hakuna mseleleko wala heshima bila ku-publish. Baadhi ya hawa wanaojiita wanasayansi 15 walishindikana hata huko kwenye vyuo vya elimu ya juu wakafukuzwa. Wana matatizo kweli kweli.
Huyu Quemu na wote wanaokimbilia hoja mfu za UDINI wanatia hasira kweli. Wanawanyima moyo hawa watu wema, Wazalendo na washapakazi. Hatupaswi kuwaendekeza. Lazima JF Admn nayo ione haja ya kuwaongeza watu wa namna hii kwenye vifungo (BAN). Wanaitia sana hasara nchi kwa kuikwamisha kuiletea maendeleo kwa kuwagawa watu.
Nashukuru Quem amepata majibu yanayomstahili. Arudi akawaambie wanafunzi wenziwe kuwa vioja vyetu vimebainika. Badala ya kumpaka tope Dr. Mshinda tumesababisha watu wamtambue zaidi kwa mshango wake mwema kuiendeleza nchi.