Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Adolph Kumburu azidi kuonyesha vituko

A.Bitegeko

Member
Aug 25, 2013
13
1
Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Adolph Kumburu azidi kuonyesha vituko

Hali si swari ndani ya Bodi ya kahawa nchini (TCB) ambako mambo ya kushangaza na kusikitisha,yanazidi kuibuka kila uchao yanayoambatana na matumizi mabaya ya mali za bodi huku Waziri mwenye dhamana akiendelea kufumbia macho uozo unaoendelea ndani ya bodi hiyo ambayo ndiyo mboni ya jicho la mkulima wa zao la kahawa nchini.

Inasikitisha kuona kwamba mkurugenzi wa bodi hiyo ambaye amebakiza wiki takribani 5 mkataba wake wa ajira ya miaka mitano umalizike,hadi sasa amekaa kimya bila kutoa taarifa kwa bodi ya wakurugenzi yenye mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya kahawa,cha kushangaza ameiruka bodi ya wakurugenzi na kumwandikia waziri moja kwa moja kumwomba waziri ambae ni swahiba wake amwongezee mkataba.
Anachokifanya kwa sasa Bw Kumburu ni kusubiri kuona kama waziri atatoa maamuzi ya kukubali barua yake ya maombi ya kutaka kuendelea na uongozi wa kuua bodi hiyo na kuikabidhi kwa wazungu.

Kwa sasa mkurugenzi huyo mkuu Adolph Kumburu bila ya kuelewa anachokifanya ameonekana akitaka kuondoka na wafanyakazi wote ikiwa ni pamoja na yeye bila kujijua. Ameonekana akitoa Scheme of Service ya shirika hilo ikiwa imetayarishwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw A.Bitegeko (a.k.a Mzee wa mademu mjini Moshi kutokana na hela apatazo ni nyingi sana hasa za exchange rate za dola za wakulima na zabuni za shirika na zile za halimashauri za Wilaya) ambaye nae ni kati ya wale wanao wania kiti hicho kwa hamu kubwa kama vile kiti hicho ni cha kurithishana.

Bitegeko amekuwa akijifanya ni rafiki mkubwa wa Bw Kumburu (tumewahi kusikia kuwa huko NSSF alikotokea hakutoka salama baada ya kugushi zaidi ya Sh Mln.20. na ndio maana alikimbia mapema akisaidiwa na aliyekuwa waziri wa fedha wakati huo Mh Mstapha Mkullo).Na ndipo kutokana na baba yake kuwa rafiki na aliyekuwa Mwenyekiti wakati huo Pius Ngeze na ndiye aliyemsaidia kupata kazi kwenye bodi hiyo bila vikwazo na kumwacha aliyekuwa ameshinda nafasi hiyo (interview)

Ameshasikika akitamba mara kwa mara kama ambavyo anavyotamba hivi sasa kuwa naibu waziri Kighoma Malima ni mtu wake wa karibu sana hivyo hakuna shida yoyote,U-DG lazima aupate kwa kuwa naibu waziri huyo ameshamwahidi kuwa atamsaidia kwa hilo,alisikika na kurekodiwa Bw Bitegeko.(Sehemu ya recording hiyo iliyorekodiwa na mmoja wa makahaba wake wa mtaani tutaiweka hapa siku za usoni).

Bw,Bitegeko akiwa ameagiza magari mazuri ya bei mbaya, amekuwa akitangaza kuuza magari yake mawili aliyonayo ili aweze kuudanganya umma.

Ni Bw Bitegeko ambaye katengeneza scheme of service akionyesha ya kuwa kila mfanyakazi wa bodi hiyo anatakiwa kuwa na Master’s degree,huku akijua wazi kuwa DG wake Kumburu hana Master’s degree na kwamba huyo Bw Kumburu ana kadegree kamoja alikokapata UDSM ka introduction ya Engineering.

Bw Bitegeko anawachezea shera kwa kuwa anajua vizuri kabisa kuwa kulingana na scheme aliyoipitisha kwa kuhonga inamuengua rafiki yake bandia na hivyo kubaki na mpinzani wake kwenye kiti hicho Bw Primusi Kimariyo ambaye naye hana vigezo vya kumtisha kwa kuwa naye ana MBA kama yeye. Anamwona Primusi pia kuwa hafai kutokana na utendaji wake wa kubabaisha hasa kwenye kuwasababishia wakulima hasara wakati wa kutoa bei elekezi zisizo za kweli.

Bitegeko pamoja na kuwa na vigezo vya kuwaengua wenzake bado anazo dosari nyingi ambazo wanashirikiana na Bw Kumburu hasa za kuwaibia wakulima hela zao kupitia exchange rate na fedha za halimashauri za wilaya Kahawa zitokapo hasa Kusini mwa nchi.

Hili hufanywa na mastermind wao Bw Goodluck Moshi ambae nae huko nyuma aliwahi kutuhumiwa na utawala uliopita kwa wizi wa hela za mauzo ya kahawa kwenye kitengo cha kukaanga na kuuza kahawa CRU kilichopo mjini Moshi,na kukiri kwa maandishi na alipoonewa huruma na uongozi uliopita ilibidi ahamishiwe Bukoba ili kuficha uovu huo (yaleyale ya kitanzania).

Hivi sasa Bw Goodluck Moshi toka arudishwe makao makuu ya bodi mjini Moshi kutoka Bukoba na Bw Kumburu na akishirikiana na Bw Bitegeko ameweza kujenga nyumba kadhaa kwa ajili ya wake zake lukuki alionao na hivi sasa anamalizia Ghorofa lake la kifahari mjini Moshi.Wakati Bw Bitegeko anajenga yak wake Mjini Morogoro.

Wizi wa fedha za Halimashauri za wilaya wanazokula ni zile wanazozituma kwenye halimashauri husika baada ya kuzikata kwenye mauzo ya kahawa za wakulima au PCB.Fedha hizi wanapozituma huzituma kimakosa makusudi, baadae fedha hizo zinarudishwa kwenye mfumo wa cash na hapo zinaporudi ndipo kazi inapofanyikia.

Kitendo cha halimashauri husika kuomba bodi ya kahawa kuwakusanyia fedha za ushuru toka kwenye mauzo ya kahawa za wakulima au wale wanaoitwa coffee buyers ndio ilikuwa utaratibu wa watu fulani kwenye wilaya hizo kuzitafuna fedha hizo wakishirikiana na wezi wa bodi hiyo,

Hii ilikuwa ni akili ya hali ya juu sana waliyotumia kufanikisha hili na mpaka sasa inasemekana ni kiasi cha Tsh 500 milioni zimeshaliwa kwa kipindi cha misimu miwili tu bila hata wakaguzi wa ndani kujua hilo.Hawa jamaa walipoona kuna wajanja ambao wamegundua hili wajanja hao walihamishwa haraka sana na kukimbizwa mikoani Mbeya na Bukoba ili wasione tena.

Viongozi hao ambao ni Bw Adolph Kumburu,Asteri Bitegeko na Primus Kimaryo wanaongoza shirika hilo kwa kuwanyayasa wafanyakazi wa bodi hiyo kwa kiwango kikubwa sana.Kutokana na wafanyakazi hao kushindwa kupeleka malalamiko yao kwa menejimenti ambayo ni wao wao imewabidi kumwandikia barua Waziri lakini pia huko kwa waziri zinagonga ukuta kutokana na waziri akihitaji kupata maelezo ya kina kunatokea mizengwe mingi kwa wale wanaotumwa na wakiondoka ndipo Kumburu anamwandikia waziri barua zenye uongo wa kutisha huku akimweleza waziri kuwa maswala hayo anamuomba amwachie kwamba menejimenti inayashuhulikia na hapo ndipo pia inasemekana majibu hayo huwa yanaambatana na bahasha nono za kumziba waziri huyo pamoja na naibu wake mdomo.

Hivi sasa wameibua jambo la kushangaza kwa kubadilisha vitasa vya milango ya ofisi zao kwa kuweka vitasa vya kufunga kwa namba (code) kitendo kilichoshangaza wengi kwa kuwa hata ofisi ya waziri mwenye dhamana haina vitasa hivyo vya namba na kufanya ofisi zao kuwa kama milango ya benki na safe zake za kuweka hela.

Wafanyakazi wanajiuliza hivi siku hizi kahawa inauzwa kwa cash au vipi! Waziri mwenye dhamana haya yote huyaelewi ?.

Kutokana na ubabe unaoendelea bila ya kutokea hata mmoja wa kiongozi ngazi ya juu serikalini kuukemea,imewafanya Wafanyakazi wa bodi hiyo kuoonekana kuwa wanyonge kutokana na hilo na wengi wao wamesikika wakisema wanamwachia Mungu.

Bodi ya kahawa kwa sasa inaonekana kama Shirika la ajabu na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuokoa jahazi, linaweza kuipa serikali mzigo mkubwa siku za usoni kutokana na kutakiwa kuajiri wafanyakazi wapya wenye Masters pekee.Kumburu yeye anasema hataguswa kwa vile pamoja na kuwa na kadigirii kamoja pekee anasema yeye anateuliwa na waziri rafiki yake na Injinia mwenzake hivyo atamfumbia macho. Degree aliyonayo Bw Kumburu inaruhusu fundi Mchundo huyo kufanya kazi kwenye viwanda vya kusaga mahindi vijijini pekee.

Ili kuhakikisha anaongezewa mkataba Kumburu amekuwa akiwaandama wale wenye Masters za Kilimo na wale wenye Masters za Engineering akiwaona wao ndio tishio kwake,

Bila kujua Bitegeko na Primus hawako nae kwa kuwa wanajua hana vigezo hivyo wako wakiomba Mungu ni lini atatoka hapo ili mmoja wao akamate usukani. .

Habari za ndani kabisa zimebaini kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wa Bodi hiyo wameomba nafasi ya kumwona Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa na vielelezo vya kutosha,ikiwa ni pamoja na jinsi fedha za wakulima zilinavyoliwa hii ni kutokana na Waziri mwenye dhamana kufumbia macho hayo yanayoendelea amesikika mfanyakazi mmoja akisema wacha iwe mbaya wamechoka.Na ikishindikana hapo kwa raisi basi watapeleka nyaraka hizo upinzani ili kila kitu kianikwe adharani.

Hata hivyo Bw Kumburu katika hali nyingine ya kushangaza ni pale alipokataa kuwalipa wafanyakazi waliostaafu kazi mafao yao akisingizia kuwa Wizara/serikali ndio iliyokataa wasiwalipe wafanyakazi hao na kusababisha wafanyakazi hao kukimbilia mahakani na mpaka sasa hivi kesi inaendelea mahakamani.

Lakini katika hali nyingine ya kushangaza zaidi ni pale ambapo yeye Kumburu baada ya kusema serikali/wizara imekataa wanaostaafu wasilipwe mafao yao yeye binafsi kwa kuwa ameshikilia mpini na kwa kuwa muda wake wa mkataba unaishia amejiwekea yeye binafsi mafao yake yasiyopungua Tsh 60 milioni kwenye bajeti ambayo anasubiri bodi ya wakurugenzi ije kuyapitisha na kuacha wengi kumshangaa mtu huyo alivyo mnyama na asivyo mwanadamu kujiwekea mafao yake huku akikataa kuwalipa wengine.

Inasikitisha anavyoshindwa kuongoza shirika lenye wafanyakazi wasiozidi 100 na huku akisikika kuwa anajitayarisha kwenda kugombea Ubunge huko kwao Mbinga kumwondoa Mh Capt Komba au Mh Kayumbo.

Yote haya waziri mwenye dhamana na bodi hii akiwa amefumbia macho bila hata ya huruma.Imagine mtu kafanya kazi miaka yake yote halafu anastaafu Kumburu na washirika wake Bitegeko na Primus wanakataa kuwalipa. Wamama hao ambao wengi wao ni wajane wamebaki wakisema wanamwachia Mola

Ni hivi karibuni mnamo tarehe 15/8/2013 Bw Kumburu akiwa kwenye kikao na wafanyakazi wa bodi hiyo alidhubutu kusema kuwa, hata kama yeye hana Masters degeree hakuna wa kumuuliza wala kumchunguza kwa hilo kwa kuwa waziri ndiye anaemtabua na kwamba kama kuna mtu analalamika kuhusu scheme of service anaweza kuacha kazi mwenyewe na kwamba sio lazima wanaolalamika kufanya kazi kwenye bodi hiyo wala hakuna mwenye hisa kwenye bodi hiyo.Kwamba yeye kama yeye hawezi kutotekeleza wajibu wa serikali kama ilivyoagiza. Sasa hapa sijui yeye ana hisa ngapi kwenye shirika hilo.

Hakuna asiyefahamu kuwa Bodi ndio zinazotayarisha scheme of service na kupeleka serikalini ili zikapitishwe na sio serikali ndio inyozitayarishia bodi za mazao scheme of service bodi hizo.Aaache kufanya watu watoto wadogo.

Serikali inatakiwa iingilie kati kumaliza migogoro ndani ya Bodi inayoletwa na vita vya madaraka kwa kutomwongezea Kumburu Mkataba na kumtafuta DG mwenye sifa arudishe heshima ya Bodi na atakaye heshimu uzoefu na michango ya wafanyakazi ambao wengi wao wamebakiza muda mfupi wsitaafu.

Kumekuwa na tabia ya muda mrefu kwa viongozi wa nchi hii ya Tanzania kutokukemea au kuchukua hatua kwa viongozi wa namna hii, kutokana na viongozi wa juu kujihusisha na ulaji rushwa kunakowafanya kuwa waoga wa kukemea maovu yanayoendelea sehemu mbalimbali ambako kumeipelekea nchi kwa sasa kuwa na uhalifu wa hali ya juu na kama tulivyoona kwenye bandari zetu,tanesco na hata viwanja vya ndege nchini kufikia kuwa HUBs za kupitisha madawa ya kulevya na pembe za ndovu.

Mh waziri mwenye dhamana na Bodi hiyo, jaribu kufuatilia yale yanayosemwa na uchukue hatua kali ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wafanyakazi ili upate ukweli kutokana na wale unaowatuma kuchunguza wanazibwa midomo na fedha wanazopewa na Bw Bitegeko kwa niaba ya Bw Kumburu, Na kama huamini na kama unadhani tunakutania ipo siku utamgundua

Kwa urahisi tu Mh Waziri ni mara ngapi yamekuwa yakisikika toka kwa viongozi hao wakiwa mtaani kuwa waziri unajenga kiwanda cha kusindika vyakula kwenye wilaya fulani mkoani Shinyanga na kwamba support waliokupa sio ndogo hivyo huwezi kuwageuka kwenye maovu wanayoyafanya ikiwa ni pamoja na ulaji wa fedha za wakulima na zile za Halimashauri za wilaya.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge LAAC (Local Authority Accounting Committee) Mh Rajabu Mbarook Mohamed unaombwa kufanya uchunguzi kwa hili.Hasa halimashauri za mikoa ya kusini Mbeya na Mbinga na sehemu nyingine za kasikazini hasa huko Karatu na kwingineko.

Akiwa anaendelea kuajiri wafanyakazi wapya kwenye bodi hiyo na wengi wao wakiwa ni ndugu zake,au wana mahusiano fulani na yeye au Primus,inasemekana ajira hizo amezifanya bila ya kupata kibali toka serikalini,amesikika akisema anafanya hivyo kuziba mapengo ya wale aliowafukuza au anaotaka kuwafukuza, kama Moses Simingwa ambae ni afisa Mwajiri ambae kichwani hata hivyo hakuna kitu (mwizi wa kugushi).

Pia ikumbukwe kwamba bw,Kumburu alimfukuza mfanyakazi ambaye alikuwa mgonjwa na akafukuzwa kazi akiwa hosptalini akifanyiwa upasuaji,akidai mfanyakazi huyo kajitungia ugonjwa,kitendo hicho kilichowasikitisha wafanyakazi wengi kutokana na aina ya mauaji aliyotaka kufanyiwa mfanyakazi huyo na huku waziri mwenye dhamana akiwa analifahamu hilo kutokana na kuelezwa na bodi iliyopita, lakini amefumba macho na masikio bila hata kujali.

Inasemekana mfanyakazi huyo tayari alishafungua mashitaka mahakamani na kesi inaendelea.Hata hivyo Bw Kumburu alisikika akisema hata kama mfanyakazi huyo akishinda kesi watakata rufaa ili kuhakikisha anatesekea huko mahakamani kama kifo kimeshindikana basi atkuwa kama wale wengine waliopo mahakamani.

Kumburu ni mtu wa namna gani kama anavyoelezea mzee Ngeze aliyekuwa Mwenyekiti.Acha kuwa mbishi.

Ni hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Pius Ngeze alisikika akisema kuwa sasa hivi ndio amemjua Kumburu vizuri na kwamba DG huyo ndiye aliyemharibia sifa za uongozi wake alipokuwepo kwenye Bodi hiyo mpaka kusababisha bodi yake kuvunjwa na kwamba amekuja kushtuka kuwa ni mtu hatari sana na mtu asipokuwa makini na Kumburu unaweza kujikuta umewekwa ndani na au hata kukuharibia jina na sifa.

Nukuu. Huyo Kumburu ni mtu hatari sana na usipomjua vizuri anaweza kukuharibia sana na hata ikiwezekana unaweza kwenda ndani,ni mtu anaependa kutegeshea wakubwa zake vitu ambavyo sio sahihi na kwamba yeyote anaefanya nae kazi anatakiwa kuwa makini sana,alipoulizwa kuhusu fedha za wakulima zinazoliwa kupitia njia ya Exchange Rate alikiri na kusema hilo ni la kweli na wakati akiwa Mweyekiti Kumburu alimwambia ndio utaratibu wa bodi kufanya hivyo kama ilivyoagizwa na serikali.

Alipoulizwa kama na yeye alikuwa ni mdau kwenye ulaji huo alikataa ila akasema yeye alikuwa akiwekewa fedha kwenye A/c yake na alipouliza aliambiwa ni fungu lake la entertainment.

Katika hali ya kushangaza ni pale ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mama Sinare aliyechaguliwa kuiongoza bodi hiyo mapema mwezi March 2013 alipoamua kuachia ngazi mwezi December 2013 kwa kushindwa kufanya kazi na Kumburu, huku akiwa anamweleza waziri mwenye dhamana na bodi hiyo yale yanayoendelea kwenye bodi hiyo Kama kubadilisha minutes za vikao vya Bodi na kuweka anachotaka yeye Kumburu. Ilimbidi mama huyo kuweka mashine ya kurekodi vikao vyote ili kuwa na ushahidi wa kutosha.

Cha kushangaza ni pale waziri bila ya kufanyia kazi yale aliyoelezwa na mama huyo, inasemakena waziri alimwita Mama huyo na kumwambia ni bora uachie ngazi kupisha wanasiasa (Mhe. Zambi ambaye ni Mbunge wa Mbozi na Mfanya biashara wa Kahawa pia akishirikiana na Kumburu) wasipige kelele bungeni.kitendo kilchoshangaza wengi na kuibua utata mkubwa.

Mama huyo kwa kuwa ni kiongozi wa kweli na asiependa rushwa,wizi na unyanyaswaji wa haki za mwandamu alimwandikia Rais barua ya kuomba kujiuzulu na kupisha wajanja waendelee na ulaji wao.Inasemekana mojawapo ya swali alilotaka kujua ni utaratibu wa mahesabu yanavyokwenda na hasa hilo la fedha za wakulima kutokana na exchange rate na utaratibu wa fedha zinazopelekwa kwenye halimashauri.

Hiyo ndio Bodi ya Kahawa Tanzania katika kumsaidia mkulima, Bado tuna mengi ya kuweka hapa hivyo msiwe mbali tutaendelea.
 
Haya yule Mkurugenzi wa utawala wa Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika kaingia kwenye bodi hii na anaonekana kama vile katumwa na waziri kuja kuangalia yanayojiri kwenye bodi hiyo hasa swala la mishahara ya wafanyakazi lakini cha kujiuliza ni je atafanya kazi ya kweli au atamwagiwa hela na Kumburu / Bitegeko aende zake USANII MTUPUuuuuu
 
Mkuu, hapa chini una uhakika napo??

Katika hali ya kushangaza ni pale ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mama Sinare aliyechaguliwa kuiongoza bodi hiyo mapema mwezi March 2013 alipoamua kuachia ngazi mwezi December 2013 kwa kushindwa kufanya kazi na Kumburu, huku akiwa anamweleza waziri mwenye dhamana na bodi hiyo yale yanayoendelea kwenye bodi hiyo Kama kubadilisha minutes za vikao vya Bodi na kuweka anachotaka yeye Kumburu.
 
"Cha kushangaza ni pale waziri bila ya kufanyia kazi yale aliyoelezwa na mama huyo, inasemakena waziri alimwita Mama huyo na kumwambia ni bora uachie ngazi kupisha wanasiasa (Mhe. Zambi ambaye ni Mbunge wa Mbozi na Mfanya biashara wa Kahawa pia akishirikiana na Kumburu) wasipige kelele bungeni.kitendo kilchoshangaza wengi na kuibua utata mkubwa"

Huyu Zambi si ndiyo yule mbunge toka Mbozi ambae Mheshimiwa Kafulila alimtaja bungeni kuwa alishuhudia wakati anaomba rishwa toka kwenye halmashauri wakati akiwa mwanakamati ya Local government!!! Hata hivyo juu ya ufisadi wake ccm bila aibu imempa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Mbeya; maajabu haya yanaweza tokea Tanzania tu ambapo wezi waliodhihilika wanazawadiwa vyeo!!!
 
hatutashangaa kumburu naye akiweka rehani jengo la bodi ya kahawa kwa mnaufaa yke binafsi kama alivyofanya Leslie Omar,tunashukuru mahakama ilimtendea haki,funzo kwa kina kumburu,Bitegeko na Primus
 
Mwenyekiti Juma Ngasongwa kuwa makini na watu hao ni hatari kubwa.Ogopa sana mtu ambae haoni haya kukuharibia jina lako kwa kukudanganya ili mambo yake ya ulaji yaendelee na kuwatesa wafanyakazi wa bodi hiyo usisahau ni mkabila sana. Simamia sheria na haki na pia ujue umezaa visasi visiende kwa uzao wako kwa namna moja au nyingine

Jaribu kufikiria kwa nini mzee Ngeze hakutoka kwa usalama na mama Sinare kukimbia huyo jamaa ni hatari wa kutegesha vitu na kukupa hela ambazo hazieleweki na kukupa zawadi za kwenda shopping ulaya kama alivyosema mchangiaji hapo juu Bulesi kuwa Tanzania ni nchi pekee inayowazawadia wahalifu madaraka

Kuwa kama viongozi hawa Mwakyembe na Magufuli. Okoa nchi yako okoa Bodi ya Kahawa inapelekwa kwa wazungu bila wachache kujua kuwa mtu wa kuheshimika waachie bodi yao waendelee utaondoka na heshima kubwa na usikubali kurubuniwa kama Ngeze ambaye ameshtuka kiza kishaingia

Kwa ushauri tu Kumburu anataka kuhakikisha yeye ndio Mwenyekiti na wewe na rubber stamp tu hapo usikubali rudisha heshima yako mahali pake
 
Habari zilizotolewa hapa sio za uongo ni za kweli kwani ni kipi ambacho kimeandikwa hapa ambacho ni cha uzushi ?

Kwani uongo kuwa hawajagushi Scheme of service ? na kama ni uongo kwanini wizara imemwadikia Kumburu barua ya kujieleza na kwanini Scheme hiyo imepigwa mhuri wa wizara uliondikwa TREASURY REGISTRY MINISTRY OF FINANCE AND ECONOMIC AFFAIR bila sahihi yoyote ? wizi mkubwa sana huu uliofanywa na Kumburu na Bitegeko.
Kwani ni uzushi fedha za wakulima haziliwi kwa kupitia Exchange rate ? na kama ni uongo wathibitishe hapa
Kwani ni uzushi kuwa Bitegeko hawanii na kusali kila siku kuomba apate nafasi hiyo ya UDG yeye pamoja na Primus?
Kwani uzushi kuwa Bitegeko hauzi magari yake na magari mengine yameshafika na yapo bandarini huku akiwa kanunua gari dogo toka mfanyakazi mwenzake ?
Kwani ni uzushi kuwa Goodluck hakuwahi kuiba CRU na kusamehewa?
Kwani ni uzushi kuwa Goodluck Mushi anajenga ghorofa na kwani uongo kuwa ana wake lukuki ?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu hajawahi kutamba kuwa waziri kamweka mfukoni kwa kuwa amemsaidia hela za ujenzi wa kiwanda chake huko Shinyanga ?
Kwani ni uongo hawakumfukuza mfanyakazi aliyekuwa anaumwa na kulazwa hosptali ya KCMC na kufanyiwa operation ya tumbo ?
Kwani ni uongo Bitegeko,Goodluck na Kumburu hawali fedha za halimashauri ?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu anataka kufukuza watu wa kabla flani kwenye bodi hiyo wote ?
Kwani ni uongo kuwa Bite sio mzee totoz mjini Moshi kuna asiyejua hillo?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu hataki ubunge Mbinga kwenda kushndana na kati ya Kayombo au Komba?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu anakabidhi bodi kwa wazungu ?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu hajaandika barua kwa waziri kuomba aongezewe muda wa kukaa hapo ?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu kupitia mgongo wa bodi anaanzisha soko lake China la kuuza kahawa na wazungu ?
Kwani ni uongo wafanyakazi hawanyayaswi kwa level ya juu kabisa ?
Kwani ni uongo kuwa Kumburu hajawaajiri ndugu zake wa kutosha kwenye bodi hiyo ?
Kwani ni uongo vitasa vya milango havijawekwa vya namba ?
Kwani ni uongo Mama Sinare hakuitwa na waziri akaambiwa aachie ngazi kupisha wanasiasa wasipige kelele ?
Kwani ni uongo kuwa Ngeze hakupigwa chini shauri ya uongozi mbovu aliokuwa nao ?

Na kwanini wanababaika walifiri wanayoyafanya ni siri ? tunayatayarisha vitu muhimu na tutavipandisha hapa mapema sana
 
Duuh hii kali, naona mkuu umeamua kutoa hoja na kuijadili mwenyewe, ama kweli bodi na hao jamaa zako wamekuudhi sana.

Sasa maoni yako ni nini? au utaishia kulalamika tuu humu JF?? scheme of service imbeadilishwa na inaweza kula kwako, watu wanapiga hela za wakulima na halmashauri nini kifanyike? hebu funguka ueleweke ili hata kama ni msaada upate
 
Adolph kumburu mweleze PHYSICS CHEMISTRY,MATHEMATICS, bending moments ,shear forces,redundant members!

Mulianzaje kumpa kahawa?
Kumburu kunywa yooote!
 
Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Adolph Kumburu azidi kuonyesha vituko

Hali si swari ndani ya Bodi ya kahawa nchini (TCB) ambako mambo ya kushangaza na kusikitisha,yanazidi kuibuka kila uchao yanayoambatana na matumizi mabaya ya mali za bodi huku Waziri mwenye dhamana akiendelea kufumbia macho uozo unaoendelea ndani ya bodi hiyo ambayo ndiyo mboni ya jicho la mkulima wa zao la kahawa nchini.

Inasikitisha kuona kwamba mkurugenzi wa bodi hiyo ambaye amebakiza wiki takribani 5 mkataba wake wa ajira ya miaka mitano umalizike,hadi sasa amekaa kimya bila kutoa taarifa kwa bodi ya wakurugenzi yenye mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya kahawa,cha kushangaza ameiruka bodi ya wakurugenzi na kumwandikia waziri moja kwa moja kumwomba waziri ambae ni swahiba wake amwongezee mkataba.
Anachokifanya kwa sasa Bw Kumburu ni kusubiri kuona kama waziri atatoa maamuzi ya kukubali barua yake ya maombi ya kutaka kuendelea na uongozi wa kuua bodi hiyo na kuikabidhi kwa wazungu.

Kwa sasa mkurugenzi huyo mkuu Adolph Kumburu bila ya kuelewa anachokifanya ameonekana akitaka kuondoka na wafanyakazi wote ikiwa ni pamoja na yeye bila kujijua. Ameonekana akitoa Scheme of Service ya shirika hilo ikiwa imetayarishwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw A.Bitegeko (a.k.a Mzee wa mademu mjini Moshi kutokana na hela apatazo ni nyingi sana hasa za exchange rate za dola za wakulima na zabuni za shirika na zile za halimashauri za Wilaya) ambaye nae ni kati ya wale wanao wania kiti hicho kwa hamu kubwa kama vile kiti hicho ni cha kurithishana.

Bitegeko amekuwa akijifanya ni rafiki mkubwa wa Bw Kumburu (tumewahi kusikia kuwa huko NSSF alikotokea hakutoka salama baada ya kugushi zaidi ya Sh Mln.20. na ndio maana alikimbia mapema akisaidiwa na aliyekuwa waziri wa fedha wakati huo Mh Mstapha Mkullo).Na ndipo kutokana na baba yake kuwa rafiki na aliyekuwa Mwenyekiti wakati huo Pius Ngeze na ndiye aliyemsaidia kupata kazi kwenye bodi hiyo bila vikwazo na kumwacha aliyekuwa ameshinda nafasi hiyo (interview)

Ameshasikika akitamba mara kwa mara kama ambavyo anavyotamba hivi sasa kuwa naibu waziri Kighoma Malima ni mtu wake wa karibu sana hivyo hakuna shida yoyote,U-DG lazima aupate kwa kuwa naibu waziri huyo ameshamwahidi kuwa atamsaidia kwa hilo,alisikika na kurekodiwa Bw Bitegeko.(Sehemu ya recording hiyo iliyorekodiwa na mmoja wa makahaba wake wa mtaani tutaiweka hapa siku za usoni).

Bw,Bitegeko akiwa ameagiza magari mazuri ya bei mbaya, amekuwa akitangaza kuuza magari yake mawili aliyonayo ili aweze kuudanganya umma.

Ni Bw Bitegeko ambaye katengeneza scheme of service akionyesha ya kuwa kila mfanyakazi wa bodi hiyo anatakiwa kuwa na Master's degree,huku akijua wazi kuwa DG wake Kumburu hana Master's degree na kwamba huyo Bw Kumburu ana kadegree kamoja alikokapata UDSM ka introduction ya Engineering.

Bw Bitegeko anawachezea shera kwa kuwa anajua vizuri kabisa kuwa kulingana na scheme aliyoipitisha kwa kuhonga inamuengua rafiki yake bandia na hivyo kubaki na mpinzani wake kwenye kiti hicho Bw Primusi Kimariyo ambaye naye hana vigezo vya kumtisha kwa kuwa naye ana MBA kama yeye. Anamwona Primusi pia kuwa hafai kutokana na utendaji wake wa kubabaisha hasa kwenye kuwasababishia wakulima hasara wakati wa kutoa bei elekezi zisizo za kweli.

Bitegeko pamoja na kuwa na vigezo vya kuwaengua wenzake bado anazo dosari nyingi ambazo wanashirikiana na Bw Kumburu hasa za kuwaibia wakulima hela zao kupitia exchange rate na fedha za halimashauri za wilaya Kahawa zitokapo hasa Kusini mwa nchi.

Hili hufanywa na mastermind wao Bw Goodluck Moshi ambae nae huko nyuma aliwahi kutuhumiwa na utawala uliopita kwa wizi wa hela za mauzo ya kahawa kwenye kitengo cha kukaanga na kuuza kahawa CRU kilichopo mjini Moshi,na kukiri kwa maandishi na alipoonewa huruma na uongozi uliopita ilibidi ahamishiwe Bukoba ili kuficha uovu huo (yaleyale ya kitanzania).

Hivi sasa Bw Goodluck Moshi toka arudishwe makao makuu ya bodi mjini Moshi kutoka Bukoba na Bw Kumburu na akishirikiana na Bw Bitegeko ameweza kujenga nyumba kadhaa kwa ajili ya wake zake lukuki alionao na hivi sasa anamalizia Ghorofa lake la kifahari mjini Moshi.Wakati Bw Bitegeko anajenga yak wake Mjini Morogoro.

Wizi wa fedha za Halimashauri za wilaya wanazokula ni zile wanazozituma kwenye halimashauri husika baada ya kuzikata kwenye mauzo ya kahawa za wakulima au PCB.Fedha hizi wanapozituma huzituma kimakosa makusudi, baadae fedha hizo zinarudishwa kwenye mfumo wa cash na hapo zinaporudi ndipo kazi inapofanyikia.

Kitendo cha halimashauri husika kuomba bodi ya kahawa kuwakusanyia fedha za ushuru toka kwenye mauzo ya kahawa za wakulima au wale wanaoitwa coffee buyers ndio ilikuwa utaratibu wa watu fulani kwenye wilaya hizo kuzitafuna fedha hizo wakishirikiana na wezi wa bodi hiyo,

Hii ilikuwa ni akili ya hali ya juu sana waliyotumia kufanikisha hili na mpaka sasa inasemekana ni kiasi cha Tsh 500 milioni zimeshaliwa kwa kipindi cha misimu miwili tu bila hata wakaguzi wa ndani kujua hilo.Hawa jamaa walipoona kuna wajanja ambao wamegundua hili wajanja hao walihamishwa haraka sana na kukimbizwa mikoani Mbeya na Bukoba ili wasione tena.

Viongozi hao ambao ni Bw Adolph Kumburu,Asteri Bitegeko na Primus Kimaryo wanaongoza shirika hilo kwa kuwanyayasa wafanyakazi wa bodi hiyo kwa kiwango kikubwa sana.Kutokana na wafanyakazi hao kushindwa kupeleka malalamiko yao kwa menejimenti ambayo ni wao wao imewabidi kumwandikia barua Waziri lakini pia huko kwa waziri zinagonga ukuta kutokana na waziri akihitaji kupata maelezo ya kina kunatokea mizengwe mingi kwa wale wanaotumwa na wakiondoka ndipo Kumburu anamwandikia waziri barua zenye uongo wa kutisha huku akimweleza waziri kuwa maswala hayo anamuomba amwachie kwamba menejimenti inayashuhulikia na hapo ndipo pia inasemekana majibu hayo huwa yanaambatana na bahasha nono za kumziba waziri huyo pamoja na naibu wake mdomo.

Hivi sasa wameibua jambo la kushangaza kwa kubadilisha vitasa vya milango ya ofisi zao kwa kuweka vitasa vya kufunga kwa namba (code) kitendo kilichoshangaza wengi kwa kuwa hata ofisi ya waziri mwenye dhamana haina vitasa hivyo vya namba na kufanya ofisi zao kuwa kama milango ya benki na safe zake za kuweka hela.

Wafanyakazi wanajiuliza hivi siku hizi kahawa inauzwa kwa cash au vipi! Waziri mwenye dhamana haya yote huyaelewi ?.

Kutokana na ubabe unaoendelea bila ya kutokea hata mmoja wa kiongozi ngazi ya juu serikalini kuukemea,imewafanya Wafanyakazi wa bodi hiyo kuoonekana kuwa wanyonge kutokana na hilo na wengi wao wamesikika wakisema wanamwachia Mungu.

Bodi ya kahawa kwa sasa inaonekana kama Shirika la ajabu na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuokoa jahazi, linaweza kuipa serikali mzigo mkubwa siku za usoni kutokana na kutakiwa kuajiri wafanyakazi wapya wenye Masters pekee.Kumburu yeye anasema hataguswa kwa vile pamoja na kuwa na kadigirii kamoja pekee anasema yeye anateuliwa na waziri rafiki yake na Injinia mwenzake hivyo atamfumbia macho. Degree aliyonayo Bw Kumburu inaruhusu fundi Mchundo huyo kufanya kazi kwenye viwanda vya kusaga mahindi vijijini pekee.

Ili kuhakikisha anaongezewa mkataba Kumburu amekuwa akiwaandama wale wenye Masters za Kilimo na wale wenye Masters za Engineering akiwaona wao ndio tishio kwake,

Bila kujua Bitegeko na Primus hawako nae kwa kuwa wanajua hana vigezo hivyo wako wakiomba Mungu ni lini atatoka hapo ili mmoja wao akamate usukani. .

Habari za ndani kabisa zimebaini kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wa Bodi hiyo wameomba nafasi ya kumwona Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa na vielelezo vya kutosha,ikiwa ni pamoja na jinsi fedha za wakulima zilinavyoliwa hii ni kutokana na Waziri mwenye dhamana kufumbia macho hayo yanayoendelea amesikika mfanyakazi mmoja akisema wacha iwe mbaya wamechoka.Na ikishindikana hapo kwa raisi basi watapeleka nyaraka hizo upinzani ili kila kitu kianikwe adharani.

Hata hivyo Bw Kumburu katika hali nyingine ya kushangaza ni pale alipokataa kuwalipa wafanyakazi waliostaafu kazi mafao yao akisingizia kuwa Wizara/serikali ndio iliyokataa wasiwalipe wafanyakazi hao na kusababisha wafanyakazi hao kukimbilia mahakani na mpaka sasa hivi kesi inaendelea mahakamani.

Lakini katika hali nyingine ya kushangaza zaidi ni pale ambapo yeye Kumburu baada ya kusema serikali/wizara imekataa wanaostaafu wasilipwe mafao yao yeye binafsi kwa kuwa ameshikilia mpini na kwa kuwa muda wake wa mkataba unaishia amejiwekea yeye binafsi mafao yake yasiyopungua Tsh 60 milioni kwenye bajeti ambayo anasubiri bodi ya wakurugenzi ije kuyapitisha na kuacha wengi kumshangaa mtu huyo alivyo mnyama na asivyo mwanadamu kujiwekea mafao yake huku akikataa kuwalipa wengine.

Inasikitisha anavyoshindwa kuongoza shirika lenye wafanyakazi wasiozidi 100 na huku akisikika kuwa anajitayarisha kwenda kugombea Ubunge huko kwao Mbinga kumwondoa Mh Capt Komba au Mh Kayumbo.

Yote haya waziri mwenye dhamana na bodi hii akiwa amefumbia macho bila hata ya huruma.Imagine mtu kafanya kazi miaka yake yote halafu anastaafu Kumburu na washirika wake Bitegeko na Primus wanakataa kuwalipa. Wamama hao ambao wengi wao ni wajane wamebaki wakisema wanamwachia Mola

Ni hivi karibuni mnamo tarehe 15/8/2013 Bw Kumburu akiwa kwenye kikao na wafanyakazi wa bodi hiyo alidhubutu kusema kuwa, hata kama yeye hana Masters degeree hakuna wa kumuuliza wala kumchunguza kwa hilo kwa kuwa waziri ndiye anaemtabua na kwamba kama kuna mtu analalamika kuhusu scheme of service anaweza kuacha kazi mwenyewe na kwamba sio lazima wanaolalamika kufanya kazi kwenye bodi hiyo wala hakuna mwenye hisa kwenye bodi hiyo.Kwamba yeye kama yeye hawezi kutotekeleza wajibu wa serikali kama ilivyoagiza. Sasa hapa sijui yeye ana hisa ngapi kwenye shirika hilo.

Hakuna asiyefahamu kuwa Bodi ndio zinazotayarisha scheme of service na kupeleka serikalini ili zikapitishwe na sio serikali ndio inyozitayarishia bodi za mazao scheme of service bodi hizo.Aaache kufanya watu watoto wadogo.

Serikali inatakiwa iingilie kati kumaliza migogoro ndani ya Bodi inayoletwa na vita vya madaraka kwa kutomwongezea Kumburu Mkataba na kumtafuta DG mwenye sifa arudishe heshima ya Bodi na atakaye heshimu uzoefu na michango ya wafanyakazi ambao wengi wao wamebakiza muda mfupi wsitaafu.

Kumekuwa na tabia ya muda mrefu kwa viongozi wa nchi hii ya Tanzania kutokukemea au kuchukua hatua kwa viongozi wa namna hii, kutokana na viongozi wa juu kujihusisha na ulaji rushwa kunakowafanya kuwa waoga wa kukemea maovu yanayoendelea sehemu mbalimbali ambako kumeipelekea nchi kwa sasa kuwa na uhalifu wa hali ya juu na kama tulivyoona kwenye bandari zetu,tanesco na hata viwanja vya ndege nchini kufikia kuwa HUBs za kupitisha madawa ya kulevya na pembe za ndovu.

Mh waziri mwenye dhamana na Bodi hiyo, jaribu kufuatilia yale yanayosemwa na uchukue hatua kali ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wafanyakazi ili upate ukweli kutokana na wale unaowatuma kuchunguza wanazibwa midomo na fedha wanazopewa na Bw Bitegeko kwa niaba ya Bw Kumburu, Na kama huamini na kama unadhani tunakutania ipo siku utamgundua

Kwa urahisi tu Mh Waziri ni mara ngapi yamekuwa yakisikika toka kwa viongozi hao wakiwa mtaani kuwa waziri unajenga kiwanda cha kusindika vyakula kwenye wilaya fulani mkoani Shinyanga na kwamba support waliokupa sio ndogo hivyo huwezi kuwageuka kwenye maovu wanayoyafanya ikiwa ni pamoja na ulaji wa fedha za wakulima na zile za Halimashauri za wilaya.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge LAAC (Local Authority Accounting Committee) Mh Rajabu Mbarook Mohamed unaombwa kufanya uchunguzi kwa hili.Hasa halimashauri za mikoa ya kusini Mbeya na Mbinga na sehemu nyingine za kasikazini hasa huko Karatu na kwingineko.

Akiwa anaendelea kuajiri wafanyakazi wapya kwenye bodi hiyo na wengi wao wakiwa ni ndugu zake,au wana mahusiano fulani na yeye au Primus,inasemekana ajira hizo amezifanya bila ya kupata kibali toka serikalini,amesikika akisema anafanya hivyo kuziba mapengo ya wale aliowafukuza au anaotaka kuwafukuza, kama Moses Simingwa ambae ni afisa Mwajiri ambae kichwani hata hivyo hakuna kitu (mwizi wa kugushi).

Pia ikumbukwe kwamba bw,Kumburu alimfukuza mfanyakazi ambaye alikuwa mgonjwa na akafukuzwa kazi akiwa hosptalini akifanyiwa upasuaji,akidai mfanyakazi huyo kajitungia ugonjwa,kitendo hicho kilichowasikitisha wafanyakazi wengi kutokana na aina ya mauaji aliyotaka kufanyiwa mfanyakazi huyo na huku waziri mwenye dhamana akiwa analifahamu hilo kutokana na kuelezwa na bodi iliyopita, lakini amefumba macho na masikio bila hata kujali.

Inasemekana mfanyakazi huyo tayari alishafungua mashitaka mahakamani na kesi inaendelea.Hata hivyo Bw Kumburu alisikika akisema hata kama mfanyakazi huyo akishinda kesi watakata rufaa ili kuhakikisha anatesekea huko mahakamani kama kifo kimeshindikana basi atkuwa kama wale wengine waliopo mahakamani.

Kumburu ni mtu wa namna gani kama anavyoelezea mzee Ngeze aliyekuwa Mwenyekiti.Acha kuwa mbishi.

Ni hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Pius Ngeze alisikika akisema kuwa sasa hivi ndio amemjua Kumburu vizuri na kwamba DG huyo ndiye aliyemharibia sifa za uongozi wake alipokuwepo kwenye Bodi hiyo mpaka kusababisha bodi yake kuvunjwa na kwamba amekuja kushtuka kuwa ni mtu hatari sana na mtu asipokuwa makini na Kumburu unaweza kujikuta umewekwa ndani na au hata kukuharibia jina na sifa.

Nukuu. Huyo Kumburu ni mtu hatari sana na usipomjua vizuri anaweza kukuharibia sana na hata ikiwezekana unaweza kwenda ndani,ni mtu anaependa kutegeshea wakubwa zake vitu ambavyo sio sahihi na kwamba yeyote anaefanya nae kazi anatakiwa kuwa makini sana,alipoulizwa kuhusu fedha za wakulima zinazoliwa kupitia njia ya Exchange Rate alikiri na kusema hilo ni la kweli na wakati akiwa Mweyekiti Kumburu alimwambia ndio utaratibu wa bodi kufanya hivyo kama ilivyoagizwa na serikali.

Alipoulizwa kama na yeye alikuwa ni mdau kwenye ulaji huo alikataa ila akasema yeye alikuwa akiwekewa fedha kwenye A/c yake na alipouliza aliambiwa ni fungu lake la entertainment.

Katika hali ya kushangaza ni pale ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mama Sinare aliyechaguliwa kuiongoza bodi hiyo mapema mwezi March 2013 alipoamua kuachia ngazi mwezi December 2013 kwa kushindwa kufanya kazi na Kumburu, huku akiwa anamweleza waziri mwenye dhamana na bodi hiyo yale yanayoendelea kwenye bodi hiyo Kama kubadilisha minutes za vikao vya Bodi na kuweka anachotaka yeye Kumburu. Ilimbidi mama huyo kuweka mashine ya kurekodi vikao vyote ili kuwa na ushahidi wa kutosha.

Cha kushangaza ni pale waziri bila ya kufanyia kazi yale aliyoelezwa na mama huyo, inasemakena waziri alimwita Mama huyo na kumwambia ni bora uachie ngazi kupisha wanasiasa (Mhe. Zambi ambaye ni Mbunge wa Mbozi na Mfanya biashara wa Kahawa pia akishirikiana na Kumburu) wasipige kelele bungeni.kitendo kilchoshangaza wengi na kuibua utata mkubwa.

Mama huyo kwa kuwa ni kiongozi wa kweli na asiependa rushwa,wizi na unyanyaswaji wa haki za mwandamu alimwandikia Rais barua ya kuomba kujiuzulu na kupisha wajanja waendelee na ulaji wao.Inasemekana mojawapo ya swali alilotaka kujua ni utaratibu wa mahesabu yanavyokwenda na hasa hilo la fedha za wakulima kutokana na exchange rate na utaratibu wa fedha zinazopelekwa kwenye halimashauri.

Hiyo ndio Bodi ya Kahawa Tanzania katika kumsaidia mkulima, Bado tuna mengi ya kuweka hapa hivyo msiwe mbali tutaendelea.

Pole sana ndugu inaonekana unaumia sana kuhusu hawa watu watatu
umejaribu kueleza mambo mengi sana nina imani wahusika watayafanyia kazi

ILA KUNA SEHEMU YA MAELEZO YAKO SIJARIDHIKA NAYO. NAYO YANASOMEKA HIVI [ana kadegree kamoja alikokapata UDSM ka introduction ya Engineering. hapa kwenye haya maneno ambayo kwenye maelezo yako nimeyaweka alama nyekundu inaonyesha hata wewe una shida[ NAOMBA UESHIMU UNAPOTAMKA "DEGREE"
unajua mtu anasoma muda gani? usirudie hata siku moja kuita "DEGREE" kadegree.
Ila kwa hayo mengine wahusika watayafanyia kazi
 
Haya makala yameandikwa kwa hisia na maslahi binafsi hata kama ndani yake yapo ya ukweli, aliyeandika ni wa ndani ya bodi ya kahawa na anatumika kuchafua bodi ya kahawa amabayo mwenyewe anafanyia kazi.
 
yaaa ni kweli mkuu kwanza kajiunga juzi juzi tu humu JF na post zake ni chache sana, jina katika avatar yake ni hao hao watuhumiwa (bitegeko), naona wamelizana mshiko jamaa kaamua kumwaga kila kitu. ndugu ulikuwa wapi ? siku zote , tuwe wazalendo wa hii nchi siyo majungu , ingawa habari hii ina ukweli kiasi wa maonevu
 
Tuna ushahidi wa kutosha kuhusu hili.Elias Temu amepata hasira baada ya kuletewa Mtu mwenye degree Kwenye kitengo chake.Elimu ya Temu ni ya kidato cha nne,failure.Baada Temu kuletewa huyo mtumishi tena wa muda aliangua Kilimo na kuzunguka Kwenye makorido ya Bodi ya kahawa akilalalamika.Hasira nyingine ya Ndugu Temu ni kutoongosewa mshahara Kwenye muundo mpya wa utumishi.Temu kwa ujinga wake anadai Mtu mwenye elimu ya kidato cha nne Kama yeye na aliyefanya Kasi miaka azidi ya ishirini Bodi ya kahawa Kama yeye,ni sawa sawa na Mtu mwenye degree!TCU mpo?sasa sisi tunamuambia,Kama ni hivyo akaombe kusoma masters Kwenye Chuo chote nchini aone Kama atakubaliwa.
 
Nimeona niingie kumtetea Elias Temu, ni kweli Kumburu alikuwa amemrubuni akamwamini akijua pengine wafanyakazi wanaoonewa wana makosa ila sasa ameshuhudia mwenyewe. Kitendo cha kujua ukweli akaanza vita ya kukemea maovu ni Mungu amemwangazia na hatuwezi kumulaumu. Tunamwomba Mungu na wengine ambao bado hayajawafika wasidhani wako salama kama hatatokea wa kumfunga kamba kichaa madhara atakayofanya ni makubwa.

Ona watu walivyo waajabu kiasi tunashangaa kama Mwalimu hakupoteza raslimali za taifa kuwasomesha, wanalaumu wanaoanika maovu yanayotendeka ndani ya Bodi eti wanachafua Bodi. Wanaochafua Bodi ni wale wanaotenda maovu. Kabla ya kuwalaumu wanaoanika maovu tunaiomba serikali ifuatilie yaliyondikwa ili wakikuta ni majungu ndipo watafutwe wanaoeneza majungu ya kuchafua Bodi.

Kinachoshangaza anayemshitaki Kumburu anageuziwa yeye mashitaka. Mathalani aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi mama Hawa Eva Sinare aliandika barua Ikulu akimlalamikia Kumburu kwa kitendo cha kubadilisha Minutes za mikutano ya Bodi, kinyume chake Kumburu akakimbilia kwenye Tume ya maadili ya viongozi kumshitaki Mwenyekiti kwa kosa ambalo tayari ameshitakiwa naye kuwa anamwingilia na anabadilisha minutes za Mikutano. Kumburu anatumia ujanja wa kizamani wa muhalifu kuwahi Polisi kufungua mashitaka. Hii si kwa Mwenyekiti pekee kwani kwa wafanyakazi ndio balaa anafanya makosa akiulizwa na Wizara anawageuzia kibao walio chini yake. Anaendesha Bodi kwa uwongo, fitina rushwa , upendeleo vitu ambavyo vinaweza vikathibitishwa kwa ushahidi au kwa mazingira kama rushwa.
Wafanyakazi wanajiuliza hata akitumia rushwa na uwongo(ambao huwa hataki uthibitishwe) akafanikiwa kuwafukuza, je yeye atadumu pale millele, je hajuhi siku akitoka ndani ya lile jengo na yeye atamfuata Omari jela. Aombe asimkute Omari kesha kuwa mzoeefu atamfanya kitu mbaya kwa vile ndiye aliyemchongea akafungwa. Hata kama Omari ana makosa ukilinganisha na ya Kumburu, Omari ni Malaika.
 
Back
Top Bottom