Mangimeli
JF-Expert Member
- Sep 15, 2011
- 1,151
- 286
Saidi mwemani mchaga acha kutuhadaaAcha uongo na chuki binafsi...namjua Dr. Hassan Mshinda personally kama rafiki na pia likuwa boss wangu!
Google profile ya Dr Hassan Mshinda halafu niambie kama katika 'top ten' ya scientist wa Tanzania hatakuwepo! He is a PhD holder, Malariologist, research guru, with hundreds of research publications in 'internationally accredited' journals. Ana awards nyingi tu katika uwanja wa research kutokana na kazi zake katika malaria.
Dr Mshinda hana undugu wowote na Saidi Mwema....Said Mwema ni mkwe're wa kutoka kijiji cha Mwetemo Bagamoyo (kati ya Kiwangwa na Msata), Dr Mshinda ni mNgazija toka Shelisheli (Seychelles), hapa Tanzania alihamia akasoma, akaoa, akazaa, na anafanya kazi brilliantly.
Utendaji kazi wa Dr Mshinda ulimvutia JK wakati alipokuja Mkurugenzi wa shirika la afya duniani (WHO) Dr Margareth Chang, Chang mwenyewe alisalute kazi kubwa iliyofanywa na Ifakara Health Institute chini ya Dr Mshinda akiwa mkurugenzi, kiasi kuna guidelines kadhaa za WHO zimekuwa developed kufuatia tafiti za IHI. Hata waziri wa Afya wa sasa Dr Hadji Mponda ametokea IHI naye akiwa na tafiti na publications nyingi tu za malaria.
Kama ana mapungufu mengine hapo COSTECH jaribu kujenga hoja kwa hayo...lakini usisingizie alibebwa kupewa post hiyo kwa uswahiba wa kuunga na gundi kwa JK.