Dr Hamis Kigwangala ahoji tatizo la ajira nchini

Itafika kipindi akifa MTU tutakuwa tunashangilia ... Mijitu kama hii ni kuishitakia kwa Mungu baba aliejuu ,Ajuae kesho yetu... Mungu tuondolee hizi takataka zinazoharibu ndoto na maisha yetu vijana

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
hajielewi huyo kigwangwala kama kujiajiri ni rahisi hivyo basi aachie uwaziri na ubunge ili akajiajili ajionee mwenyewe
 
Sasa si mmewachagua wenyewe na mtawachagua tena tulieni dawa iiingie...hakuna haja ya kumkandia kigwa...anasema ukweli tuache uvivu na kutegemea ajira pekee tubuni mbinu naimani kwenye wasomi hakikosekani kitu
 
Jamani wanaJF,

Kiukweli kati ya viongozi ambao sijawahi kumwelewa ni huyu anayejiita khamis Kigwangalla ,ni aina ya mwanasiasa anayependa kuishi kama celebrity na kujaribu kuwahadaa na kuwadanganya watu kwa falsafa zake ambazo hata yeye haziamini.

- Leo eti anashangaa vijana wengi kwenda kwenye usaili wa TRA ??
- Yaani baada ya utumishi kuwatesa watu kwa kuwatoa mbali huko kama KIGOMA na kuja kwenye usaili hapa Dar yeye hata hajui kama TATIZO LA AJIRA ni ZITO NCHI HII, sijui alipochukua fomu ya urais alimaanisha nini kama hata MATATIZO YA VIJANA hayajui ?
- Umeshindwa kuwasaidia hata vijana wanaohitimu vyuo vya afya kupata vyeti vya NACTE umebaki na DRAMA na DHIHAKA tu kwa vijana wa taifa hili wanaoteseka na JINAMIZI LA UKOSEFU WA AJIRA.
- Unaambiwa vijana wajiajiri, watajiajiri vipi wakati hawapewi TAX HOLIDAYS wala GRACE PERIODS. Gharama za usajili wa Makampuni kwa fresh graduates ni kubwa, hakuna benki inawaamini hata kwa mikopo, unataka wajiajiri vipi, wawe MACHINGA ili muwapige MABOMU ?
Si Kigwangalla si wewe hakuna kati yenu anajua kinacho endelea kuhusu ule usaili bali wote mmeongozwa na upepo tuu baada ya kuona picha..... Tatizo la ajira halijaanza leo na hao wanao onekana kwenye hiyo picha hiyo huwa wanakuwepo kila usaiili..kwa hiyo hilo si jambo jipya...
Halafu swala la pili ambalo hujui ni kwamba hakuna aliyetoka kigoma kuja kufanya usaili huo wa TRA dar bali ulio waona hapo Dar ni wenye anuani za makazi ya Dar na pwani na hawazidi 2000 mikoa mingine napo imefanyika na ni kila kanda...
Swala hapo ni tatizo la ajira si kuwatupia lawama utumishi.... sasa sijui mlitaka waitwe watu watatu?
Kwa hiyo huyo Kigwangalla ana shida kubwa kichwani...
 
Sasa si mmewachagua wenyewe na mtawachagua tena tulieni dawa iiingie...hakuna haja ya kumkandia kigwa...anasema ukweli tuache uvivu na kutegemea ajira pekee tubuni mbinu naimani kwenye wasomi hakikosekani kitu
Hapa tunazungumzia NDOTO, DESTINY na FUTURE za VIJANA wa taifa hili. Masuala ya uchaguzi yana mambo mengi, kuna watu wanachaguliwa kwa MIHEMKO tu wala hawajawahi kuwa na msaada kwa taifa hili
 
Anashindwa kushangaa hospitali na vituo vya afya vina uhaba mkubwa sana wa wafanyakazi ilihali mtaani kuna watumishi zaidi ya 20,000 wa kada y afya hawajaajiliwa? Na yeye ndo mshauri wa Raisi, kama mshauri wa Raisi anashangaa je sisi wengine tufanyaje sasa?
 
Hakuna kiongozi mwenye MIKAKATI yoyote ya kuwaokoa VIJANA wa Taifa hili. Zilizopo ni SIASA na POROJO hakuna msaada wowote, ukisema uwe MACHINGA unapigwa mabomu

Kwa sababu wote wanajua utakapo mpo uwezo masikini atapata akili na atakuwa na kiuchumi na uwezo mzuri na si rahisi kumrubuni.

Leo ikifika wakati wa uchaguzi Mama anapewa kilo ya sukari au paketi ya chumvi ili amchague muwakilishi wake bungeni unaenda kuwapata akina Bajaji,wale watoto pumbavu wa wabunge waliorithishwa nafasi,akina Musukuma na kaliba ya akina Musukuma halafu unafikiria Tanzania itapata Maendeleo.

Labda CCM wote waondoke duniani maana akibaki hata mmoja Tanzania haitanusurika kamwe
 
Back
Top Bottom