DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

Wakuu kwa maamuzi haya ya kuwalipa IPTL hayo mabilioni ya pesa,nilikuwa nauliza uhalali wa kesi inayoendelea ya wakina Shose Sinare na Sioi Sumari maana kama sikosei inahusiana na hili swala.
 
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...
Mkuu heshima kwako,
Hilo lipo juu ya uwezo wa DPP kuamua..... Ni vyema ungesema ukweli... Mzigo mzito huu..... Na Ni mtihani Mkubwa kwa "Mtukufu"
Kama ya Lugumi yalikwama haya yatawezekana kweli?
 
Kwa taarifa yako watakanyaga wote kama watuhumiwa wa kesi 2 tofauti.
Naona hujui mambo kabisaa ile ya mwakyembe lilikuwa ni zengwe ndiyo maana walipoambiwa watoe ushaidi bungeni yule mbunge alibakii anabung'aa tuuh yeye kasoma kwenye gazeti linalomilikiwa na mbaya wa mwakyembe akaenda pupapupa kama vile alikuwa kwenye mgahawa!!!
 
Masikofu walituambia ni chaguo la Mungu Mungu atalipa Hilo deni
 
We want a
Mzee mwanakijiji umetoka speed kwenye ule uzi umeamua kuanzisha wakwako kabisa. kwa taarifa yako kwenye hili la IPTL hapo ndio utajua ili hadithi unayoaminishwa kwamba watu wanapambana na mafisadi basi ni vidagaa tu ndio wanaobanwa. Muda ndio utasema.
We want actions not stories. Matapeli na wezi hao lazima wakamatwe na wawe prosecuted. Na accounts na mali zao zikamatwe ili kulipa deni hili.
 
Masikofu walituambia ni chaguo la Mungu Mungu atalipa Hilo deni
Maaskofu waliopata mgao huo nao wahojiwe, walipata mgao huo baada ya kuwa wamefanya kazi gani? Loss of moral authority of th clergy.
 
ISHU HII BABA NANI ANAICHUNGULIA KWA MBALI,NA HATOIGUSA .......NGUMU KUMEZA HII

OVA
 
ISHU HII BABA NANI ANAICHUNGULIA KWA MBALI,NA HATOIGUSA .......NGUMU KUMEZA HII

OVA
Serikali ya awamu ya 4 kwakujua kabisa walijipa "ukipofu" wa kutofanya due dilligence ya kutosha juu ya uhalali wa wanaolipwa pesa hizo toka Tegeta Escrow account. Kisheria this unethical and illegal act was done maliciouslly, with full knowledge. Hii kesi tumeshindwa kihalali. Tatizo hili tumelitengeneza wenyewe kwa makusudi.
 
Mkuu heshima kwako,
Hilo lipo juu ya uwezo wa DPP kuamua..... Ni vyema ungesema ukweli... Mzigo mzito huu..... Na Ni mtihani Mkubwa kwa "Mtukufu"
Kama ya Lugumi yalikwama haya yatawezekana kweli?

Na yakiwezekana utaamua kuhamisha goli tena?
 
Waliyotengeneza si ndiyo hao vigogo wetu mkuu....kwanini wasitwishwe huu mzigo wao..

Ova
Serikali ya awamu ya 4 kwakujua kabisa walijipa "ukipofu" wa kutofanya due dilligence ya kutosha juu ya uhalali wa wanaolipwa pesa hizo toka Tegeta Escrow account. Kisheria this unethical and illegal act was done maliciouslly, with full knowledge. Hii kesi tumeshindwa kihalali. Tatizo hili tumelitengeneza wenyewe kwa makusudi.
 
Masikini Mwanakijiji, hicho kitendawili cha Esrow bora usingekizungumzia maana hakuna 'aliye huko' asiyehusika nacho. Ikiwa Kikwete alisema fedha za Escrew si za serikali unataka aliyemkabidhi kijiti asemeje. Mbona unamjaribu? Unampa jukumu ambalo akilishindwa tumwone hafai? Unawezaje kufikiria kumdhalilisha kiongozi kwa kiwango hicho? Au uvumilivu umekushinda? Usitukumbushe ya Escrew wakubwa wetu walishatuambia hela hazikuwa za kwetu basi. Nakama waliochukua hela zetu wanataka tuwalipe zingine watafutiwe wapewe. Ugomvi wa nini? Kama kweli unataka wahujumu washughulikiwe subiri mahakama ya wahujumu uchumi itawashughulikia wote. Hizi mahakama ndogo ndogo haziwezi.
 
Kama Magu atataka kujaribu kuicheza hii ngoma ya IPTL basi awape huo uwanja UKAWA, aruhusu tu wafanye siasa zao kwa uhuru, kwa gear hiyo ataweza kupenya na kupambana na IPTL.

Tofauti na hapo, ataishia kujikaanga kwa mafuta yake.

Mfanye siasa kama zile za Mwembeyanga na List of shame?
 
Suala la kushugulikia mafisadi haiitaji haraka kama unavofikiria ni suala la kisayansi ambapo ushaidi wa kutosha unaandaliwa nakuaminisha hili ni suala Dogo kwa MAGUFULI stay tune!!!
Ni dogo kwa MAGUFULI? Usinichekeshe wewe dogo...!

Kama ilivyokuwa kwa Lugumi, nyumba za serikali, kivuko chakavu na mengine mengi. Unalosahau kijana ni kwamba na yeye wako watu wanazo faili zake...akimwaga tu mboga na wao wanamwaga ugali, hapo sasa.

Magufuli amekuwa sehemu ya serikali hiyo hiyo kwa zaidi ya miaka 20 akiwa Waziri, hakuna namna ya kumtenganisha na wale aliokuwa akishirikina nao katika maamuzi yote yaliyochukuliwa na serikali kiutendaji na kiutekelezaji.

Nawahurumia mnaodanganyika kuwa mtukufu mikono yake ni misafi, hilo linawezekanaje wakati alikuwa anaishi nao na kukaa nao? Kumbuka kutwaa Uraisi hakumbadilishi mtu, kunafichua tu tabia halisi ya mtu alivyo.
 
Ila mm hii ishu ya ESCROW huwa inanichanganya sana. Yaani mpaka leo sijajuaga nini ni nini , na sijajua nani mchawi au nani mwema kwenye hili.

Mara nasikia PAP , mara IPTL , mara sijui nn , yaani story kibao. Kwa ufupi tu sielewi kitu
Cha muhimu kujua ni kuwa, escrow ni Ufisadi wa Habinder Singh, Lugemalila na Serikali ya Tz. Lakini haya majina mara PAP mara IPTL. mara MEM mara MEMKWA mara Richmond mara Dowans, mara Hivi mara vile ni kutuvuruga tusijue. Tena JK analijua ipasavyo hili dili.
 
Hii nchi itamalizwa.!!
Bana wee
Wanaelewa kabisa mikataba ya kimataifa haivunjwagi ki holela holela kabisa kama vile mambo ya national house...
Na sheria zake always zina wa favor matajili
Inashangazaa xana issues ya symbion jamani
Let waiting for da next episode....
 
Back
Top Bottom