DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

Mbona Magufuli mambo mengi tu ambayo sio mamlaka yake kisheria ameyaingilia?

hili unataka kumsukumia lawama Dpp? unaogopa kumpa lawama Magufuli?

kweli tumbo si mchezo
Ulimpa za mbavu!!
 
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...
DPP anatoa vibali vya kushtaki kwa waliochunguza sasa hapo umemiksi konyagi ndogo na balimi
 
Ila mm hii ishu ya ESCROW huwa inanichanganya sana. Yaani mpaka leo sijajuaga nini ni nini , na sijajua nani mchawi au nani mwema kwenye hili.

Mara nasikia PAP , mara IPTL , mara sijui nn , yaani story kibao. Kwa ufupi tu sielewi kitu
Kakojoe ukalae
 
Unajifanya huijuia CCM na serikali yake!!
Mkuu huyu ni Magufuli jamani siyo kada wa CCM huyu kama kina Lowasa, Kikwete, Mkapa, huyu aliingia CCM kwa lengo moja tu la kumkomboa mwananchi lakini alicheza karata nzuri na uwezo wake wa akili ni mkubwa sana maana alijua kabisa kuwa akienda upinzani na katiba yetu hii hawezi kufika popote ataishia kupigwa virungu tu. Mbona wapo waliojaribu kwa nia nzuri tu kama kina Mtikila walishindwa pamoja na kwamba hawakuwahi kuwa CCM.

Mpeni muda atawashangaza ninyi wengi.....
 
Amekumbwa na 'politics of the stomach'
hana ujanja
sasa inakubidi umuombe msamaha MM maana ninyi watu walijazwa na hasira za kukosa urais kwa Swaiba wenu ambaye mwanzoni alikua adui wenu mkawa mnaandika tu ili mjifurahishe kwa kuwatukana watu.
 
DPP ana ubavu wa kuwafungulia mashtaka marais wote wastaafu na kuanzisha impeachment process kwa rais Magufuli?

Haya mambo yamepita katika vikao vya cabinet.
Duh DPP kum impeach magufuli???? hivi unajua nani mwenye uwezo wa kum impeach rais? kweli hizi siasa za kuziangalia katika TV za wazungu zitatufikisha pabaya.
 
Back
Top Bottom