DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,250
Reaction score
44,579
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...
 
Mbona Magufuli mambo mengi tu ambayo sio mamlaka yake kisheria ameyaingilia?

hili unataka kumsukumia lawama Dpp? unaogopa kumpa lawama Magufuli?

kweli tumbo si mchezo
Tena kwa mbwembwe anashindwa kuingilia kati swala la bukoba alafu anaenda kuingilia mambo ya Gazeti la Uhuru uku akijua ile ni kampuni inatakiwa ijiendeshe kwa faida!!
 
Ila mm hii ishu ya ESCROW huwa inanichanganya sana. Yaani mpaka leo sijajuaga nini ni nini , na sijajua nani mchawi au nani mwema kwenye hili.

Mara nasikia PAP , mara IPTL , mara sijui nn , yaani story kibao. Kwa ufupi tu sielewi kitu
 
Watu wamepiga fedha nzuri sana , sasa wanajaribu kukwepa vihunzi.

Mimi nauliza , hawa wa HongKong wamefikaje hadi kuja kuwadai TANESCO?
Ina maana Tanesco walikuwa wanamlipa mtu mwingine Capacity charge bila kujua?
 
Mfupa wa kumshinda Fisi, paka ataishia kuutazama tu, hata kuunusa hataweza sembuse kuulamba.
Hii kitu ni nzito mnoo kwa utawala wowote chini ya CCM, kwa hii issue kumnyoshea kidole DPP itakuwa ni jambo la kumwonea tu, ni sawa na kumtoa kafala tu.

Hii ngoma hata Ngosha haiwezi aisee. Wewe subiri uone kama hata kama anaweza kusema neno.
IPTL ni kina kirefu sana.
 
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...

mlopokaji ajaribu na hapo kugusa aone nguvu ya mzee wa msoga, urafiki utafiaa hapo hahaaaaaaaaaaaaaa

kesi za kupambana na serikari mahakamani tamu sana
 
Back
Top Bottom