Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...
DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!
Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...