DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

Zile sifa zionekane kwenye mambo kama haya sasa lakini kusifia debe tupu lenye kelele za kufukuza mwizi haisaidii kitu.

Ni mpaka chama kongwe kitoke ndio utakuwa mwisho wa michezo kama hii.
[HASHTAG]#mabadilikomuhimu[/HASHTAG]
 
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...
Mimi ninachokijua serikali ya awamu ya 5 chini ya MAGUFULI ni serikali imara na inayojali maslahi ya wanyonge hivo hili ni suala Dogo sanaa kwa mkulu! Na litashughulikiwa vizuri sanaaa
 
Singasinga japo anaonekana kuwa kinara wa sakata hili,yawezekana yeye alitangulizwa mbele tu ili kuwakinga vigogo waliopo nyuma ya sakata zima.Kama kweli mabilioni yale yaliyokwapuliwa na kugawanywa kama pilau la shughulini hadharani kisha kupakiwa kwenye mifuko ya Rambo na sandarusi yangekuwa hayana uhusiano na vigogo,tungekuwa tumeshawafahamu wote waliogawana hayo mabilioni pale Stanbic.
 
Kama Magu atataka kujaribu kuicheza hii ngoma ya IPTL basi awape huo uwanja UKAWA, aruhusu tu wafanye siasa zao kwa uhuru, kwa gear hiyo ataweza kupenya na kupambana na IPTL.

Tofauti na hapo, ataishia kujikaanga kwa mafuta yake.

Hapo umenena .Ngoma nzito hii ndani ya chama.Kukata tawi uliokalia unahitaji Moyo ya chuma.
 
Mzee mwanakijiji umetoka speed kwenye ule uzi umeamua kuanzisha wakwako kabisa. kwa taarifa yako kwenye hili la IPTL hapo ndio utajua ili hadithi unayoaminishwa kwamba watu wanapambana na mafisadi basi ni vidagaa tu ndio wanaobanwa. Muda ndio utasema.
 
Hilo sakata la IPTL ni jini kwa watanzania mim bado namini serikali ya ccm haipo tayari kuona madudu haya yanayo litafuna taifa kuayaondoa coz ni wanufaika na haya madudu yanayo liumiza taifa ccm hamuwezi kubadilika coz siasa za hoja mnaziogopa ndiomana yana wakuta mambo haya ya escrow mmebaki na mfumo wa kulindana taifa halisongi mbele hela za kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo tunaenda kuwalipa matapeli
 
Tusubiri new episody kwa hili nalo! Masikini watabanwa vilivyo n deni litalipwa tu tutake tusitake na hakuna wa kuguswa! Acheni wastaafu wapumzike! Atabeba mizigo yote yeye....
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...
 
Mimi ninachokijua serikali ya awamu ya 5 chini ya MAGUFULI ni serikali imara na inayojali maslahi ya wanyonge hivo hili ni suala Dogo sanaa kwa mkulu! Na litashughulikiwa vizuri sanaaa
Nadhani Lugumilization ilikuwa ndogo ya hii sasa sijui kama ataitumbuaga bana.
 
Waliokula dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani (mahakama mpya)
 
DPP anareport ya CAG,na report ya PIC na PAC afanye kazi awapeleke hao walijigawia hela ya Umma mbele ya mahakama sheria ichukue mkondo wake
 
Naona unaamisha magoli kutoka kwa mkulu mpaka kwa DPP.
Waliopewa hela wanajulikana,report ya CAG wanayo.
 
Back
Top Bottom