DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

DPP Biswalo Mganga Afanye Kweli Sakata la IPTL

CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...
Wewe nawe unatukumbusha maumivu tunayotaka kuyasahau ingawa hayasahauliki. Bingwa wa sheria Mwakyembe pamoja na Mwanasheria Sita walituaminisha kuwa dowans haiwezi kulipwa kwa sababu ni mkataba wa kifisadi lakini mwisho wa siku tumeambiwa tuilipe dowans mpaka senti ya mwisho. Kwa kuwa wewe ni mpingaji ufisadi mwambie Raisi alishughulikie suala hili na wala si DPP. Hakika hili litapita kwa kulipa deni lote kama ilivyoamriwa. Ufisadi ni mfumo na kuutumikia hatuna budi, mengine yote ni mikwara tu ili kuganga njaa.
 
Ila mm hii ishu ya ESCROW huwa inanichanganya sana. Yaani mpaka leo sijajuaga nini ni nini , na sijajua nani mchawi au nani mwema kwenye hili.

Mara nasikia PAP , mara IPTL , mara sijui nn , yaani story kibao. Kwa ufupi tu sielewi kitu

😡😡😡 Lengo lao mojawapo ndio hilo la kuchanganya baadhi ya watu.
 
Kumbuka Chenge ndiye alikua mshauri wa PAP katika kufanikisha deal

Mshirika kwenye kuuibia umma wa Tanzania. Halafu ndiye mwenyekiti wa bunge letu. Duh! JPM upo, embu tumia taasisi yako kutoa hawa watu? Kwanza fomu za maadili na mali zao wamezijaza?
 
sizungumzii hilo, nasema Mwakyembe ndie aliesoma ripoti ya richmond na akasem kuna mambo wameacha ili kuiokoa serekali. Hata hilo lingine huyo mbunge alishindwa kujieleza tu.
Hivi mkuu unashindwaje kujielezea kitu kama una uhakika nacho na una data kama si propaganda za kupeana na kusoma magazeti ya udaku!
 
Unajifanya huijuia CCM na serikali yake!!
Ndio maana nilisoma sehemu moja kwamba tukubaliane kama taifa na hii kesi wapewe akina Kibatala, Lissu na wenzao alafu ndio tutajua maana ya sheria na kanuni zake.
Nilivyounganisha dots na kujiuliza kama kweli watu wale wale waliokataa kutoa msamaha wa kodi kwenye kuingiza nchini mashine za kubadilisha taka za Dar es Salaam kuwa mbolea wanaweza kuwa na dhamira ya kushinda kesi kama hizi ...sijatoa machozi lakini nimelia!
 
Wizi na uporaji wa aina hii utaendelea kufanyika bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa so long as CCM iko madarakani na katiba iliyopo inaendelea kutumika. Ikumbukwe kuwa kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, CCM kilikuwa ni chama dola rasmi chenye mtandao mpana nchi nzima 'parallel' na ule wa serikali. Mzigo mkubwa wa kuendesha CCM ulikuwa unabebwa 100% na Hazina. Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa, CCM kikaendelea na mfumo wake na ukubwa ule ule; lakini sasa kwa vile sio tena chama dola kisheria na hivyo hakipati tena fedha kutoka bajeti ya serikali (mbali na ruzuku), na zingatia kuwa gharama za uchaguzi zimepaa; hilo pengo la kimapato linazibwa kwa kupitia vitendo vya kifisadi kama huu wizi wa Tegeta Escrow. Hivyo kiuhalisia, CCM ni taasisi ya kihalifu yenye vigogo ambao kazi yao ni kubuni na kuratibu dili za kuliibia taifa. CCM ni kupe anayeishi kwa kunyonya damu ya Watanzania, ndio maana itikadi yake pekee ni kuendelea kubaki madarakani kwa gharama yoyote na kupinga katiba ya wananchi.

...😱😱😱...kweli tupu.
 
Mara matajiri wameficha hela majumbani wakati escroooo walibeba kwenye magunia
 
Leo la DPP,Je DPP anateuliwa na nani?Nchi iko chini ya Rais aamue moja tu halipi au analipa
 
tusijisahau sana..........remote iko kwa mtuk.fu malaika,..ambaye yeye ndie mahakama,bunge na serikali kuu
 
Hivi mkuu unashindwaje kujielezea kitu kama una uhakika nacho na una data kama si propaganda za kupeana na kusoma magazeti ya udaku![/QUOTE
Kuwa na data na uwezo wa kujieleza ni vitu viwilo tofauti. watu wangapi wanafungwa kwa kuwa na uwezo mdogo wa kujieleza hata kama.si wakosaji?
 
Wewe nawe unatukumbusha maumivu tunayotaka kuyasahau ingawa hayasahauliki. Bingwa wa sheria Mwakyembe pamoja na Mwanasheria Sita walituaminisha kuwa dowans haiwezi kulipwa kwa sababu ni mkataba wa kifisadi lakini mwisho wa siku tumeambiwa tuilipe dowans mpaka senti ya mwisho. Kwa kuwa wewe ni mpingaji ufisadi mwambie Raisi alishughulikie suala hili na wala si DPP. Hakika hili litapita kwa kulipa deni lote kama ilivyoamriwa. Ufisadi ni mfumo na kuutumikia hatuna budi, mengine yote ni mikwara tu ili kuganga njaa.

Sasa mkimtaka Rais aingilie kisheria hivi au kutumia madaraka si ndio tena mtaibuka na kumuita "dikteta uchwara".. kwamba haheshimu utawala wa sheria?
 
Hivi tutaendelea kuorodhesha kashfa za wizi na ufisadi hadi lini??
 
Sasa mkimtaka Rais aingilie kisheria hivi au kutumia madaraka si ndio tena mtaibuka na kumuita "dikteta uchwara".. kwamba haheshimu utawala wa sheria?
Mkuu hapa kuna hoja zipatazo nne
1. Kuingilia hakuna maana afikishe wahusika mahakamani.
Ni yeye amwelekeze DPP kuchukua hatua.

Tunajua DPP ni wajibu wake, lakini kwa set up ya system yetu hawezi.

Nilitoa mfano wa msajili wa vyama aliyeshindwa kutafsiri sheria alizo nazo kuhusu mikutano hadi 2020 ''akichelea'' kuudhi watu.

2. DPP hawajibiki kwetu wala chombo chochote.
Tunawezaje kumwekea shinikizo?

Huyu kateuliwa na Rais na anawajibika kwake, kutushawishi sisi ni kututaka tumwekee shinikizo tukiwa hatuna 'uhusiano' naye kikazi

3. Tatizo linalomkumba DPP na wahusika wengine ni zao la mfumo mbaya.

Laiti DPP angewajibika kwa chombo kingine tusingebabaika namna ya kuweka shinikizo kwa mtu asiyetuhusu

4. Kama tulishindwa kumwekea shinikizo Naibu Spika atoe taarifa ya bunge kuhusu Lugumi , bunge linawajibika kwetu, tunawezaje kumwekea shinikizo DPP tusiye na uhusiano naye isipokuwa mahakamani tu?

Tunaposema mfumo mbaya, waliotubeza sasa wanatuelewa.
 
Mbona Magufuli mambo mengi tu aJpm.h sio mamlaka yake kisheria ameyaingilia?

hili unataka kumsukumia lawama Dpp? unaogopa kumpa lawama Magufuli?

kweli tumbo si mchezo
Huyu Mzee nilishamzarau alitumika km Condom sasa njaa inamfanya aogope kumtaja Jpm.
 
Hivi tutaendelea kuorodhesha kashfa za wizi na ufisadi hadi lini??
Hadi tutakapokaa chini na kubadili mfumo ili kila mtu awajibike

Hadi tutakapokaa chini kuondoa bureaucracy ya mtu mmoja kubeba sheria zote

Na hili walijua , wakakataa rasimu ya Warioba, at least ilijaribu kuonyesha njia.

Waliokataa wanatumia mbinu zile zile kufunika uozo wakituaminisha tunakwenda vema.

Mfumo wetu ni mbaya sana, hili watu wanalikataa lakini taratibu wanatuelewa

Tulisema kutumbua majipu ni kutumia asprin kwa maumivu si kutibu.

Kama tunatibu, iweje makosa yale yale yanayofanywa na serikali ya chama kile kile kwa miaka 50 yanajirudia kwa mtindo ule ule na watu wale wale?
 
unataka kushindana na wamiliki wa mabilioni kwa mawakili wanaoshindana kupanda mabasi ya mwendo kasi. jamani mtawazeesha watoto wa wenzenu. iulizeni serikali imeipatia ofisi ya dpp kiasi mwaka huu, naamini utapata jibu. mwanakijiji tupe jibu
 
CX4jjMBWMAI-sIe.jpg

Juu IPTL - Baada ya Tanesco kuamriwa kuilipa IPTL mabilioni ya shilingi kufuatia kushindwa kwake kesi mahakama ya Word Bank (usuluhishi wa Biashara), na kwa vile sote tunajua fedha zile za kwenye akaunti ya escrow hazikupaswa kulipwa mtu mwingine yeyote basi ni wakati wa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuandaa mashtaka na kuagiza wahusika wote waliokuwa dili la escrow wakamatwe na wafikishwe mahakamani huku kumtaka Singasinga wa PAP kurudisha fedha zote alizopokea chini ya tishio la kufisiliwa mali zake zote hadi kulipa deni hilo...

DPP aangalie sheria zinamtaka afanye nini kuhakikisha kuwa Wananchi wa Tanzania hawalipi deni mara mbili sababu ya uzembe wa watu fulani serikalini... Waliochukua hela za mboga wote wazirudishe!

Idara yake iko huru Kikatiba na Kisheria; hapaswi kumsubiri Magufuli kumuelekeza nini cha kufanya; afanye kile ambacho anajua ni kwa maslahi ya taifa. Kama anasubiri maelekezo toka "Ikulu" hapaswi kuendelea na wadhifa wake huo...Na kama anaona hana kitu chochote cha kufanya ni vizuri aseme wazi kuwa haoni namna yoyote ya kuwashughulikia wahalifu walioliingiza taifa kupitia ile kashfa ya Escrow...

IPTL ni kokoro....unalijua kokoro wewe?

kwa hiyo....si DPP wala bosi wake, wala bosi wa bosi wake atakayegusa hili dubwasha.
 
Back
Top Bottom