Download hapa katiba ya Chama Cha Kijamii (CCK)

Jan 29, 2012
39
38
Wana jamvi,baada ya kuweka tamko lililotolewa siku ya tarehe 27/01/2012 juu ya ujio wa CCK na wachangiaji wengi kuomba kupata nakala ya katiba ya Chama Cha Kijamii (CCK),kwa heshima na taadhima leo nawapeni katiba hii ambayo kwa kila hali inadai mabadiliko ya haja ya kijamii na kiuchumi katika nchi yetu,naomba kuwasilisha.
 

Attachments

  • KATIBA YA CHAMA CHA KIJAMII.doc
    272.5 KB · Views: 693
Joseph Zablon

IPO dhana kuwa nchini kuna utiriri wa vyama vya kisiasa hivyo hakuna haja ya kuanzishwa chama kipya, hoja ni kuwa vilivyopo vinatosha.

Tanzania inavyo vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu. Lakini bado vipo vingi vilivyowasilisha maombi na vingine vilivyopewa usajili wa muda.

Kuongezeka kwa idadi ya vyama vya siasa kunachangiwa na mifarakano inayoibuka katika vyama vyenye usajili ambapo baada ya kufarakana na kugawanyika huzaa makundi ambayo kutoka na kwenda kuanzisha vyama wanavyoviita vyao.

Chama cha Kijamii (CCK), ni chama kipya kilichopata usajili wa kudumu. Tofauti na vyama vingi vinavyoanzishwa kutokana na migogoro katika vyama vikubwa, hiki hakijazaliwa kutoka chama chochote kati ya 18 vilivyopo.

Mwenyekiti wa CCK Constastine Akitanda anasema bado Tanzania inahitaji kuwa na vyama vingi vya siasa ili wananchi wachague chama wanachokitaka.

Anasema chama hicho kimeanzishwa na wananchi wa kawaida na ni tofauti na vingine ambavyo vimezaliwa kufuatia kumeguka ama kuhitilafiana kwa viongozi wa vyama vingine.

Chama lazima kitoke kwa wanachama wenyewe na CCK ni chama cha wanachama na ni cha Watanzania, anasema Akitanda

Akitanda anasema licha ya kuwepo kwa utitiri wa vyama vya kisiasa nchini lakini CCK wana sababu tatu za msingi za kuanzisha chama hicho ambazo ni pamoja na ukweli kuwa nchini hakuna chama kingine cha upinzani chenye itikadi na msimamo kama CCK.

Anasema hadi sasa toka kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hakuna chama ambacho kinawaridhisha watanzania.

Mwenyekiti huyo kijana anasema ukweli wa jambo hilo unathibitishwa na mwenendo wa wananchi katika upigaji kura ambapo anadai kuwa walio wengi zoezi hilo wamelisusia na wamebaki kuwa wapiga kura wa kuangalia upepo wa kisiasa.

Sababu ya tatu anaitaja kuwa CCK ni chama ambacho kinaitikia changamoto za milenia mpya pamoja na vizazi vyake na kwamba ni chama kilichojipanga kukipokea kijiti CCM na wanaamini kuwa wana uungwaji mkono mkubwa na makundi ya vijana na wazee.

Akitanda anasema hata jina ambalo wamelichagua linaakisi makusudio ya chama chenyewe ya kuwa na mchango wa maana kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuinua hali za maisha ya watanzania wa kawaida, kujenga uchumi imara na shindani wenye kutoa fursa zawa za kufanyakazi na ajira kwa watu wake.

Tunaamini kuwa sera za chama kilichopo madarakani na hasa ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita zimekuwa kinyume na matarajio ya Watanzania walio wengi, anasema.

Anaendelea kusema kuwa kauli mbiu ya baada ya uhuru ni kuunda jamii ya watu walio sawa na huru dhana ambayo haijatimia na zaidi inatoweka.

Anasema watu ambao ni sawa na huru ni wachache tena ni wale ambao wana nguvu za fedha, ujanja wa kisiasa na madaraka na msukumo wa pamoja kama taifa wa kupigania jamii haupo tena na baadala yake kila mmoja anaangalia maslahi yake binafsi na wale ambao wamemzunguka.

"Msisitizo wa kupigania jamii yetu haupo tena na ndio maana tumeunda CCK ili kuziba huo ufa" anasema na kuongeza kuwa sera za chama hicho ni kujenga jamii ya kisasa ya watanzania yenye utu, heshima na mchango kwa taifa badala ya kuwa kama ilivyo sasa.

Anasema itikadi ya chama chao hicho ni uhafidhina wa kijamii na kiuchumi na msingi wa itikadi ya namna hiyo ni historia ya Taifa ambayo ni kujenga jamii iliyo sawa na haki ambapo serikali imekuwa na matumizi makubwa kuliko vipato vya wananchi wake.

CCK ni chama cha wananchi wote na sio kikundi fulani cha watu kama ilivyo kwa baadhi ya vyama, anasema Akitanda na kuongeza kuwa chama hicho kinataka kupendekeza sera ambazo zitakuwa na majibu tofauti na ilivyo sasa hususani katika suala la uchumi.

Anasema CCM imeshindwa kutengeza uchumi wa kisasa na badala yake umekuwa wa watu wachache ambao wananufaika huku wananchi wa kawaida hali zao zikizidi kuwa mbaya kwani mkazo kwa chama kilichopo madarakani ni kukopa badala ya kutafuta njia za uzalishaji.

Tumeshindwa kufuata dira za waasisi wa Taifa hili ambao ni Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, anasema Akitanda.

Anaongeza kuwa CCK itapitia njia walizopita waasisi hao ili kufikia malengo na matarajio ya Watanzania.

Akitanda anasema chama chake ambacho kimepata mapokezi mazuri toka kwa wanachama na watanzania kwa ujumla wake, anasema hakina uadui na chama kingine chochote cha upinzani na hasimu wao mkubwa ambaye ni wa kudumu ni CCM.

Hatuna urafiki na CCM na ni maadui zetu wakubwa lakini tupo tayari kuwa karibu na chama kingine chochote cha siasa ili mradi tuwe tunaafikiana katika masuala ya kisera, anasema.

Anasema miongoni mwa malengo ya chama chake ni kuona CCM ikidhoofu na hatimaye kutoweka katika ulimwengu wa kisiasa kutokana na mateso ambayo wameyasababisha kwa watanzania.

Anasema Chama chake kinatembea na kauli mbiu ya 'mabadiliko ni sasa, mabadiliko ni sisi'. Na kuwa katika kuihitimisha kaulimbiu hiyo, wapo tayari pia kumuunga mkono mgombea wa chama kingine endapo ataonekana kuleta mabadiliko.
 
nilikuwa mmoja kati ya watanzania wengi waliokuwa wanaisubiri kwa hamu katiba ya chama hiki,asanteni sana CCK kwa kutuletea na wengine tuliopo mbali na mako makuu
 
Kila mtu akitaka madaraka anatumia sentesi "tumaini/ matumaini mapya kwa watanzania" mwisho wa siku hakuna mabadiliko yeyote..kifupi ww na matapeli wenzio mnaoanzisha chama kipya ni wale wale tu!!!
 
acheni woga,swala hapa ni nani anaweza kuwatumikia watanzania kwa moyo wa kujitoa muhanga si kwa kukinga mikono na kutaraji kupata ruzuku inayotokana na kodi zetu,hongereni CCK kwa kukataa ruzuku
 
Asante nikipata muda nitaipitia vipi hamtoi sitting allowance.
 
Ngoja tuisome vizuri,sasa mkuu naomba ulijibu hili kwenye kituo kimoja wewe pamoja na katibu wako mlisema serikali ifute rudhuku kwenye chama,sasa we unafikiri vyama vitajiendeshaje? Si ndio vitakua mali zenu sasa?
 
Kitapata watu wakati wa kura za maoni, kwani watakaotoswa CCM na CDM wataingia CCK. Let keep an eye on this ...
 
safi sana tutajiunga kwa wingi kushinda CCM,CUF,CHADEMA na wengine

Husna naomba unitumie namba yako ya simu (Tongue in cheek). BTW hii CCK sio Prototype ya CCJ?

Serious kabla hata sijasoma katiba yenu (because most of katibas za vyama ni nzuri including our evil party CCM).
Mimi ninataka kufahamu msimamo wenu wakati huu tete wa kuandika katiba mpya.
  1. Muundo wa Muungano
  2. Madaraka ya Rais wa JMT
  3. Kuwepo/kutokuwepo kwa wabunge wa viti maalumu
  4. Kuwepo/kutokuwepo kwa RCs DCs
  5. Mameya wa majiji kuchaguliwa na madiwani
  6. Tume huru ya uchaguzi (muundo na upatikanaji wa wajumbe wake)
  7. Matokeo ya kura za Rais kutohojiwa na chombo chochote kile
  8. Wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri
  9. Uteuzi wa CJ, CDF, IGP, Wakuu wa mashirika nyeti ya umma kufanywa na Rais pasipo kuidhinishwa na chombo chombo chochote kile au nafasi hizo zitangazwe na kugombewa kulingana na qualification
  10. Muundo wa SMT kuwa na Rais, VP, PM ni sahihi
Ukinijibu haya machache labda yanaweza kunipatia/kutonipatia hamu ya kusoma katiba yenu.
 
CCK wanaonesha wana mbinu za kutumia mtandao, maana wewe inaonesha utakuwa mpiga debe wao mkubwa. Kwakwakwa. Hongera, lakini hao ni pumba tu hawana lolote jipya, CCJ sasa CCK ikishadondokea puwa kutakuwa na CCL.

Katiba yao itatusaidia nini?

Chama cha mapacha watatu nini? Yaani wale wengine.
 
wana jamvi,baada ya kuweka tamko lililotolewa siku ya tarehe 27/01/2012 juu ya ujio wa cck na wachangiaji wengi kuomba kupata nakala ya katiba ya chama cha kijamii (cck),kwa heshima na taadhima leo nawapeni katiba hii ambayo kwa kila hali inadai mabadiliko ya haja ya kijamii na kiuchumi katika nchi yetu,naomba kuwasilisha.

katiba cck:

Nimeisoma na kujaribu kuichambua katiba ya cck lakini imekosa jambo moja muhimi, haikutaja sera/msimamo wake kamili kuhusu muungano.

Katika siasa za tanzania, suala la kujua msimamo au sera kuhusu muungano ni jambo la lazima laini cck imejaribu kulikwepa sijui wana nia gani.

Cuf, chademe msimamo wao ni serikali tatu (3) ccm msimamo wao ni serikali mbili.

Kwa hiyo tunataka tujue nyinyi cck msimamo wenu kuhusu muungano ni upi?

Naomba jibu tafadhali viongozi wa cck, au kama mumeutaja kwenye hiyo katiba sikuufahamu si vibaya mukawa wawazi.

Naomba kuwasilisha, nikijua msimamo nitafanya maamuzi.
 
Wana jamvi,baada ya kuweka tamko lililotolewa siku ya tarehe 27/01/2012 juu ya ujio wa CCK na wachangiaji wengi kuomba kupata nakala ya katiba ya Chama Cha Kijamii (CCK),kwa heshima na taadhima leo nawapeni katiba hii ambayo kwa kila hali inadai mabadiliko ya haja ya kijamii na kiuchumi katika nchi yetu,naomba kuwasilisha.
Usife moyo kutokana na kauli za ovyo ovyo za baadhi ya watu humu JF kwani uanachama wa JF hauna mchujo. Watu wenye akili timamu wanatakiwa kukupinga kwa hoja, sio kejeli na matusi.

Lakini pia jitahidi sana kujibu hoja za msingi zinazotolewa humu, la sivyo jitihada zako humu hazitazaa matunda.

Vinginevyo umefanya jambo la maana sana. Hongera na kila la kheri.
 
Wabongo bwana, yaani tumeshindwa kuvipa nguvu vyama vilivyopo tunang'ang'ania kuanzisha vipya? Demokrasia hailetwi na wingi wa vyama vya siasa bali uimara wa vichache vilivyopo. Utitiri kama huu nauona kama evidence ya UBINAFSI!
 
Back
Top Bottom